Diamond Kujenga Msikiti, Je Masheikh Wataupokea??

Kama mashekhe wenyewe ni hawa akina Alhad Mussa Salum, wataupokea tu hamna shida
 
Sheikh wa mkoa anasemaje kuhusu hilo?
 
Mziki ni haramu katika Uislamu, so sidhani kama wataruhusu msikiti Ujengwe na mtu anayefanya kazi HARAMU kidini
 
Aah shukran kwa ufafanuzi ila vita iliyoanzishwa inautukana uislam kwa ujumla. Wengi wataona ni dawa ya kuwaondoa viongozi wa bakwata ila hapana ni njia mbaya.
BAKWATA ni Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, sio dhehebu.

Madhehebu mojawapo ni Shia, Ibadhi, Aswar sunni,......
 
Mmh mond ajenge na asitoe picha maajabu nahisi hajajenga au kaukarabati tu kisha anakuja kujitapa kajenga
Mimi sijawahi kusikia, labda unitajie hata mmoja tu kama uthibitisho.
 
Bakwata watapokea tu hawana shida.ila ingekuwa dhehebu lingine angetupiwa mskiti wake km aende nao kwao akawasalishe WCB.ila rafk yake mange ataenda kuuzindua kabisa
Kanisa lizinduliwe na msikiti nao uzinduliwe? this is too much.
 
Mmh mond ajenge na asitoe picha maajabu nahisi hajajenga au kaukarabati tu kisha anakuja kujitapa kajenga
Kweli kabisa, japo kwa muumili wa kweli akifanya jambo hawezi kujitangaza kwa sababu anajua malipo atalipwa Muumba wake, ila ukijitangaza umefanya kwa ria(yaani kwa kujionesha) ambapo malipo yake yanakuwa ni batili.

Jee kwa jinsi tunavyomjua Mond, kama kweli alifanya asingeweza kutangaza? Jibu ni Hapana.
 
Makafiri mmebishana wee wenyewe tupo kimyaaa ndio raha ya Uislamu.
 
[A case of Rugemarila vs Kilaini of 2014 Escrow Scandal] under judge Mkwere (Rt)
 
Mi siingii msikiti wa Bongo Fleva. Haramu.
 
Diamond kajenga msikiti
By: Millard Ayo | Tue 26 Jan 2016, 08:37



Diamond Platnumz kajenga msikiti iliyogharimu zaidi ya milioni 30
Inawezekana umemuona mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz akiwa kwenye maisha mazuri kuanzia nyumbani kwake mpaka usafiri anaotembelea ila hujajua kwamba amekua akifanya ibada na kumshukuru Mwenyenzi Mungu.

Kwenye exclusive na DStv.com leo Diamond kakutana na reporter Millard Ayo na kuweka wazi kwamba ni kweli amekua kwenye ujenzi wa msikiti.

Pia unaweza kujua mengi kuhusu mastaa wa Tanzania na maisha yao kwenye Inside Bongowood, Jumatano saa 18:35 kwenye Maisha Magic Bongo.

Amesema, "Msikiti nimeujenga kule Mkuyuni Morogoro ni baada ya boss wangu Tale kuniambia kwamba kuna msikiti kule Mkuyuni na watu wanaswali kwa tabu sababu Msikiti ni wa udongo, watu wanapata tabu."

Diamond akaongezea, "Tuliuvunja mpaka tukaanza mwanzo kuujenga, sasa hivi ulipofikia ni karibia kukamilika.... gharama yake mpaka kukamilika ni zaidi ya milioni 30."

Akaendelea, "Mwaka 2015 nilijitahidi kufanya vitu vingi vya dizaini hii Mwenyenzi Mungu aone kabisa inawezekana kazi yangu ya muziki sio nzuri ila natumia kufanya mambo ya msingi."


Si useme tu kuwa hujuia, haya muongo mimi au wewe?
Acha uongo Moro na Iringa iko maeneo gani hiyo misikiti.
 
Msanii namba 1 Afrika kwa sasa, Diamond Platnumz ajenga nyumba ya Ibada (Msikiti)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…