Dhiki yetu, Faraja yetu 2025

Dhiki yetu, Faraja yetu 2025

Ngetyo

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2024
Posts
268
Reaction score
403
Wakuu salaam kwenu!

Kuelekea 2025
Kumekuwa na tabia ya baadhi ya Wabunge kuhama makazi yao baada ya kuchaguliwa na kuwa Mbunge.
Wakati wote mtu alikuwa mkazi wa Jimbo X, anaomba ridhaa kupitia jimbo hilo X, wananchi wanamchagua awe Mbunge wao wa Jimbo X.
Baada ya kuapishwa yeye na familia yake wanahamia Dares Salaam, jimboni anaenda Sikukuu hadi Sikukuu.
Baada ya miaka minne wa tano mwanzoni anaanza kwenda mara kwa mara na kuhani misiba huku akitoa misaada kadhaa.
Hali hii hufanya wananchi kukosa huduma stahiki kutoka kwa mwakilishi wao, hivyo nashauri vyama vyote vya siasa kuhimiza Wagombea/Wabunge wao kuendelea kukaa na wananchi wao hata baada ya kuchaguliwa ili wajue uhalisia wa matatizo na mahitaji ya wananchi wao.
Aidha wananchi wawapime wagombea kwa uwezo wao wa kuwahudumia siyo kwa zawadi za muda mfupi wanazotoa baadhi yao.
Vijana wajitokeze kujiandikisha na kupiga kura, maamuzi ni kwenye sanduku la kura siyo kusubiri kulalamika.
Nawasilisha asante sana, karibuni.
 
Back
Top Bottom