Diamond hakuna unachodaiwa Kwenye music, lakini muombe saana Harmonize aendeleee kuwa juu la sivyo endelea kusimamia Biashara zako

Diamond kaanzaa kuwika hata Harmonize hajafika mjini Dsm. Hao kina Harmo ndo wananufaika na uwepo wa Chibu ila chibu hanufaiki anaweza survive bila msanii yoyote nyuma yake na huyo ndo Simba.
Kuanza kuwika lini sio tatizo..
Hata Mr Nice, Dudu baya nao walianza kuwika miaka na wakapotea...kwahiyo sio issue ya lini ameanza but ni issue ya sasa, simbenzi Diamond hata kidogo, ni mkongwe, mbunifu, anajituma, hana majivuno kama Harmonize lakini ukweli nj kwamaba uwepo wa Harmonize kwa sasa ndio unampa kufanya muziki kwa jitihada na akili zaidi kuliko wakati wowote ule
 
kwahiyo Yyyyyooooooooh Yyyyeeeh Baba hayupo kwenye battle?
Kiba ni kama timu ya Azamu, hata Yanga na Simba wakipotea yenyewe itakwepo tu na wala haitakuwa ndio kinara katika ligi ila itaendelea kuwa number tatu tu kwa maana KMC au Singida watakuwa vinara
 
khaaaa yaani Umlinganishe Diamond na harmonize
mleta mada umevuta bhangi ya wapi wewe
Don't take it personal mkuu Atacms hata yule ambaye kila siku huongoza darasani humuhofia namba mbili wa kila siku anapomkaribia..
 
Mkuu don't underestimate kipaji, kujituma, ubunifu na skills alizotokanazo usafini Harmonize, watu wengi walijua alipotoka usafini atapotea lakini amemaintain kuanzia muziki na mafanikio ya kawaida, nakubaliana Harmonize yawezekana hajamfikia Mond kimusic lakini kwa namna Harmonize anavyoendesha muziki wake na maisha yake Mond atamuwaza Harmonize kuliko Kiba, Kiba ni kama Azam tu haivumi lakini ipo, Yanga na Simba hata siku moja hawawezi muhofia Azam asiye jitangaza wala kuwa na ubunifu wowote katika kuvutia mashabiki zake
 
Let's be honest kwa ile Interview aliyofanya Harmonize airport kulikuwa na cha kujibu pale? Wote tunajua Harmonize alio ongea ukweli tena ukweli mtupu, Diamond asingiziwe yote yale then akae kimya ? Labda Sio Diamond huyu.
Kuhusu vijembe labda hufuatilii, lakini Mond pia anampiga vijembe mara kibao. Nakubaliana na wewe kuwa Mond yuko juu lakini bado ukweli unabaki mshindani wa Mond ni Harmonize
 
Nzuri sana hii👍👍
 
Hamuwezi kukubali au kujua kwa sasa mshindani wa Mondi ni Konde, kizazi cha kina Mondi na Ali ndio kina sie tunaanza kuzeeka majukumu tele,
Wakina Konde, Zuchu, Marioo, Nandy, wapo kati baadae waje wakina Abby Chams, Yami,
Tukubali zama zinabadilika
 
Mshatoka kwa kiba saizi mmempa Harmonize? [emoji1]

Sent from my M2101K7AG using JamiiForums mobile app
Very soon watahama kwa Mmakonde watahamia kwa Marioo, hata Rayvanny angegombana na Diamond possibly wangeweza kuwa kwake pia. Diamond amekuwa aki-shine kabla hata ya kushindanishwa na mtu yoyote though ushindani huwa ni mzuri kwani hufanya fans wafuatilie kila kinachoendelea.
Scenarios nyingine zote alizozitumia kama mifano nakubaliana naye kwa 100%, palikuwa pia Msondo vs Sikinde.
 
Umeongea sawa kabisa Mkuu

Sent from my M2101K7AG using JamiiForums mobile app
 
Ni kumkosea heshima kumfananisha Diamond na wajinga wajinga , Harmonize hata akijifia amemkuta Diamond yupo juu, yeye ndo anatakiwa aombe Diamond awe juu ili aendelee kujishikiza kama kupe
 
Hamuwezi kukubali au kujua kwa sasa mshindani wa Mondi ni Konde, kizazi cha kina Mondi na Ali ndio kina sie tunaanza kuzeeka majukumu tele,
Wakina Konde, Zuchu, Marioo, Nandy, wapo kati baadae waje wakina Abby Chams, Yami,
Tukubali zama zinabadilika
We jiulize wasanii wangapi walishindanishwa na diamond sasa hivi wakowapi Kuna Belle 9, Darassa alivyotoa wimbo wake wa Mziki, Aslay, Richmavoko, Alikiba n.k angalia hawa wasanii walipo na alipo Diamond sasa hivi ndio utajua Diamond haitaji hashindanishwe ili apae kimziki bali hao wasanii ndio wanamuhitaji Diamond wafanye vizuri kimziki
 
Kwa mujibu wa Harmonize alichosema pale airport ni kwamba Diamond akikushika mkono anachukua nyota yako je wewe unaamini ya kwamba Diamond akikushika mkono career yako inakufa?
 
Yule shangazi wa "naona mambo iko huku taarab imo taarab imo..." aliitwa NASMA HAMIS KIDOGO na sio NAJMA kama ulivyo nena.
 
Aisee leo JF kuna mabandiko ya maana hasa

Safi mkuu endelea kutupa vitu kama hivi, wacha niende MMU kusoma Fantasy kwanza
 
Duu kisa kaweka bango yupo single, clone haiwezi shindana na original.Endelea kujifurahisha kumfananisha Mondi na jamaa,mimi naona wanacho fanana ni jinsia basi.
 
Kwa mujibu wa Harmonize alichosema pale airport ni kwamba Diamond akikushika mkono anachukua nyota yako je wewe unaamini ya kwamba Diamond akikushika mkono career yako inakufa?
Hapana mkuu naona kama unapotosha maana ya alichokisema Harmonize kuhusu kushika mkono..Lakini pia hoja kubwa ya Harmonize haikuwa mambo ya nyota bali ilikuwa ni kuonyesha Umma namna aliyoyapitia, figisu na manyanyaso wakati wa kuvunja mkataba wake..kuhusu aliyoyasema kama ni kweli au uongo anajua Harmonize na WCB
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…