Diamond, Ali Kiba na mtu wa tatu

Kazwala mkuu

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2016
Posts
1,034
Reaction score
2,250
Salaam

Katika wasanii wa kizazi kipya wenye gumzo kubwa kwa sasa ni Diamond na Ali Kiba, wasanii hawa wana timu kubwa za mashabiki kiasi kwamba kila upande huamini kuwa msanii wao ndiyo zaidi hivyo ligi hiyo haijawahi kuhitimishwa popote pale.

Naam mambo yamepamba moto kweli kweli na mziki wetu unapasua anga zaidi kila kukicha kupitia ushindani wao.

Mziki wa sasa umekuwa unafika mbali na kusikilizwa na wengi duniani, lakini pia vijana wetu wengi wamejiajiri kupitia mzikiLakini kila unapouliza nani msanii namba moja, kama hutajibiwa Diamond basi utajibiwa Ali kiba, tuwachukue wote kwa pamoja na tuendelee mbele.....nani mtu wa tatu? Ni yupi anaefuata mara baada ya hawa?

Je, ni vijana wa Diamond, Rayvan na Harmonize?

Je, ni vijana wa Kiba, Baraka de prince na Abdul Kiba?

Ni Barnaba boy

Rich mavoko

Duly Sykes

Ben Poul

Jux

Ommy Dimpoz

Belle 9

Rama dee

Chegge

Au nani?

Je, kwanza wao (Diamond na Kiba) wanastahili kuwa mbele ya wasanii hawa wengine?

Yupi mtu wa tatu?

Karibuni wataalam wa tasnia hii.
 
Mtu wa tatu bado hajajitokeza
Naona hawa farasi wawili wanakimbizana wenyewe tu hao wengine naona wanajifurahisha wenyewe tu
Mfano kama wakati huu ni wasanii wengi wana ngoma kali na video kali lakini hawatajwi kama hawa mabwana, mfano wa wasanii wenye ngoma tamu kwa sasa ni Barnaba boy (lover boy) Chegge (Waache waoane) Dully (Inde) Ben Poul (Moyo mashine) Jux (Wivu) na wengine wengi.....lakini bado wanaonekana kuachwa mbali mno.
 
Kwa sisi watu wa Hip hop tunaamini mtu wa kwanza ni Fid Q.....ila katika hawa wawili wanaovuma ni kwa sababu ya nguvu kubwa ya watu wazito na wenye pesa walio nyuma yao na team pia.
 
yaani umeongea kitu cha msingi sana, hao wengine hata wapige ngoma kali vipi watu wanawaanhalia hao tu namba 1 na 2


Kwangu Mimi namba 3 ni Vanessa au Navy Kenzo ( kimtazamo Wa kimataifa)
Kweli kabisa vanessa anastahili kua namba tatu nevy kenzo inabidi waamke na wawe serious na mziki wao
 
Kwa sisi watu wa Hip hop tunaamini mtu wa kwanza ni Fid Q.....ila katika hawa wawili wanaovuma ni kwa sababu ya nguvu kubwa ya watu wazito na wenye pesa walio nyuma yao na team pia.

kuliko joh makini??
 
Samahani mkuu naomba kukuuliza,hivi hao madogo Baraka na Abdukiba unaosema "vijana wa " kiba una maanisha nini sijakuelewa .............???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…