Diamond: Agent alishangaa watu wengi kuulizia nyumba niliyonunua SA

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Diamond amedai kuwa idadi kubwa ya watu, hususan kutoka Tanzania ilikuwa ikipiga simu kwa wakala aliyekuwa akihusika na mauzo ya nyumba aliyonunua Afrika Kusini kutaka kujua kama ameinunua kweli nyumba hiyo au alipiga changa la macho.



Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM, Jumamosi iliyopita, Diamond alisema wengi walikuwa wakiiuliza nyumba hiyo kinafiki
hadi wakala alishangaa imekuwaje! “Baada ya yale maneno maneno, hata yule agent alishangaa ‘hii nyumba mbona sasa hivi inauliziwa’ maake ile wikiendi iliulizwa sana sababu birthday ya Zari ilikuwa Ijumaa so wikiendi kuanzia Jumamosi, Jumapili watu wakawa wanaenda eti kujaribu kutrack ‘vipi nyumba inapatikana.’

Kwahiyo baada ya hivyo wenye nyumba hata wakashangaa ikabidi Zari akawaambia kwamba mpenzi wangu ni celeb na ndio maana alivyopost watu wanaulizia kinafiki,” alieleza. “So baada ya hapo basi ikawa easy wakaitoa kwenye mtandao kabisa, halafu wakaweka kibango kwamba ‘sold out’ wamesahau tu chini kuandika Nasib Juma,” aliongeza Diamond.

Kwa upande mwingine staa huyo amedai kuwa aliinunua nyumba hiyo wa fedha alizozilipa mara moja ambazo ni takriban shilingi milioni 394 pamoja na fedha za transfer zaidi ya milioni 20. Diamond anadai hatua inayofuata ni kwenda kuipamba kwa kumtumia mtu wake wa decor. “Nataka kwanza nikapatengeneze, hapo sasa nataka kufanya ushembenduzi, watu wanafikiri nimefanya, kumbe bado sijafanya sababu vitu kama hivyo lazima uwe proud kwasababu mimi nimekuwa katika mazingira magumu sana kutoka Tandale,” alisisitiza.

“Kwahiyo ile kwangu mimi ni achievement kubwa, kumiliki nyumba South Africa sio kitu kidogo, na ndio maana nataka nikapapambe vizuri nikapitie njonjo haswaa halafu nikiingia South Africa ni mashauzi mengi sana. Of course sometimes you need to do that sababu unafanya kazi kwa bidii.”
 
niliwahi ku-comment ktk thread nyingine siku chache zilizopita iliyokuwa inamjadili diamond kununua nyumba SA.nilisema wabongo wote wanaohoji suala la diamond kununua au kutokununua nyumba SA ni ''mapumbavu na malofa'' in mkapa's voice.
 
anastahili kwa kazi anayofanya kwenye music Industry
 
Mimi kinachonishangaza sio diamond kununua nyumba, ila nimeshangaa kuhusu hiyo bei, naona kama ni ndogo ukilinganisha na nyumba ilivyo, hivi bongo unaweza pata nyumba ya namna hiyo kwa milioni 400?
 

Kwetu hapa tanzania 400m ni hela ya kiwanja real estate kwetu kila mtu anajiamulia. Tu
 
Naona kama hiyo pesa ni ndogo uki compare na nyumba yenyewe.
 
Mimi kinachonishangaza sio diamond kununua nyumba, ila nimeshangaa kuhusu hiyo bei, naona kama ni ndogo ukilinganisha na nyumba ilivyo, hivi bongo unaweza pata nyumba ya namna hiyo kwa milioni 400?
Dar es salaam nyumba zenyewe zipo wapi!! Ndo maana unakuta bei za hovyo hovyo! Sasa kwa South Africa, unaweza kukuta Pretoria peke yake ina nyumba zaidi ya 20,000 zilizo sokoni kwa wakati mmoja hasa ukizingatia kutokana na kupanuka kwa J'berg, majenzi yamehamia Pretoria!! Sasa hivi Dar es salaam nyumba za maana zilizopo sokoni zinaweza kufikia japo 1000?! I doubt... It's all about supply-price relationship.
 
Mimi kinachonishangaza sio diamond kununua nyumba, ila nimeshangaa kuhusu hiyo bei, naona kama ni ndogo ukilinganisha na nyumba ilivyo, hivi bongo unaweza pata nyumba ya namna hiyo kwa milioni 400?
Mkuu, ile mbona kubwa. Umeziona hizo za NHC zinazouzwa mil. 200 na kuendelea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…