Diamond, freemason siri nje

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363


Diamond akisalimiana na mtasha kwa ishara ya Kifreemason.

Stori: Shakoor Jongo na Erick Evarist


SIRI imefichukua kuwa madai kwamba ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ ni memba wa jamii ya siri inayodaiwa kumwabudu shetani, Freemason a.k.a Wajenzi Huru zilianza kitambo lakini sasa zimeshika kasi baada ya kunaswa kwa picha inayomuonesha akisalimiana na mtasha kwa ishara ya Kifreemason, Ijumaa Wikienda linaibumburua.
Kwa mujibu picha hiyo, tukio hilo lilijiri nchini Uingereza, mwaka jana, Diamond alipokwenda huko kwa ajili ya shoo.


MAVAZI

Ilidaiwa pia kuwa mavazi ya Diamond (meusi) yalishabihiana sawia na yale ya mtasha huyo yanayoelezwa kuwa sehemu ya mavazi ya jamii ya Freemason.


ISHARA

Kingine kilichoibua maswali ni ishara ya salamu ya wawili hao ambayo ilitengeneza nembo ya Freemason ya ‘V’ au bikari kwa namna walivyogusana kwa vidole.
Kwa mujibu wa wadau walioiona picha hiyo iliyonaswa kwenye mtandao wa Twitter, Diamond amekuwa na ishara nyingine nyingi za aina hiyo hivyo kuzidi kuzua utata kama ni memba wa jamii hiyo.
“Lakini inawezekana kwa sababu nasikia ukishajiunga unapata mafanikio ya ghafla. ‘So’ kuhusu hili, sina upande wa kusimamia,” ilisomeka sehemu ya maoni kwenye mtandao huo baada ya kuibuka mjadala mzito juu ya ishu hiyo inayozidi kushika kasi mithili ya moto wa kifuu.
“Tungeshukuru kama Diamond mwenyewe angejitokeza aseme ukweli kwani akinyamaza anazidi kutuweka njia panda,” ilisomeka sehemu nyingine ya maoni hayo huku ikiungwa mkono na wengi.


UNATAKA KUMSIKIA DIAMOND? SOMA HAPA


Ili kumaliza utata wa je, Diamond ni Freemason au la, Ijumaa Wikienda lilibeba jukumu la kumtafuta ili aanike ukweli wake ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Unajua mwanzoni nilikuwa sikumbuki ni lini na wapi nilipiga picha ya dizaini hiyo. ‘Anyway’, isiwe kesi, nakumbuka ilikuwa Uingereza kipindi kile nilikuwa na shoo nchini humo.
“Nakumbuka walinifuata watasha wengi tofauti lakini huyo mmoja alining’ang’ania sana nipige naye picha.
“Kwa kweli alinilazimisha sana kwa sababu mwanzo nilikataa lakini baadaye nikaona isiwe ishu nikampa ushirikiano alioutaka.
“Mimi sikuona matatizo alivyotaka tusalimiane kwa kugusisha vidole kwa sababu nilikuwa sijui chochote kuhusu Freemason. Nimeijua baada ya mambo haya kuyasikia kwa sana hivi karibuni.
“Kwa hiyo inawezekana siku hiyo waliniunganisha bila mimi kujua (kicheko).”


SASA UKWELI NI UPI?


Mara kadhaa Diamond amekuwa akihusishwa na Freemason kutokana na mafanikio ya ghafla aliyoyapata na mvuto alionao kwa mashabiki wake ndani na nje ya Bongo.
Ijumaa Wikienda lilipotaka kupata ukweli kutoka kwake, Diamond alifunguka:
“Si kweli bwana, mimi nazisikia tu hizi habari kama wengine. Nasikia tu ipo hapa Bongo na kiongozi wake ni Sir Andy Chande, zaidi ya hapo sijui chochote.
“Mimi ni mtu wa swala tano na mafanikio yangu naamini Mungu ndiyo kila kitu.”


KUNA MSANII MWINGINE

Mbali na mwigizaji Jacqueline Wolper na marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ ambao wamekuwa wakitajwatajwa na mambo ya Ufreemason, Ijumaa Wikienda limetajiwa msanii mwingine ambaye yupo mbioni kujiunga akidai anakwenda kufuata utajiri.


AANZA KUPATA MAFANIKIO

Msanii huyo ambaye ni mwigizaji mwenye jina (tunalihifadhi kwa sasa) anadaiwa kuanza kupata mafanikio ya ghafla hivyo Ijumaa Wikienda lipo mzigoni na litakapomuweka kati litamrusha hewani
 

Attachments

  • diamond.jpg
    93.9 KB · Views: 4,730
  • DiamondFreemason.jpg
    35.5 KB · Views: 4,685
Iyo ishara hutumiwa na rastafarians.

Haya magazeti ya shigongo yamehusika sehemu kubwa kuleta haya matokeo mabovu ya form 4.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Freemason kwa sasa ni inshu ya kitoto imeni chosha kuisikia
 
Iyo ishara hutumiwa na rastafarians.

Haya magazeti ya shigongo yamehusika sehemu kubwa kuleta haya matokeo mabovu ya form 4.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Sio siri mkuu haya magazeti yanahusika sana ktk hiyo makitu, ningekuwa ktk vyombo vya maamuzi ningetafuta sababu nikayafungia magazeti yote ya shigongo
 
Atajijua kila mtu na kaburi lake...na kila mtu na msalaba wake.!
 
Hana uwezo wala sifa za kuwa freemasoon. je Bakharesa ni nani? Mtu akilimiki hata suruali ni freeemasoon acheni kuwashushia hadhi wale ni balaaa!
 
Hakunaaaa wewe ki2 kama hicho, full uongo2, kwa kuzusha noooooooooooooooooooma!:high5:
 
Shetani mwenyewe hataki umwite shetani coz naye pia ana wivu so anataka aitwe mwema na kuhabudiwa vilevile
 
Watanzania mkiacha uzembe wa kufikiri nchi inaendelea hii. Akina shigongo wametumia ujinga wetu kujitajirisha.
 
Bado nna hasira na refa aliyeibeba real Madrid nagomea kutoa comments na ntagoma kula poyoyo sanaaaaaa
 
Bado nna hasira na refa aliyeibeba real Madrid nagomea kutoa comments na ntagoma kula poyoyo sanaaaaaa

Huyo refa ni freemason ndio maana kaibeba Real Madrid,.....ahahahaaaaaaaaaaaaaa
 
Mtu akiwa maskini kimya, mafanikio kidogo tu,,, ooohh fremason
Hebu acheni imani za kishamba.
 
Iyo ishara hutumiwa na rastafarians.

Haya magazeti ya shigongo yamehusika sehemu kubwa kuleta haya matokeo mabovu ya form 4.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

[h=5]Pliz my name is MKUWA RAJAB I am finish fom for. Ze everybody is to say we get za divishen 0, My part I am saying not I am not get divshen 0. I am vere vere intelijens, but pipoz don't like me. I have experience in singing bongoflava, so pipoz are jelas, the have put ...majik so I get diveshen 0. But I am clever becoz ask me forekzampo, what is fomula for water? Ze fomula for water iz Hech to O. Now why you give me dishen 0? Ok ask me anadha forekzampo what iz President of America? Ze president of America iz Obama. Ze gavament shud change my marks to dishen 2, because the youth are ze future of my country. If we get divishen 0 zen all the future is divishen 0. So giv us more maks becoz of ze future. Pliz mzee put on ze yua fb wall so ze Plezident will see.......[/h]
 
HII NDIO TANZANIA...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…