Diamond amejibana kwenye Kona ya CCM na Simba

kunamaisha njr ya kila kitu
Kunamashabiki wa simba ambao ni wapenzi wa chadema hvyo watampenda diamond kwa sababu ya simba hvyohvyo kuna mashabiki wa ccm ambao ni mashabiki wa yanga watampenda Diamond kwa sababu ya ccm
Vlevle kunasisi tulio nutral tutampenda kwa music wake tu
 
herman joshua mbona diamond aliwapigia kampeni CCM 2015 mbo Hadi sasa anazidi tu kuongeza mashabiki na anavizuri kwenye game na ndio Top artist Hadi sasa.
 
cha msingi akaoe kale katoto kanaitwa Chuchu sijui Zuchu akapige matukio mpaka mama mkwe almaarufu hadija Kopa awe flat kama bendera ya chama.
 
Niambie msanii mkubwa aliyewahi kufanya hivyo, labda ana malengo ya kuacha Sanaa na kuingia siasa.
Kwa Tanzania msanii mkubwa ni Simba Chibu Dangote. na kuna wengine wasanii wadogo wapo kwenye saisa wengi tu.
Kwa nje ya Tanzania ni Boby Wine.
 
Amini
Kua pesa ndio kilakitu
Hafanyi bure
 
Tandalese sasa ni rasmi anahodhi "brand" jina "Simba". Jamaa mjanja sana.

Namna alivyoacha kujiita "Dangote" na kujikita zaidi kwenye "Simba", huwezi amini. Huko nje wanaweza fikiria na timu anamiliki !!

Sasa kawaimbia "Simba kiboko yao...." Pale mnamtaja yeye ndio kiboko yao na Simba kama timu humo humo...
 
Wao ndo wanamhitaji mondi kwahyo watamfata popote aendako

Sent from my TECNO K9 using JamiiForums mobile app
 
Kila shughuli Ina miiko yake. Unapoazimia kuwa mwanamusic mkubwa saana everybody counts. Huku kwetu mambo yetu hayajanyooka Kama huko kwa wenzetu. Hapa kwetu siasa Ni ugomvi wa kuchomeana nyumba na ofisi, kuuana, uhasama. Simba na Yanga Ni uhasama pia wa kufa mtu. Usimlinganishe huko na huku.
 
Barack Obama wakati alipokuwa president wa United States alionyesha waziwazi kuwa yeye ni shabiki wa Chicago Bulls na haikuwa na madhara yoyote kwa raia wake.
Hata Magufuli anaweza kuwa SImba au Yanga na ikawa poa tu.
Tatizo lako Ni kulinganisha Marekani na Bongo. Marekani vyama vya siasa kupokezana Ikulu Ni Jambo la kawaida, wanashindana kwa sera. Sisi hapa Ni tofauti kabisa.
 
Cjaelewa ulichokiandika naomba urudie tena
herman joshua Kweli nimekosea si unajua niliandika nikiwa kwenye daladala alafu linanesanesa nilichomaanisha mbona diamond alifanya kampeni 2015 na ajashuka mpaka Leo na siku zinavyozidi anazidi kuongeza mashabiki Jana amefikisha 4M subscribers kwenye YouTube nakuweka record ya msanii pekee wa sub-saharan kawapita davido, Wizkid,burna boy n.k.hao mashabiki wa Yanga wanaolalamika kwanini Diamond asiwaimbia utawaona Taifa wakienda kumsikiliza Diamond watalalamika kwenye mitandao tu but physically mioyo yao haisemi hivyo.
 
Huenda angeshavuka hapo alipo leo unajuaje? Lazima ufanye impact assessment ndio uweze kutoa hitimisho Kama hilo.

Mfano, mke wangu ameacha kununua kazi za msanii fulani baada ya kupanda majukwaani na kusema vibaya viongozi wa chama fulani Cha kisiasa. Hapo msanii kapata au kapoteza? Angekaa kimya angeendelea kuvuna oeza ya mke wangu.
 
Mbona wasanii wengine ni mashabiki kwanini iwe nongwa kwa diamond


Tundaman -simba
Afande sele -simba
Mwana fa- simba
Maalim Mc -Yanga
 
Mbona wasanii wengine ni mashabiki kwanini iwe nongwa kwa diamond


Tundaman -simba
Afande sele -simba
Mwana fa- simba
Maalim Mc -Yanga
Wako wapi Sasa kimziki hao unaowasema. Mimi Ni shabiki mkubwa wa diamond, najivunia kuwa na mtu Kama yeye kwenye industry ya music, anathubutu, napenda awe focused kwenye Sanaa ili awe huru kupata mawazo na support ya watu wote iwezekanavyo. Siasa zetu bado Ni changa Sana kuzishobokea, zina mengi sana bado.


Hata mpira wetu bado unazo changamoto nyingi sana, hasa Simba na Yanga ambao wanashangilia timu ngeni kwenye mashindano sembuse Diamond.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…