Diamond: Bob Junior ana mchango mkubwa kwenye maisha yangu

Maboso

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2013
Posts
5,164
Reaction score
5,762
Diamond hafanyi tena kazi na Bob Junior, lakini hawezi kusahau ukweli kuwa producer huyo wa Sharobaro Records ndiye aliyemfungulia njia ya mafanikio kimuziki. Akizungumza kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz Alhamis hii kupitia EATV, Diamond alikiri kuwa Bob Junior ana mchango mkubwa kwenye maisha yake.

“Kiukweli Bob Junior ana mchango mkubwa sana katika katika maisha yangu kwasababu ukiangalia nyimbo zangu zote zilizonitoa ni yeye ndiye alikuwa ametengeza,” alisema Diamond.

“Japokuwa hata kipindi ambacho nilikuwa nazitengeneza inawezekana watu walikuwa hawajamuona kama anaweza kuwa producer mzuri sana. Lakini mimi nilikuwa naona mbona huyu natoka naye, nakufa naye mimi yaani huyu natoa nyimbo na inahit,” aliongeza.

“Nakumbuka tulifanya nyimbo kama sita, Nenda Kamwambie, Mbagala, Nitarejea, Binadamu, nyimbo tofauti tofauti. Kila nyimbo alikuwa akinitengenezea akinipa beat nikifika nyumbani naandika vibaya sana. Na mpaka nakumbuka ilifika time niliweka kama chuki fulani kwa wasanii waliopo pale wakaona mbona unampendelea mtu fulani, yeye akasema mimi ni producer, natengeneza beat nikimpa msanii kaandikie kitu kikali, akasema huyu nikimpa analeta beat kali.”

Kwa upande mwingine staa huyo alidai kuwa Mbagala ni moja ya nyimbo zake anazozipenda sana kwakuwa aliuandika kwa ufanisi mkubwa.
 
Mbn hajamshukuru kiba maana ndo alimpa ruhusa ya kusain pale sharobalo rec
 
Au sababu nasikia alipitia pale na taulo kiunoni. Baba lazimaa amuheshimu
 
Kweli maisha yanabadilika nasikia diamond alikuwa anaosha hadi vyombo kwa Bob junior leo kijana hakamatiki kwa mpunga!
 
safi sana,, hakuna mtu ambaye Mwenyezi Mungu umbariki zaidi km mtu MWENYE KUSHUKURU,, KUTHAMINI NA KUKILI WALIOMSAIDIA katika safari yake ya mafanikio,, Mungu akujalie sana Diamond ila nawe watendee wenzako kama ama zaidi ya wewe ulivyotendewa,, all the best of lucks in your daily hustles!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…