Dhibiti hasira yako kuepusha matatizo na walimwengu

Dhibiti hasira yako kuepusha matatizo na walimwengu

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
2,912
Reaction score
12,904
Habari jamiiforum

HASIRA ni nini?

Hasira ni Ono linalompata kiumbe yeyote yule, binadamu ,mnyama mdudu au ndege pindi anapokutana na pingamizi.{credit na Wikipedia}

Leo tuangalie Kwa binadamu madhara ya hasira na hatua za kuchukua.

Maudhi yapo kila siku,kila saa na kila muda ,ni wewe tu kuamua kupuuzia ,

Mume au mke nyumbani atakuudhi.
Boss au mfanyakazi ofisini atakuudhi.
Bodaboda barabarani atakuudhi,na vingine vingi vyenye kuleta matata ili tu uishie pabaya.

Kwa mujibu wa maandiko kwenye vitabu vitakatifu hususani biblia imeandikwa ,

Hasira hukaa kifuani mwq mtu mpumbavu.
Sasa kwanini uwe kwenye kundi la watu wapumbavu? Kumbuka hasira inaweza kufanya ukafukuzwa kazi,kufungwa jela,kuuwawa na kushusha heshima yako

Chukua hatua hizi ili usiruhusu hasira ya mapema .

1.Jifunze kuchukua sekunde 30 hadi 45 kabla hujazungumza

hii itakufanya kubadili uelekeo wa maneno kabla hujaharibu. Kuongea fasta hutengeneza malumbano na matatizo kisa kuropoka bila kufikiri.

2.Sikiliza kabla ya kutoa maamuzi.

Ni kweli mwanao,au rafiki yako alikuazima chombo ,lakini baadaye anarudisha kikiwa kimeharibika vibaya,cha kufanya mpe nafasi ajieleze ,huu muda anaotumia kujieleza unaweza kushusha hasira yako hata kama maelezo hayana mantiki.

3.Jifunze kupuuza .

Boss atakufokea Kwa mambo ambayo hujafanya,mkeo atajiamini Kwa kuongea shombo bila adabu,
Mtu aliyekwangua rangi ya Gari yako Kwa kuovertake vibaya,ataongea shombo ili tu uonekane mwenye makosa.

Tulia,muone kama mjinga subiri sheria ifuate mkondo.

4.Thibiti hisia zako

Unatoka zako huku ,mara unakuta watu wanapiga mwizi,sasa kwakuwa na wewe ni siku chache zimepita umetoka kuibiwa,basi unaungana na watu unaanza kupiga yule mtu, kumbe kafananishwa au kaitiwa kelele ya mwizi na demu wake.

5.Ongea taratibu (kwa tuo)

Kuongeza haraka bila mpangilio kutafanya watu wakujibu vibaya,Hali itakayoamsha hasira zako,hivyo kuongea kwa utaratibu kutakufanya unaojibizana nao ,nao waongee kistaarabu.

6.Epuka mabishano.

Mnaanza Kwa kutaniana habari za siasa au za mpira ,mwisho siku mwingine akiishiwa hoja anakutukana tusi la nguoni.

Mfano ni Mimi mwenyewe, niliwahi kubishana na mtu kuhusu timu ya Yanga kubeba ubingwa mara tatu mfululizo,sasa baada ya opponent wangu kuishiwa hoja akadai Kwanza habari za Simba na Yanga zinasaidia nini ,Mimi Daniel ningekuwa na akili ningekuwa napanda daladala?

Aisee hii ilinigusa vilivyo hali iliyopelekea kushikana mashati.

7.Epuka kutumia lugha za matusi.

Utatukana ndiyo,lakini
Kuna watu wanajua kutukana na kuudhi hivyo tusi utakalopewa likikosa comeback unaweza okota jiwe ukamrushia mtu. Kuna jamaa aliamua kumtimua demu wake kisa ni Malaya,watu tukajaa kusikiliza kulikoni wapendanao kutimuana.

Mwanaume akatamka mbele za watu kwamba mwanamke Yule ni tasa hawezi kuzaa hivyo hawezi kuishi na mti usio wa mbao,matunda wala kuni.

Mwanamke naye akajibu yeye hana tatizo hilo ila asisahau kuwa yeye mwenyewe (yaani mumewe) ana bwana wake anayemfi*** na ndiyo maana hana shughuli zote na maisha Yao yanaenda.aisee mjuba alikuwa tayari kuua huku akiliq kama mtoto mdogo ,kumbuka watu zaidi ya thelathini,wapo watasema huenda si kweli,wapo watakaosema lisemwalo lipo.

8.Ishi kikawaida,usiruhusu dharau,au ujinga eti kuepusha Shari wewe siyo mjinga.
 
Bora uwaambie wasije wakaribu wakaja huku chuo cha urekebishaji maana huku tutawafundisha kuzituliza hasira kwa lazima
 
Back
Top Bottom