Diamond azungumzia kuhusu Chibu Beats

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Baada ya ukimya wa muda mrefu tangu msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz atangaze ujio wa bidhaa zake za headphone ‘Chibu Beats’, msanii huyo ameelezea kinachochelewesha.

Muimbaji huyo ameiambia XXL ya Clouds FM kuwa bidhaa hizo zimechelewa kutokana na mchakato wa usajili wa jina.

“Katika usajili wa Chibu Beats jina lilileta matatizo kidogo, ilikwamisha hapo kwa sababu neno beats mtu kashalisajili dunia nzima mtu mwingine asilitumie neno la beats, siunajua ni la Dre. Kwa hiyo tunaweka namna nyingine ambayo itakuwa nzuri, zitatoka zimeshakuwa tayari mpaka sampo, tumeshasikiliza ni fresh sound hatari” amesema Diamond.

 
Jamaa ni kama kachanganyikiwa kila biashara anataka kufanya yeye..

Vipi ile kampuni ya kuhost events kama maharusi na dhifa mbalimbali alishaifungua? Chibu pafyumu nayo inafanyaje sokoni?
 
Kijana anapasua anga. Nahofia sana taratibu zetu za kodi ndizo zitakazomkwaza. Punde ataanza kufuatiliwa na watu wa kodi
 
Kijana anapasua anga. Nahofia sana taratibu zetu za kodi ndizo zitakazomkwaza. Punde ataanza kufuatiliwa na watu wa kodi
Sidhan mkuu
ukishakua karibu na .........
unadhan utasumbuliwa tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…