Diamond Ampa Heshima Hii Alikiba

HELA

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2015
Posts
200
Reaction score
192
Meneja wa Diamond, Babu Tale ameonyesha kuwa wao hawana tatizo na Alikiba baada ya kupost kipande cha video kinachoonyesha picha ya msanii huyo ndani ya studio ya Wasafi Records.


Ni muda mrefu imezungumzwa kuwa Diamond na Alikiba wana bifu mpaka kupelekea kuanzishwa kwa baadhi ya team za mitandaoni za kukejeli mafanikio ya msanii wa team nyingine lakini hiyo ni dalili kuwa ipo siku itabaki historia tu.

Babu Tale alipost kipande hicho cha video kinachoonyesha baadhi ya picha za wasanii wakubwa Bongo akiwemo Marehemu Bi Kidude, Mr Blue, Dully Sykes, Juma Nature, Q Chief, Alikiba na wengine wengi.

Je, hiyo inaweza ikawa ndiyo kiki ya kuikaribisha video ya wimbo mpya wa Diamond aliowashirikisha P Square ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni?

Tazama video hapa.


Bongo5
 

Attachments

  • kibaa.PNG
    66.6 KB · Views: 168
 
[emoji81] [emoji81] [emoji81] [emoji81] [emoji81] [emoji81]
 
Kukosa tuzo sio mchezo atapost mpaka akiwa uchi ili watu wasahau kuhusu bet na hatusahau sisi
 
kwa kweli naju ukishapotea kwenye gemu ya bongo ndo kwa heri, ila alikiba anasumbua nampongeza sana huyu blaza.
 
Kukosa tuzo sio mchezo atapost mpaka akiwa uchi ili watu wasahau kuhusu bet na hatusahau sisi
Nani kawaambia msahau kwani? Msisahau tu muone mtapata nini. Haters it is 2016.
 
Nani kawaambia msahau kwani? Msisahau tu muone mtapata nini. Haters it is 2016.
Mi sio hater bwana mi napenda mziki mzuri kama wa wizkid na alikiba sipendi mzki wa Freemason Mimi
 
Hawa vijana wana mambo ya Kitoto sana.
Dai kaoa sasa ni mtu mzima atulizane na familia yake, kiba sio rika lake tena..daaadeki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…