Dhumuni kuu la NASA kutuma keppler telescope Kwenye Anga ni lipi hasa?

Kuhusu Darwin 4 sikufuatilia, lakini Kama ni moja ya hizo exoplanet hiyo basi hilo linawezekana kwa sababu mpaka sasa kuna sayari zaidi ya 1000 ambazo ni earth like.
Kuhusu telescope hiyo kuzidetect hizo sayari unapaswa uwelewe muundo wa hiyo Kepler yenyewe ilivyoundwa unaweza tafuta mwenyewe mi nitaeleza kwa jinsi ninavyoelewa kwa kifupi.
Kepler ina image sensor ambazo in pixels zake zinafikia 95m halafu kuna mirror inaitwa primary mirror ambayo imetengenezwa kwa glasi ambazo ni utra low expansion, sasa basi ili kuwa na sensitivity kubwa kuzigundua hizo sayari ni pale ambapo zinapita mbele ya hiyo nyota husika hivyo imewabidi ile primary mirror waivalishe kitu kinaitwa reflectance coating ili kuwa na uwezo mkubwa wa kusense hivyo kwa msaada wa ion assisted evaporation pia na surface optic Corp inakuwa ni rahisi kuweza kudetect hizo sayari. Basi mi sijaelewa unaposema kwamba ni ngumu kudetermine sayari zilizo karibu na nyota.
 
Asante mkuu nilifanikiwa kimtindo!
 
Kwa hiyo uliishia njiani au bado unafuatilia?

Asante nimepata somo hapa ,ila nimefikiria kama watagundua Sayari nyingine zinazoruhusu viumbe kuweza kuishi nikafikiri umbali wa kuzifikia nikalinganisa na umri wa binadamu kuishi nikakwama..Hebu tusaidie pia ugunduzi wa Sayari hizi utaisaidiaje Dunia !.Au tutabaki na kumbukumbu tu au kwa namna ipi!..

Tusaidie Mkuu ,kwa uelewa wako...
 
Madhumuni yanaweza yakawa mengi moja wapo hata uwezekano wa kuishi huko lakini Kama ulivyosema kwa teknolojia ya sasa hakuna uwezekano wa kufanya safari za interstellar yaani kutoka solar system hii na kwenda nyingine maana hapo mars tu ambapo ni jirani mpaka sasa bado ni shughuli kupeleka watu. Kuna nadharia ya kutumia shortcut kufika kwenye galaxy nyingine kwa kutumia wormhole kuunganisha black holes za galaxy swala la ambalo liko na ugumu mno na linaweza hata lisiwezakabike. Kwa hiyo kwenye kufanya hizo tafiti wanaweza wakagundua vitu vingine zaidi ambavyo vina manufaa na dunia mfano tu ugunduzi wa hivi karibuni kulithibitisha uwepo wa gravitational waves na wakadai huko mbeleni wanaweza tumia hizi kwa ajili wa mawasiliano hasa anga za mbali.
 

Mkuu.nitangulize Shukrani kwa kujibu kwa wakati, asante sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…