Diamond akwaa skendo nyingine ya kutembea na Mia

Diamond akwaa skendo nyingine ya kutembea na Mia

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
Diamond-Platnumz-Tanzania.jpg

Mwanamuziki aliyeuteka ulimwengu wa Bongo fleva Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amejikuta ndani ya skendo nyingine baada ya mwanadada mrembo anayeitwa Mia kukiri kuwa alilala na nae nyumbani kwake Madale.

Wiki chache zilizopita Diamond alikamata headlines zote kwenye mitandao ya kijamii baada ya msichana huyo aliyetambulika kwa jina la Mia kuonekana akijirekodi ndani ya nyumba ya Diamond iliyoko Madale.

Baada ya kusambaa kwa video hiyo, mara moja taarifa zilienea kuwa msichana huyo alikuwa ni mchepuko wa Diamond na alikwenda Madale, jambo ambalo lilizua tafrani hata kwa Zari ambaye aliamua kumrushia dongo na kusema Madale pamekuwa Guest house.

Lakini tetesi hizo zilizimwa siku inayofuata baada ya timu ya Diamond kusambaza picha na video zilizokuwa zinamuonyesha msichana yule akiwa nyumbani kwa Diamoand, Madale lakini safari hii alionekana akiwa amekumbatiana na Bajuni ambaye ni mmoja Kati ya madansa wa WCB. Hivyo kuonekana kuwa Mia alikuwa ana uhusiano na Bajuni na sio Diamond kama ilivyodaiwa awali.

Ikiwa ni wiki chache tu zimepita baada ya sakata hilo kutokea, mrembo Mia amefunguka na kueleza ukweli wote ambapo amedai kuwa habari zilizoenezwa kwenye mitandao ya kijamii sio za kweli kwani yeye alienda Madale kumfuata Diamond.

Katika mahojiano aliyofanya na kipindi cha Shilawadu kinachorushwa na runinga ya Clouds, Mia alifunguka na kusema kuwa, alipigiwa Simu na Diamond aende Madale mida ya saa nne usiku na alipofika akalala naye mpaka asubuhi ya kesho yake asubuhi ndipo alichukua simu yake akajirekodi video akiwa anatembea tembea nyumbani hapo.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mia, Diamond alimuona akijirekodi kupitia kamera zilizokuwa mule ndani, ndipo akaichukua simu yake kwa lazima na kuanza kuisachi, kisha akaifuta kila kitu kilichokuwepo yaani picha zote mpaka video.

Aliendelea kueleza kuwa, baada ya hapo Diamond akawaita Bajuni na Harmonize na wakamlazimisha aanze kupiga picha na Bajuni ili ionekane kama ni wapenzi ili baadaye Diamond aje aseme alienda Madale kwa Bajuni na siyo kwake.

Mia aliongea kwa uchungu akidai amedhalilishwa na Diamond na watu wote wamejua kuwa yeye anatembea na Bajuni wakati alikuwa hajawahi hata kumuona hapo kabla wakati aliyeenda kumfuata Madale ni mwenyewe Diamond


Muungwana
 
Picha ya uyo Mia iko wapi tumthaminishe kama anafaa kua mboga ya uyo boss w Wcb
 
Hahahahha "kwa uchungu eti kadhalilishwa".... vibinti vingine wazazi walizaa kutoa uchafu tu.
Tufanye ni kweli kaliwa mambo na domo so what? Abebe mimba basi na yeye kiki ikolee...
Pumbavu kabisa uende mwenyewe, utamu ule wewe kuja kutughasi mitandaoni. Kwani ilikua ni porno hiyo kwamba baada ya tendo iwe matangazo?
 
Huenda wasichana wanafikiria kwa kutumia Medulla oblangata, Watu wanatafuta urithi kwa nguvu, au Mond anakojoa dhahabu.
 
Eti picha zote zilifutwa, halafu tena akalazimishwa apige picha na akina Harmonize. Sasa hapa mbona sijamuelewa
  1. Picha aliyoituma kwenye social networks ikionyesha anatembeatembea kwenye nyumba si ilifutwa, sasa yeye aliitoa wapi tena?
  2. Kama picha zilifutwa kulikuwa na ulazima gani wa kuwalazimisha Harmonize na Bajuni wapigine nae picha?
  3. Na kwani hawa akina Harmonize na Bajuni hawaogopi kuharibu mahusiano yao hadi walazimishwe kupiga picha?
 
Back
Top Bottom