Diamond atangaza ujio wa Wasafi FM na Wasafi TV

Rais wa WCB, Diamond Platnumz ametangaza habari njema kwa watanzania hasa hasa kwa wadau wa tasnia ya habari kwamba anatarajia kufungua Wasafi FM na Wasafi TV.


Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Waka’ akiwa amemshirikisha msanii wa muziki wa kufoka kutoka Marekani, Rick Ross, alitoa taarifa ya ujio wa redio hiyo na TV kupitia twitter yake Disemba 30 mwaka 2017 lakini muda mfupi baadae aliifuta taarifa hiyo.


Weekend iliyopita muimbaji huyo akiwa nchini Kenya katika show za kuufungua mwaka 2018 alifanya mahojiano na kituo cha runinga cha KTN na kueleza mpango wake huo wa kufungua Wasafi FM na Wasafi TV.


Hiyo ni habari njema kwa wadau wa habari kwani kuanzisha kwa kituo hicho bila shaka kitazalisha ajira za kutosha kwa watanzania.

 
wasafi hawategemeyi tena ma radio ...insta na youtube ndo kila kitu kwao..
YouTube ndo platform wasani wengi wanaitengemea kwani inalipa kile mtu anapata, acha na hizi tv na radio kwani hazito mraba wa malipo kwa wasani kama ilivyo elekezwa na mamlaka nyenye zama kwa wasani.
 
Watu woyoooooo! Hayo ndio mambo tunayoyataka, lete mambo support utaipata
 
Mimi naona itakua poa especially kipindi hiki TV channels nyingi zinavyombania
 

Basi kama hivyo amiliki online radio na sio hizi za kawaida ...mimi nina marafiki wana radio wengi wanataka kufunga ,haziwalipi ...especially na hizi faini za TCRA ikitokea bahati mbaya tu umetoa content ambayo hawaitaki wanapiga faini hadi milioni 100 ambao ni mtaji wa radio ...huku ni kuuwa njaa waandishi na wamiliki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…