MosiOfThunder kama ambavyo wenyewe wa Zambia wanapenda kuliita hili tamasha ni kati ya matamasha makubwa Zambia na linafanyika kila mwaka chini ya wizara ya Utamaduni na kampuni ya Bewaries yaani kama inavyokua Fiesta huku kwetu na wana utaratibu wa kualika wasanii toka nje ya Zambia na safari hii ilikua atumbuize Tekno ila akashindwa kwenda dakika za mwisho ndio kijana wetu Diamonda akapata nafasi ya kwenda kama mbadala wa Tekno.
Tuache uwasilishaji mbovu wa habari ni aibu kama Tekno alivyokuja Fiesta Dar alafu akatangaze aliujaza uwanja wa Leaders wakati kulikua na timu kubwa ya wasanii wetu ambao wamewavuta hao watu hii ni sawa Diamond yeye alienda kama mualikwa naamini hata angeenda Kingwendu watu wa Zambia wangejazana kwenye tamasha lao maalumu ila tunadanganyana kua kijana wetu amejazana uwanja ingawa mwenyewe Diamond aliweka wazi kua anaenda kuungana na wasanii lukuki toka Zambia kwenye hilo tamasha ni sawa uwepo wake ni chachu lakini hata asingeenda asingepunguza idadi ya watu,kwenye ukweli tuwe tunaambiana tu sio vibaya ila pia Diamond ametuwakilisha vyema kwa classic show.
hivi fiesta Dar mkisema anakuja Rihanna na kusema watakuepo wakina Lina tu?
lipi litajaza?
sio mfanya biashara ,ila uwepo wa Main artist katika tamasha unalipa Thamani Tamasha zima kwanzia Attention ya watu, mpaka Pesa ya kiingilio.
kwa maana akija Rihanna wanaweza fanya kiingilio 30000 kutokana na thamani ya msanii isiyokwepeka ,na local artist ikawa 10000 na wasijaze vile vile
local wanaweza piga show hata wasanii 10 club na haijai! club tu...
kwahiyo hapo diamond kafanya chachu kubwa sana. tumpe heshima yake, kwenda kuwa main Artist tu ni kujidhihirisha kuwa hata bila sapoti ya wasanii wengine anaweza akajaza vile vile.
ukizjngatia ameimba na mashabiki mwanzo mwisho ni kwasababu wanafahamu uwepo/ukubwa wake
Diamond anajitambua sana. asipokushika kwenye Tungo zake, basi mavazi atakayovaa ,usipoyapenda utapenda Dance!
ana sifa zote za kuwa mtumbuizaji Bora Africa.
sifa zake tumpe ,kafanya vizuri zaidi Zambia[emoji8][emoji8]