Diamond hakumtukana Zari, Hamisa wala Wema; alimtukana msichana aliyejifanya anamjua sana

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Wiki hii huko mitandaoni haswa Instagram kuna machafuko makubwa ambayo sababu kubwa ni madai kwamba Diamond Platnumz amewadhalilisha wanawake anaotembea nao ambao wanaosemwa haswa kwamba hilo dongo ni lao ni pamoja na Hamisa Mobeto na Zarina Hassan.

Mtafaruku huu kwa kiasi kikubwa umefanya baadhi ya mashabiki wa kike kuanza kususia kazi zake haswa hii Jibebe iliyotoka hivi karibuni kwa madai kwamba Diamond anawadhalilisha sana jinsia yao kutokana na maneno yake machafu ya mara kwa mara ambayo licha ya kuonywa lakini bado hasikii.

Mwanadada Rachel Temu ni mmoja ya wanawake ambao wamechukizwa sana na kauli ya diamond aliyoitoa mwanzoni mwa wiki hii kwa kumfananisha mwanamke na Kima.

Lakini kiukweli kwamba madai yote wanayoyaelekeza kwa Diamond ni batili na mengi yanafanywa na haters wa Diamond Platnumz ambao kwa namna moja au nyingine wana nia ya kumshusha kimuziki maana waswahili husema "Penye neema ya Mungu husda lazima iwepo" ila yote kwa yote aliyepewa amepewa tu hata wafanye nini hawataweza kumshusha Simbaaaa watashindana lakini hawatashinda zaidi na zaidi watajipotezea muda wao bureee.


Ukweli ni kwamba Diamond alimuita Kima yule msichana aliyejifanya anamjua jua sana kiasi kwamba anaanza kumuingia katika maisha yake binafsi badala ya muziki wake, sio kweli kwamba amewaita kima mademu zake.

Diamond ingawa mara kwa mara wanamchafua ,yeye siku zote huwa hajibu kitu ila kwa huyu msichana alivuka mipaka ndipo Diamond akaamua kumpa za uso bila huruma.

 
Kima mmoja aliyeongea? DIAMOND huwa anaongea na huyo alocomment? Angetaka kumzungumzia mtoa comment angesema aliye andika!
 
Hivi uanamziki hasa wa Diamond mnauangalia kwa kigezo kipi? Maana kuna wanamziki tangu nabalehe wako kwenye game (hawashuki na wanazidi kupanda), sasa huyu hata miaka mitano bado lkn kiki na nguvu kubwa sana inatumika sambamba na Ali Kiba. Kimaadili Diamond yuko too low lkn kwa watu tuliolelewa bila kupendelewa moja kwa moja lawama ni mama yake mzazi na inafahamika wazi mzazi mmoja hasa mama akiwa hayuko stable katika kukukemea amini utakuwa na tabia za ajabu ajabu tu.
 
Naomba kujua Kima ni nini!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…