Diamond aelezea jina la "Diamond Platnumz" lilivyotokea

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Diamond Platnumz ni mmoja wa wasanii wakubwa barani Afrika kwa sasa. Siku za hivi karibuni alipata nafasi ya kushiriki tamasha la muziki la Coke Studio Afrika kusini ambapo alitengeneza wimbo uliowavutia wengi kwa kushirikiana na Cassper Nyovest, wimbo unaitwa My Heart.

Akiwa katika tamasha hilo alifanya mahojiano na waandaaji na moja ya yaliyowavutia wengie ni alipoeleza jinsi alipopata jina lake la sanaa ‘Diamond Platnumz.’

Akielezea chanzo cha jina hilo, Naseeb Abdul Juma alisema kuwa jina hilo lilianza kitambo alipokuwa akiimba ambapo rafiki zake mtaani walikuwa wakimwambia kuwa yeye ana kipaji kizuri cha kuimba na siku akipata mtu wa kukiendeleza, ataweza kuwa mwenye thamani kama Diamond.

Alieleza kuwa katika kipindi hicho walianza kumuita jina hilo la Diamond na kwavile hapakuwepo na msanii yeyote anayetumia jina hilo, akawaza kwanini asilitumie. Ndipo na yeye akaaza kujiita Diamond.

Akifafanua lilipotekea jina Platnumz, Naseeb alisema kuwa neno hilo lina maanisha mtu mtanashati mwenye swaga, mwenye muonekano wa kuvutia na mtu wakupendeza kila mara. Hivyo akajiita Diamond Platnumz na ukawa ndio mwanzo wa jina lake hilo.
 

Safi jina amelitendea hali go shibu dangote simba
 
Na Dangote, chibu, simba
Dangote ni Alike Dangote tajiri namba moja wa afrika...alijiita hivyo kwa kujifananisha nae.

Chibu ni kifupi cha jina lake halisi Nasibu.

Simba ni Simba mnyama mwenye nguvu na mtemi Porini.
 
weka pichaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…