Diamond afafanua ishu ya Mbosso kuondoka WCB

Diamond afafanua ishu ya Mbosso kuondoka WCB

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mwanamuziki na mmiliki wa Lebo ya WCB, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefafanua taarifa za msanii wake Mbwana Kilungi maarufu ‘Mbosso’ kuondoka kwenye lebo hiyo, huku akisema yeye ndiye mtoa tamko wa lebo hiyo.
IMG_2925.jpeg

Soma: Baba Levo atangaza Mbosso kuondoka WCB Wasafi na uamuzi wa Diamond

Kupitia ukurasa wake wa Instagram leo Februari 4, 2025 Diamond amesema kuwa tayari wamekamilisha mazungumzo na Mbosso kuhusu namna nzuri ya kusimamia kazi zake hivyo kwa sasa taarifa yoyote inayozungumzia jambo hilo ipuuzwe.

"Tumekuwa na mazungumzo mazuri sana na Mbosso namna ya kuanza rasmi sasa kusimamia kazi zake na tumekamilisha jambo letu vizuri sana. Tafadhali story yoyote inayozungumzwa kuhusu jambo hili la Mbosso naomba zipuuzwe mpaka mimi binafsi na Mbosso tutakapotoa tamko rasmi," ameeleza Diamond.

Utakumbua taarifa hiyo imekuja kufuatia kuwepo kwa maneno yaliyosambaa mtandaoni kuwa Mbosso amejing'oa kwenye lebo ya Wasafi.
Screenshot 2025-02-04 172745.png
 
Ila ujio wa digital platforms unawalipa sana wasanii, watu wanatengeneza mamilioni ya fwedha.
Unakuta umeingiza 500M kwenye digital platforms halafu label inasema utoe 40%, hapo ndipo vijana wanaamua kuaga... hahahh
Sasa yeye si anabaki na 300M mbona ni nyingi tu!
 
Sasa yeye si anabaki na 300M mbona ni nyingi tu!
We ungekubali ukatwe milioni 200 ubaki na hizo milioni 300.
Kuna ile umekaa peke yako unaanza kuwaza laiti nisingekuwa chini ya watu hii milioni 200 ingekuwa yangu pia, hapo ndipo unafanya maamuzi...
 
Back
Top Bottom