Dhumuni kuu ni kupambana na umaskini bila kuvunja sheria za nchi

Kibundi wa getto

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2013
Posts
455
Reaction score
877
Wakuu Leo na Mimi ngoja niongee kidogo.


Umaskini ni kitu kibaya sana duniani.Umaskini unasababisha kumkufuru mwenyezi mungu mara kwa mara,hata kwenye vitabu vya mungu umaskini umepigwa vita sana.

Maisha yanabadilika kila kukicha,upatikanaji wa fursa unabadilika kila siku.Kuna fursa ambazo zamani zilikua zinatoa kipato kikubwa lakini sasa hivi kipato ni kidogo sana.Kuna aina ya utaftaji zamani ilikua inalipa lakini sasahivi hupati kitu.

Duniani kila mtu anapenda utajiri lakini tatizo ni jinsi gani ya kuufikia huo utajiri,na hii ndio sababu maskini ni wengi zaidi kuliko matajiri.Ili uwe tajiri ni lazima ufanye kitu ambacho kwa walio wengi sio rahisi kufanya hicho ambacho unataka kufanya wewe.

Kuna matajiri,watu wa kati na maskini.Duniani watu wengi ni watu wa kati,kisha wanafatia maskini na mwisho kwa idadi ni matajiri.Kila mtu ana ndoto zake apa duniani,wengine ndoto zao huishia njiani ama kwa kutojituma,kutokutambua nini wafanye au kuridhika na pale walipo.

Sasa basi lengo la kufungua Uzi huu ni kuwakumbusha kuwa umaskini ni kitu kibaya sana na kina madhara makubwa sana apa duniani.

NINI KIFANYIKE

(1) Kila mtu aangalie fursa iliyopo mbele yake, uhakikishe kila fursa unayohisi inatija kwako usiiache iende bure ilihali auvunji sheria za nchi.

(2) Duniani binadamu uwa tunapokea ushauri kwa mtu ambaye amefanikiwa katika icho unachoomba ushauriwe.

(3)Duniani hakuna njia sahihi ya kuwa tajiri,bali ni akili yako na uvumilivu tuu.

(4)Hakuna pesa rahisi duniani,lazima upambane sana,uwe mvumilivu,uwe Mwenye nia na ukubali kuzaraulika.

(5)Lazima ufeli sana ili uje kufanikiwa,pesa nyepesi huondoka haraka na pesa ya jasho hutunzwa kwa heshima.

MWISHO

Usiogope kupoteza,lazima ukubali kupoteza sana ili uje upate kilicho sahihi.

Take Risky....take risky....take risky.

Uoga wako ndio umaskini wako.
 
Asante kwa ushauri,Mkuu...
 
Kuna hekima nyingi kwenye haya maandishi,ila wapumbavu wa kupinga lazima watokee.
 
Hahahaaa ngoja wafuasi waje, Ni kweli unacho sema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…