Diamond, Jokate WAMWAGANA !

mathematics

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2012
Posts
3,322
Reaction score
1,110


Stori Imelda Mtema na Erick Evarist | Gazeti la Uwazi

PENZI motomoto kati ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond' na Mrembo Nambari 3 wa Tanzania 2006, Jokate Mwegelo limedaiwa kuvunjika, Risasi Jumamosi linatambaa nayo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, raia wa Tanzania anayecheza mpira wa kikapu nchini Marekani, Hasheem Thabit Manka anatajwa kuwa chanzo cha penzi la wawili hao kusambaratika.

KWANINI?
Awali, Thabit aliwahi kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba ‘anatoka' na Jokate, madai ambayo kwa upande wake mrembo huyo aliyakanusha vikali akisema anasingizwa licha ya kujikanyaga katika maelezo yake.

Hata hivyo, baadaye wawili hao ikasemekana wamemwagana kwa sababu ambazo hazikuwa wazi kwa vile uhusiano wao ulikuwa wa siri kubwa.

WAMERUDIANA?
Safari hii, kwa mujibu wa chanzo chetu, Hasheem amemrudia Jokate kwa nguvu zote huku ikidaiwa kwamba hitimisho la uhusiano wao litaishia kwenye kufunga ndoa na kuishi kama mke na mume.

KUMWAGANA KWA DIAMOND NA JOKATE
Sosi mmoja alimjulisha paparazi wetu kwa staili ya kumuuliza swali kama anafahamu lolote kuhusu wapenzi hao kupeana mkono wa kwaheri.

"Hivi jamani mnajua kama Jokate na Diamond wamemwagana? Demu amerudiana na Hasheem Thabit, tena safari hii watafunga ndoa kabisa," alisema sosi huyo.

Akazidi kudai kuwa mbaya zaidi, Jokate amekata waya wa mawasiliano kati yake na Diamond, hali ambayo inampa wakati mgumu jamaa kwani uhusiano wao umevunjika huku akiwa bado anampenda.

‘WATUHUMIWA' WASAKWA
Ili kupata uhakika wa madai haya, Risasi Jumamosi lilimsaka Diamond kwa njia ya simu ambapo alipopatikana na kuulizwa kuhusu madai hayo, alikuwa na haya ya kusema:

"Hamna, hamna kitu kama hicho. Unajua mambo kama hayo msiandike. Mimi nitaondoka keshokutwa kwenda kufanya shoo Big Brother, si umesikia?"

Paparazi: Yeah! Tumesikia, habari tayari ipo kwenye gazeti.

Diamond: Basi ndiyo hivyo, hiyo habari ya Jokate bwana hamna kabisa.

JOKATE NAYE ASOMEWA MASHITAKA
Baada ya kuongea na Diamond, paparazi wetu alimtwangia simu Jokate ambapo alisikiliza madai mwanzo hadi mwisho lakini badala ya kujitetea au kufafanua, alikata simu.

WEMA ATOA LA MOYONI
Kwa upande wake, aliyekuwa mchumba wa Diamond, Wema Sepetu alipoulizwa kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wa wawili hao, alisema:

"Nilisema mimi mkanipuuza, sasa mmekiona alichokifanya Jokate? Naamini ni laana yangu kwani mimi sikuwahi kumfanyia jambo lolote baya Diamond. Mungu ameona, amenilipia. Teh! Teh! Teh!"

TUJIKUMBUSHE
Awali, ukiachana na mademu wengine, Diamond aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema. Penzi lao lilifikia hatua nzuri kwa mwanaume huyo kumvisha pete ya uchumba mrembo wake huyo.

Hata hivyo, uchumba wao ulivunjika baadaye huku Wema akimshutumu Jokate kwamba ndiye chanzo.

Jokate mwenyewe amekuwa akikana kuwa na uhusiano na Diamond lakini ilifika mahali mambo yakawa hadharani, Diamond akakiri kweupe kuwa anampenda sana mlimbwende huyo na hakuna anayeweza kuvuruga uhusiano wao.

Siku za karibuni, kuliibuka madai kwamba mcheza filamu mwenye heshima nusunusu Bongo, Aunt Ezekiel na Diamond walinaswa wakiwa kwenye hoteli moja jijini Dar es Salaam, hali iliyodaiwa kumfanya Jokate kulia wivu kwa kitendo hicho.

Kwa maana hiyo, kama Jokate amerudiana na Hasheem inawezekana kitendo cha Diamond kudaiwa kukutwa na Aunt kimechangia.
 

Attachments

  • RISASI.jpg
    65.7 KB · Views: 2,488
its funny bcoz diamond said jokate is special and was much better than wema, lol. umaarufu mwingine!

@Pwito, most posts are made during office hours, at least hatucheki NSFW sites
 
We got so many thangs to deal with. Apart from those retards.
 
Almasi piga number 3 kama 1 na 2 wamezingua nakuaminia kwanza jana bonge la shoo umefanya big up.
 
Kwataarifa yenu tu ...Jokate na Diamond hawakuwahi ku date..nimekua nikilisema hili jambo sana si tu kwakua na urafiki nao lakini nikitu ambacho media inashobokea lakin hakina umuhimu wowote..
 
wasanii wetu, wananifurahisha na 'sharing policy' yao tu! yaani bila kinyongo, huyu anamgonga huyu, yule naye mara karudia matapishi yake ya mwaka juzi! basi ilimradi uselebriti! lolest!
 
Kwataarifa yenu tu ...Jokate na Diamond hawakuwahi ku date..nimekua nikilisema hili jambo sana si tu kwakua na urafiki nao lakini nikitu ambacho media inashobokea lakin hakina umuhimu wowote..

na kuhusu ile status ya diamond fb, hebu fafanua! ambayo pia millard ayo aliweka! mmhh .....
 
Kwataarifa yenu tu ...Jokate na Diamond hawakuwahi ku date..nimekua nikilisema hili jambo sana si tu kwakua na urafiki nao lakini nikitu ambacho media inashobokea lakin hakina umuhimu wowote..

Wewe unawakanushia na kuwasemea kwamba hawajawahi kudate, mbona wenyewe hawakuwahi kukanusha hilo, na zaidi Diamond alisikika kumsifia Jokate na kusema hapo ndio amefika!
 
mhu.!! Nilibadili mademu kama vidaladala...!kijana tafuna mfupa angali meno bado yapo,nashuhudia Wema akijipigia debe kwa mara nyingine.!!
 
wasanii wetu, wananifurahisha na 'sharing policy' yao tu! yaani bila kinyongo, huyu anamgonga huyu, yule naye mara karudia matapishi yake ya mwaka juzi! basi ilimradi uselebriti! lolest!

Wanasema kizuri Kula na Nduguyo, usiwe mchoyo. Balaa ni pale ukisikia "Mmoja ana kikohozi, wenzie wooote wanakua na Homa" hamadi sijui anaugua nini??????
 
Dogo angalia maisha madem wana kuzinguwa sana umaarufu ni wamuda tu
 
Mimi uwa nahisi hawa wanaojifanya ni mastaa wa bongo sio binadamu wa kawaida.
 
Mtanzania ukishapa vijisenti hasa wasanii, kutwa nzima unawaza ujirushe na manzi gani! Huu ni umaskini uliokithiri... Mapenzi yenyewe ya kiduanzi tu, damn!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…