Diamond afunguka haya kuhusu issue ya mama yake kutopost picha ya Zari siku ya kuzaliwa kwake

Diamond afunguka haya kuhusu issue ya mama yake kutopost picha ya Zari siku ya kuzaliwa kwake

STUNTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
13,076
Reaction score
17,247
Habari za kuwepo kwa bifu kati ya Mama mzazi wa Nassib Abduli aka Diamond Platnumz na Zari ambayeni mpenzi wa msanii huyo na Mama wa mtoto wake wa kwanza zilichukua sura mpya.

Mwezi uliopita baada ya Mama mzazi huyo kutopost picha ya Zari kwenye BirthDay yake na kuja kupost picha ya Wema Sepetu akimtakia Birth Day njema.

Kwenye The Playlist ya Times FM, Diamond aliulizwa swali hilo ambapo alifunguka kwa kusema kuwa inabidi ifike mahala kuwa wawape watu kitu cha kuzungumza kwakuwa kibongo bongo familia yao inatizamwa kama ya kina Kardashian.

“Sisi ndio pambo la mitandao, Mtu akiamka lazima aingie kwenye familia ya kina Diamond ajue inafanya nini, ni familia ambayo ina mshikamano na ipo kibiashara zaidi”.

“Inabidi tuwape watu vitu vya kuzungumza zaidi, Kila kinachofanyika kinafanyika kwa makusudi na Mama yangu na Zari wanaelewana sana, ndio maana Zari yupo Tanzania kwa sasa”
 
Haya wapenda ubuyu, mnakaribishwa
1475690134062.jpg
 
Ila dangote amshauri Zari aache kutafuta kick za kijinga ili aache kutakanana na wadogo zake, kile kitendo cha kupost hereni za Hamisa na kusema cheap stuff hakikuwa kizuri hata kidogo, na alijua kabisa walikuwa kazini hizi ni kiki za kijinga
 
Una uhakika n za hamisa? Au zari alitaja kua ni za hamisa,si nyie wabongo mkipewa picha mnaweka story yenu
 
Una uhakika n za hamisa? Au zari alitaja kua ni za hamisa,si nyie wabongo mkipewa picha mnaweka story yenu
Ujaribu kutumia akili japo kidogo, zari aliona picha za hamisa zimerushwa zikiwa na hizo hereni sikioni kipindi akiwa south, ndio zari nae akapta sababu ya kupiga picha, jaribu kutumia akili kidogo usipende kutafuniwa ndio umeze, na kama kitu hujui pita kimya.
 
Hivi hujaelewa Diamond alivyofafanua hapo juu au hujasoma huu uzi unasema nini. Diamond amesha kwambia yote waliyofanya ni kiki tuu. Hakukua na aliyeacha hereni chumbani kwa Diamond. Yote yalikua kuwapa watu cha kuongea. Haya sasa uache kukazana na hii issue ya Zari
 
Ujaribu kutumia akili japo kidogo, zari aliona picha za hamisa zimerushwa zikiwa na hizo hereni sikioni kipindi akiwa south, ndio zari nae akapta sababu ya kupiga picha, jaribu kutumia akili kidogo usipende kutafuniwa ndio umeze, na kama kitu hujui pita kimya.
Akili ipo unataka nitumie wakt kila kitu kinajionesha,we umeona hereni kisa zinafanana ukatengeneza habari chaumbea wwe
Kazi kufatilia ya watu
wasichana kibao wanahizo hereni

Sent from my GT-I9060I using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom