Diamond angalia usirudie kosa hili tena kwenye biashara yako ya muziki.

Diamond angalia usirudie kosa hili tena kwenye biashara yako ya muziki.

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Wasalaam wana jamvi!

Bila shaka hakuna ubushi kuwa Diamond ni msanii ambaye ameendelea kufanya vizuri Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla na hata Ulaya ana kubalika na hadi kufanikiwa kuingia kwenye vinyang`anyiro vya kuwania Tunzo tofauti kama Channel O, AFRIMA, BET na nyingine nyingi!

Katika kosa ambalo aliwai kulifanya kwenye muziki wake ni kuachi nyimbo mbili kwa wakati mmoja(Mdogo Mdogo na Bam Bam) na akitegemea zote zifanye vizuri maana kwa mujibu wake aliwekeza pesa nyingi kwenye hizi nyimbo pamoja na video zake hivyo mategemeo yalikuwa zote zimlipe!

Ni wazi Wimbo wa Bam Bam ulifeli na haukuwai kufanya vizuri kinyume na matarajio ya Diamond na Pesa alizowekeza +Nguvu na ulifanya vibaya kwa sababu nyingi sana pamoja na kukosa promo kulinganisha na Mdogo Mdogo!

Katika hoja za Diamond kutetea sababu za kutoa nyimbo mbili kwa mkupuo ilikuwa ni kupigania au kupambana na soko la kimataifa hivyo Wimbo wa Bam Bam aliutegemea umtoe zaidi kimataifa kuliko nyingine maana aliimba kwa kingereza na aliamini kuimba kingereza kungesaidia kumsukuma zaidi kimataifa!

Ukweli ni kwamba Wimbo wa Bam Bam haukuwai kumsaidia Kabisa Diamond kwenye biashara yake na ni wazi ni mmoja wa wimbo ulio mtia hasara na wengi wanaweza kunishangaa kwanini nasema umemtia hasara wakati anapiga show lakini wanatakiwa kujiuliza ni Mara ngapi huo wimbo umpush au kuutumia kwenye show zake? Kimsingi hata ukiangalia kwenye nominations alizopata kwenye Tunzo tofauti huu wimbo haupo kabisa na sidhani kama kuna mtu ameshawai kufikiri kama huu wimbo bado hupo!

Kuna interview moja alifanya kwenye kituo kimoja cha Tv hapa nchini Diamond aliulizwa kuwa mbona kuna watu wana lalamika kuwa matamshi yake hayasikiki kwenye wimbo wa Bam Bam lakini yeye alisema hahaha hao sio hawasikii bali hawaelewi......!Mimi siamini Diamond ana hitaji kuimba kwa kingereza ili kuteka uwanja wa kimataifa na katika hili liko wazi kabisa maana anapata show huko kwa kuimba kiswahili tuu.......

Ina hitaji nguvu kubwa sana na ubunifu wa hali ya juu kutoa nyimbo mbili na zote zika Fanya vyema na kukulipa! Hivyo Diamond anatakiwa kufikiri kwa kina anapo taka kutoa nyimbo mbili kwa wakati mmoja maana uhitaji kuwa na nyimbo mbili kupenya kima taifa bali wimbo mzuri,promo,ubunifu na lugha yako zina tosha kabisa!

Diamond kama Una mpango wa kutoa nyimbo mbili kwa lengo la kuteka soko la kimataifa nakushauri mpango huo uachane nao maana huitaji kubadili lugha au kutoa nyimbo mbili ili kupenya kimataifa! Ni vyema ukatoa wimbo mmoja kama ni kingereza au kiswahili na ukaufanyia promotion kuliko nyimbo mbili!

Karibuni Wana jamvi!
 
Umeingea point muhimu sana hamna haja ya kuachia nyimbo mbili kwa wakati mmoja mfano wa bam bam hakua na haja ya kuimba kingereza na alimeza maneno sana kama ni kutoka kimataifa hata kwa kiswahili kunatosha ili na sisi tuwe na mziki wetu na style ya kibongo hamna haja ya kuimba kingereza ambacho hakisikiki mbona mafikizolo na wa South Africa wanatoboza tu na mother tongue zao awe anatoa wimbo mmoja mmoja ili upate air time ya kutosha
 
Kipindi cha nyuma kuna wakati amewahi kuachia nyimbo 2 kwa wakati mmoja pia zilifanya vizuri, nafikiri ndo zilimfanya aamini na hizi zinge-hit kwa pamoja. Big mistake
 
katika huo wimbo huwa naskia tu oh my God baasi vingine haskiki kabsaa alimeza sana maneno. Ni vyema aendelee tu kutumia kiswahili
 
Bam Bam sijawahi kuusikia mdogo mdogo kitorondo nshausikia,kama kuimba kiingereza ndio kuteka soko basi ni sheeeeddaaaaaa!!
 
Hapo kwenye kutafuna maneno alikataa kabisa na alisema ninyi ndio hamuelewi sio hamsikii! Tatizo kuna watu wana muaminisha kuwa kutoka kimataifa lazima kuimba kingereza lakini hanashindwa kushangaa mbona anapata show za nje kwa nyimbo zake za kiswahili? Katika kosa ambalo alifanya ni kutoa nyimbo mbili!

Umeingea point muhimu sana hamna haja ya kuachia nyimbo mbili kwa wakati mmoja mfano wa bam bam hakua na haja ya kuimba kingereza na alimeza maneno sana kama ni kutoka kimataifa hata kwa kiswahili kunatosha ili na sisi tuwe na mziki wetu na style ya kibongo hamna haja ya kuimba kingereza ambacho hakisikiki mbona mafikizolo na wa South Africa wanatoboza tu na mother tongue zao awe anatoa wimbo mmoja mmoja ili upate air time ya kutosha
 
Sidhani hata kama yeye mwenyewe bado ana ukumbuka huu wimbo wake ambao anasema ulimgharimu kuliko mdogomdogo!

Bam Bam sijawahi kuusikia mdogo mdogo kitorondo nshausikia,kama kuimba kiingereza ndio kuteka soko basi ni sheeeeddaaaaaa!!
 
Alisema ninyi ndio hamuelewi sio hamsikii.....
katika huo wimbo huwa naskia tu oh my God baasi vingine haskiki kabsaa alimeza sana maneno. Ni vyema aendelee tu kutumia kiswahili
 
Kipindi cha nyuma kuna wakati amewahi kuachia nyimbo 2 kwa wakati mmoja pia zilifanya vizuri, nafikiri ndo zilimfanya aamini na hizi zinge-hit kwa pamoja. Big mistake
Deonava, Diamond aliwai kuachia nyimbo mbili yaani mmoja kiswahili na mmoja kingereza?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom