Diamond atangaza rasmi kufunga ndoa na Wema, apanga kufanya harusi uwanja wa Taifa

Diamond atangaza rasmi kufunga ndoa na Wema, apanga kufanya harusi uwanja wa Taifa

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Msanii huyo ghali zaidi nchini kwa sasa, ametamka hayo alipozungumza na Mwanaspoti nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam juzi Jumatano. Alisema kuna mambo mengi yaliyomchelewesha kufikia hatua hiyo, ikiwamo maandalizi kwani amepanga mashabiki wake wahudhurie harusi hiyo.

ndoa_diamond.jpg


"Ndoa ni kitu cha heri na baraka, lakini kitu kinachofanya kidogo mambo yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni mtu ninayefahamika, kwa hiyo hata ndoa yangu watu wengi wanatamani waihudhurie," alisema Diamond.

Pia amesisitiza kwamba ndoa si jambo la masihara kwani ni tendo la kiimani na ndio maana amekuwa makini katika mipango yake.

"Nataka kila kitu kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza hata kuifanyia Uwanja wa Taifa," aliongeza.

"Unajua nilishindwa kufanya mambo haya haraka kwa sababu wengi nadhani wangeamini kwamba ninafanya hivyo ili kutafuta umaarufu zaidi, tunataka tufanye kiusahihi yasije tokea mambo kama ya Instagram tunataka tuje kuwa mfano wa kuigwa."

Alipoulizwa tarehe ya ndoa hiyo Diamond alisema: "Nilishasema ni hivi karibuni, unajua siku zote vitu vya kheri waswahili wanasema lazima uvifiche, hata Mwenyezi Mungu naye anasema anampenda mtu aliye na siri, lazima vitu vingine uvifiche ili vipate kufanikiwa. Wakati mwingine kunakuwa na husda, hasidi kwa hiyo ukiviweka wazi sana vinaweza kutofanikiwa."

Taarifa kwamba Diamond hataoa zilisambaa na kudaiwa kumchefua mchumba wake Wema Sepetu ambapo katika mahojiano mkali huyo wa wimbo ‘Mdogo Mdogo' alisema: "Kwanza sikuwahi kusema siwezi kuoa, nilishtushwa na gazeti hilo, nilisikitika kwa kweli na iliniuma sana, lakini nikaona nikijibu nitaonekana kwamba sina adabu, kwa sababu siku zote anayeanza huwa haonekani lakini anayemaliza. Pia siwezi kubishana na vyombo vya habari, mwisho wa siku ni watu haohao nitawategemea wanifanyie kazi zangu," alisema.

Hata hivyo Diamond alisema mchumba wake anaumizwa na vichwa vya habari ambavyo vimekuwa mwiba kwake.

"Hata hivyo magazeti yetu tumeshayazoea jinsi yanavyoandika, wakati mwingine inakuwa kama chachandu au kufurahisha baraza," aliongeza.

Kuhusu taarifa kwamba ameachana na mchumba wake huyo, alisema: "Hatuna tatizo watu wengi wanasema tumeachana, lakini hatujaachana na hatuwezi kujibishana.

"Sijui nikujibu nini kwa sababu kila nitakachokujibu utaona namsifia kwa sababu yule ni mchumba wangu.
"Lakini ninachoweza kukwambia ni kuwa sisi ndio tunaoujua ukweli wa uhusiano wetu.

"Sidhani kama ni sahihi mapenzi yetu yakawa na wasemaji wengine zaidi yetu wenyewe. Sasa ni ajabu watu wanaposema yao.

Chanzo: bongomovies.com
 
Attention seeker to nothing new si alisema wamemshauri asioe asije akaporomoka anajishtukia tu baada ya kumsema hadharani kaona madhara yake
 
Mimi ni miongoni wa Watanzania ambae ningependa kuona hawa vijana wawe pamoja. Ila Kijana Nasibu Abdul, aache tabia ya kutoa mambo yao ya ndani hadharani kama nikweli kile kinachosemwa amekiandika katika Mtandao wa Instagram.

Kila la heri Nasibu na Wema. Do it guys.
 
Ntakua wa kwanzaa kushuhudia hiyo ndoaaa yerewuuuuuu
 
Siku hizi mdomo anaukunja hadi unakuwa mdunchu....
kila laheri kwenye ndoa yenu
 
Hawa mademu vicheche ina kuhitaji uwe na akili ya ziada hata pindi unapo amua kumuoa ili akae kwenye mstari. Tena kijana hakikisha mkwanja wa show unaona pata mfungulie akaunti yake kabisa manake siku muziki wako ukifika kikomo huna mkwanja tena ata sepa tu ....jamii forums siipo, tuta kuja kutarifiana tena yetu macho
 
Back
Top Bottom