Diamond awaumbua team Wema

Diamond awaumbua team Wema

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Jambo limezua jambo, pamoja na kuanza kwa kishindo safari yake ya kuelekea Afrika Kusini ' Sauz ' kwa ajili ya fainali za kuwania Tuzo za MTV Africa ( MAMA ) , mwanamuziki Nasibu Abdul ' Diamond Platnumz ' na baby wake, Wema Isaac Sepetu wamechafua haliya hewa , Ijumaa Wikienda lilikuwa linarandaranda ndani ya nyumba.

Mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz' akijidai ' ndani ya ukumbi wa Club Billicanas. Pamoja na kufanya makamuzi ya kufa mtu kwenye shoo ya kuwatambulisha wasanii wanaowania tuzo hizo kwenye Ukumbi wa Bilicanas uliopo Posta, Dar , Diamond hakumpandisha Wema stejini kama kawaida yake, jambo lililozua kizaazaa.

Kuna muda mashabiki wake walipiga kelele wakimtaka Wema apande stejini lakini hakuikuwa hivyo kwa Mbongo Fleva huyo. Wema Sepetu akihojiwa na mmoja ya watangazaji katika ukumbi wa Billicanas. Msauz huyo alifanya shoo ya dakika 20 kisha akampisha Diamond ambaye aliingia naKibao cha Uswazi Take Away Remix, ambacho ndani yake amemfagilia HalimaHa roun ' Kimwana ' ambaye ni hasimu wampenzi wake, Wema.

Baada ya kumaliza wimbo huo ndipo baadhi ya mashabiki wakasikika wakimwambia Diamond ampandishe Wema la sivyowatakinukisha. Diamond akigonga shoo.

Ishu hiyo iliendelea hadi jamaa aliposhukastejini hapo. Wakati Diamond akiendelea kufanya makamuzi yake hayo, Wema na Halima Kimwana wote walikuwepo ukumbini hapo na kwa bahati nzuri kama si mbaya walijikuta wote wakimshangilia Diamond , tena wakiwa VIP ya juu ambapo walikuwa wakiingia watu maalum.

Mwanahabari wetu aliwashuhudia wawili hao walipogeukiana kila mmoja alionekana kumwekea mwenzake uso wa mbuzi .Nyomi ya kufa mtu. Hali hiyo ilidumu hadi Diamond alipomaliza shoo yake na Wema kushuka na kumuacha Halima Kimwana. Baada ya shughuli za shoo Diamond alibaki na Halima Kimwana wakicheza disco.

Kufuatia hali hiyo kwenye mitandao yakijamii usiku huohuo , kuliibuka maneno mengi kutoka kila upande kuwa shoo ya Diamond ilichafuliwa na Wema na Halima Kimwana ambaye alidaiwa alijipanga kwenda kumfanyia fujo Wema kwa kuwa yupo upande wa Penniel Mungilwa ' Penny' .
 
khaaa sijaona logic ya mashabiki kumtaka Wema apande jukwaani.. ina maana kila anapofika huyu kaka amtambulishe na Wema? limekuzwa tu hili jambo na Shigongo km kawaida.
 
Hao mashabiki sasa nao ni too much, hayo ni maisha yao
diamond asipokuwa na msimamo watampangia hata awe anapiga vingapi....

Yaan wanataka wema na diamond waishi na kufanya wanavyotaka wao, na bora alivyowakomesha maana wamezid vimbelembele sijui wakoje, safi sana ndomo, maana watakuzoea vibaya hao, ujinga wao wafinyie uko insta
 
khaaa sijaona logic ya mashabiki kumtaka Wema apande jukwaani.. ina maana kila anapofika huyu kaka amtambulishe na Wema? limekuzwa tu hili jambo na Shigongo km kawaida.

Hawa mashabiki na wenyewe sijui wapoje, sasa walienda kwenye show ya ndomo au walienda kutambulishwa wema, kwani hawamjui au ndo ushabiki maandaz, bora alivyowachuniaa maana akiwaendekeza watampangia had siku za kugongana na wema
 
hawa mashabiki wamezidi sasa bora kawakomesha mana ile ilikuwa show ya kutumbuiza na sio ya Wema kama kila kitu wanawaza kupandisha na kazi sa ngapi sasa
 
Yaan wanataka wema na diamond waishi na kufanya wanavyotaka wao, na bora alivyowakomesha maana wamezid vimbelembele sijui wakoje, safi sana ndomo, maana watakuzoea vibaya hao, ujinga wao wafinyie uko insta
Kawakomesha, wasimpangie maisha wamwacheeeee
 
wema anaweza kuwa Mke Kweli.....?

Kwa ndomo kaoza anaweza jitahid, ila ndomo sasa sidhan kama anamfagilia wema kihivyo maana rommy jones ndo kafanya mambo had wema kurudiwa baada ya madame kulia lia na kumuaid rommy kumnunulia gar kama ndomo akimrudia inshort romy ndo kamuokoa wema
 
Back
Top Bottom