Diamond aeleza jinsi alivyokutana na Don Jazzy na kushiriki katika wimbo wao

Diamond aeleza jinsi alivyokutana na Don Jazzy na kushiriki katika wimbo wao

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304

“Wakati nipo Nigeria nimebakiza siku moja kurudi wakaniemail wakaniambia ‘Mavin Records, Don Jazzy na Dr Sid wangependa kufanya kazi na wewe kama bado upo Nigeria,” Diamond ameiambia Bongo5. “Niliona ni jambo zuri kufanya kwasababu Don Jazzy ni mtu mkubwa na ukiangalia industry ya muziki ni mtu ambaye ana sehemu yake. So nikakaa na uongozi wangu nikawaambia ‘nimepata email kutoka kwa Don Jazzy anasema anapenda kufanya kazi na sisi. Basi nikawa link na menejimenti yangu wakazungumza wakapanga vitu vyote vinavyotakiwa tukaenda tukafanya,” ameongeza.

Amesema katika wimbo huo wa Dr Sid, Don Jazzy ambaye ndiye producer naye ameweka sauti yake. Hata hivyo Diamond amesema wimbo alioshirikishwa na Waje ndio alioupenda zaidi na kwamba utakuwa moto wa kuotea mbali.
 
Hayaaa twasubiriiii sier vitu motomoto halaf HOD kapotelea kwenye ndege ya Malaysia etii maana haji kutupa habariii halaf pia akachangamsha na jukwaa
 
Hayaaa twasubiriiii sier vitu motomoto halaf HOD kapotelea kwenye ndege ya Malaysia etii maana haji kutupa habariii halaf pia akachangamsha na jukwaa

Almasi anaandamana na HOD ziara za hapa hapa nyumbni kwenye nchi ya madafu.
 
Back
Top Bottom