Diamond Amwaga Machozi Studio

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Profesa J amesema Diamond Platnumz, alilia machozi wakati anafanya chorus ya wimbo wake ‘Kipi Sijasikia'
Rapper huyo alikiambia kipindi cha Sunrise cha Times FM kuwa wakati Diamond anarekodi chorus hiyo yeye na Majani walishangaa kumuona hitmaker huyo wa ‘My Number One' akibubijikwa na machozi ndani ya ‘booth'.



"Lakini kilichotushangaza alipoingia booth ili arekodi chorus Diamond alikuwa anaimba huku analia. Sisi tuko kwenye monitors huku tunamuangalia jamaa upande wa pili kwenye booth tunamuona Diamond analia. Alikuwa emotional unajua ile…ilimgusa sana. Sisi tulikuwa tunashangaa mimi na Majani ‘huyu jamaa analia nini?' Lakini baadae tulimuuliza alituambia ‘nimefurahi sana katika maisha yangu kufanya kazi na Profesa Jay pamoja na Majani, hilo moja. Lakini pili, mlivyoimba humu ndani vyote vinanihusu mimi…vimenitokea sana katika maisha yangu na changamoto zote hizo'..so yale ndio yalitokea studio. Kiukweli hii ngoma ilikuwa blessed tangu studio na kila mtu alikuwa anasema ‘yeah men it's on', alisema Profesa J.
 
Naikubali sana hiyo ngoma,nadhani majani kafanye kile ambacho nilikuwa nakitamani siku zote.
Profesa kapiga miondoko ile ile ya kitambo.
Nice song.

"Nlikuwepo":bolt:
 
unayehukumu ni wewe MwenyeziMungu naomba unilinde......ata nikinywa maji wanasema nakunywa pombe..

kipi sijasikia?
 
Ila mawingu haupigwi kbs nilikuwa sijui kuwa hata Prof Jizz naye kapigwa Ban.
 
Mwe ngoja nami niusikilize...ndiyo unaitwa "kipi sijasikia"?
 
Prof anajua muziki na anajua kuishi kama mwanamuziki...huyo Diamond inabidi Akue kidogo bado ana utoto utoto
 
Diamond kawa bausa lol na suruali zake za rangii nae akuee haachii,hongera zaooo
 
Eti wanatangaza amani huku wameficha mapanga,ha ha hii ni kali>
 
Jay kabebwa na diamond,Chorus nzuri lkn verses za kizamani. jay kaishiwa amebaki kujitetea tuu ooh sina ngoma!.. Kama huna si uweke cheti tuone kama upo negative!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…