Dhibiti matumizi ya sukari za nyongeza ili uimarishe afya yako

Dhibiti matumizi ya sukari za nyongeza ili uimarishe afya yako

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Changamoto za kiafya huja kwenye nyakati tunazotumia sukari nyingi za nyongeza, ambazo wazalishaji wa vyakula na vinywaji viwandani huiongeza ili kuboredha (kuongeza) ladha.

6AF0D34F-D02C-49D1-98CE-C652C7A4EBBC.jpeg

Aina hii ya sukari ni hatari kwa afya ambapo tafiti za kisayansi huihusisha na mambo yafuatayo-
  • Kuongezeka kwa uzito wa mwili
  • Kuharibika (kuoza) kwa meno
  • Huongeza nafasi ya kuugua magonjwa sugu hasa yale ya moyo na mfumo wa damu, kisukari, saratani pamoja na figo
  • Huhusishwa na kusababisha kuzeeka haraka kwa ngozi pamoja na kutokea kwa chunusi
Vyakula vyote vyenye asili ya wanga (Carbohydrates) kama vile matunda, mboga za majani, nafaka na bidhaa za maziwa huwa na sukari za asili ambazo ni salama kwa afya.

Pia, mmeng’enyo wa vyakula vyenye asili hii hufanyika taratibu hivyo sukari zake hutoa uhakika wa upatikanaji wa nishati inayohitajika kwenye seli za mwili ili kudumisha uhai.

Chanzo: Harvard Medical School
 
Back
Top Bottom