Diamond achezea kichapo iringa.

ramson34

Senior Member
Joined
Oct 29, 2009
Posts
109
Reaction score
4
DJ Muba ni DJ maarufu anayetikisa mkoa wa Iringa na Tanzania ila ni DJ mpole aliyetaka kuzichapa na msanii chipukizi Diamond











Mshindi wa tuzo za Kilimanjaro 2010 Diamond (jukwani )akiwajibika katika jukwaa la Voda com Miss Iringa kabla ya kupokea kichapo nje ya ukumbi wa st.dominic Iringa baada ya kutaka kumpiga DJ Muba na msanii wa vichekesho Athuman Mussa a.k.a Mwalubadu .







Diamond alifikia hatua hiyo ya kufanya fujo kubwa katika ukumbi huo baada ya kumaliza kuimba na kushuka jukwani na akiwa nje ya ukumbi huo alimtukana matusi ya nguoni kwa kutumia ishara ya kidole Mbarouk Salum maarufu kama DJ Muba ambaye alikuwa akipinga muziki katika ukumbi huo .







Hatua ya msanii huyu kumtukana DJ Muba ilionyesha kuwakwaza mashabiki wa DJ huyo ambao wamekuwa wakimtegemea katika tasnia ya burudani ndani ya mkoa wa Iringa kwa kupitia kituo cha Radio Ebony Fm na ukumbi wa club V.I.P wa mjini hapo hali iliyopelekea mashabi hao kuanza kumshambulia msanii huyo Diamond kwa kumwita mchanga sana katika sanaa hiyo na kuwa tuzo ya Kilimanjaro isimfanye matawi ya juu pamoja na kumweleza ukweli kuwa DJ Muba ni maarufu mara 100 kwake hivyo asitake kujifanyanisha na DJ huyo kauli zilizomkwaza msanii huyo Diamond.
 
Kumbe hajachapwa...., matusi ndio salamu mkuu siku hizi.
 
arghhhhhhhhhhhhhh!

Mnatuchafulia jina la Iringa nyie wote na mleta maada!
 
Habari hii ni ya uwongo....Diamond mwenyewe amepinga habari hizo (source clouds fm)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…