Diamond akitaka kuandika wimbo wa kuumizwa kimapenzi humfikiria msichana huyu

Pilipilihoho

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2016
Posts
202
Reaction score
145
Diamond Platnumz ni bingwa wa kuandika nyimbo za kuachwa, kuumizwa na kutendwa kimapenzi.

Kamwambie, Mbagala, Mawazo, Ukimwona, Nataka Kulewa, Bado na zingine, zilihit kwasababu ziligusa maisha ya wanaume wengine wahanga wa malavidavi.

Lakini staa huyo ambaye hivi karibuni alisema Zari ameutunza moyo wake kwenye friji kiasi cha masuala ya kuumizwa kuyasikia tu kwa wengine kwa sasa, humkumbuka msichana mmoja kila anapotaka kuandika nyimbo za aina hiyo.

Si Wema wale ex wake mwingine unayemfahamu, Harmonize amemtaja baada ya mimi kumuuliza tetesi kuwa mashairi ya bosi wake huyo kwenye Bado, yalimlenga ex wake, Wema Sepetu.

“Diamond hajaanza kuimba leo mambo ya kuachwa, aliimba Kamwambie, akaimba Mbagala,” Harmonize amesema kwenye Chill na Sky.

“Mimi naamini kabisa, hata mimi mwenyewe nilivyomuuliza ‘kwani ulimuimbia nani Kamwambie?’ akasema mimi nikitaka kuandika nyimbo yoyote ya mapenzi namkumbuka Sarah mwanamke ambaye nilimpenda sana.”
 
Sara ndio Nani?? Tuwekee picha yake
 
Huyo Sarah ndiye aliyekuwa demu wake kipindi Domo anaokota vyuma chakavu 'scraper'?
 
Sarah yuko wapi sasa? ukirudi tuwekee na picha ya sarah
Sara ndio Nani?? Tuwekee picha yake
Huyo Sarah ndiye aliyekuwa demu wake kipindi Domo anaokota vyuma chakavu 'scraper'?
haya , halafu nitaweka picha
Kumbe sarah mjanja
Ila Sarah na Nassib ni vitu viwili tofauti, mafuta na maji.


Huyo white hapo
 

Attachments

  • 1459915163037.jpg
    13.1 KB · Views: 162
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…