Diamond laana hiyo!

sasa hapa mnataka kuingilia Uhuru wake Binafsi wa Maamuzi Binafsi , acheni Unafiki yeye mwenyewe anajua analofanya , Hukumu huwa hapahapa Duniani ...! Mtu unakata Mauno , kitu kinatiki unasepa ! Dangote angekuwa Muokota chupa za Plastic angejitokeza ?? Mtamu akiwanazo ehee .....
 
Michael essien pia alitoswa na dingi yake. Na yy baada ya kupata mafanikio akamtosa pia. Na hajawahi kupata laana.

Dingi yake Huyo alikufa nadhani ni mwaka juzi au jana.
 

Ndo maana tunaambiwa tumshukur mungu kwa kila jambo, ningekuwa mimi ningemshukuru sana baba diamond, kwa sababu yeye ndo aliyemfanya afike apo alipo kimafanikio, kumkataa kwake na kutokumsomesha kumemfanya awe mwanamuzik mkubwa sana na mwenye mafanikio, pengine angesoma angekuwa mwalimu asingekuwa na mafanikio kama aliyonayo sasa so hana haja ya kumchukia
 
Ni kwel inaumiza sana kutolelewa na mzaz au kukataliwa na mzaz...
Lakin kuna neno MSAMAHA...binadam ni nan had asiweze kusamehe..Mungu wetu anatusamehe makosa mengi hivyo nasi tunatakiwa kusamehe....
Ukifanyia wema mtu aliyekufanyia mabaya unapata thawab kwa Mungu na unamchoma moyo huyo MTU..

LET LOVE LEAD
 
watu hawajui mamake alihangaika vipi na mtoto ..baba mtu si alimbwaga mtoto akihisi anapunguza najukumu...sasa atulie tu sio kupiga kulele hasaidiwi wakati yeye hakusaidia

mmmmmm imekugusa lakini angemsaidia tu kisasi ni juu yake mungu
 
Mwanga mkubwa huyo mzee, huyo kaka dimond angekuwa mpiga debe leo hii angethubutu kwenda kwenda kwny media kumdai hela ya ma2miz, avimbe kabsa apasuke coz huo ndo mshahara wa aliyoyafanya kwa mwanae, shwain kabsaa
 
Dua la kuku halimpati mwewe.Mzee kabugi huyo,leo ndio anakumbuka kuwa anahitaji msaada wake.Yani alivyokuwa kilaza hajaomba msamaha kwa aliyo mfanyia mtoto wake,sijui anapata wapi hiyo confidence ya kulalamika kuwa hasaidiwi.
 
mzazi ni mzazi !
Usilipe ubaya kwa ubaya.

kweli unayoyasema lakini nahic hayajawai kukupata mtu unalia unamaliza maneno yote kujiuliza kosa lipi ulilomkosea haswa ad akukane? simchukii baba yangu ila popote alipo ajue kuna nafsi inamlilia na kunung'unika juu yake kila jua linapochomoza na kuzama sina memory nzur yoyote na yeye leo unahic atokee hapo yu hoi bin taaban anahitaj msaada ntastuka???? ntamsaidia labda kwa huruma ya kibanaadam ila co kwa kusema huyu baba angu, mda mwengine hatuhitaj hata pesa ila tunahitaj uwepo wenu wa kwa uongo na kweli inatosha.Wanaume msifanye hivi inatesa sana jamani
 
Lakini jamani mmeisoma hiyo habari vizuri? Ni wapi huyo mzee kalalamika? Si huyo mwandishi ndiye aliyeanza na yeye akatoa nje kumzungumzia Diamond?

Mwacheni Mzee wa watu ale chukuchuku zake
 
kwa akili za kibinaadamu ningesema diamond asimsamehe baba yake, ila 2kirudi kwa Mungu amsamehe tu ila ni vibaya sana kukana damu yako huku ukijua dhahir unatakiwa kua responsible kwa kila kitu juu ya mtoto wako, all in all yote hiyo hufanywa na washamba na malimbukeni kama huyo baba yake diamond
 
Aaah muache huyo mzee ajifunze,yeye ndio analaana ya diamond,hayo mambo ndio kama ya q chief
 
Huyo mzee Abdul kama vipi aombe msaada kwa Nassibu kama Mtanzania mwenzie sio mwanae,kua baba ni zaidi ya kutoa hizo mbegu mbona kuna watu kibao mtaani wametelekezwa na baba zao tena hawajuani na maisha yanaendelea akumbuke huyo Nassibu kapambana Tandale na Sandra wake wakati yeye anakula bata zake nao walikua wanalia pia,bata ni zamu kwa zamu.
 
Kama unawapenda wale wakupendao tu je wafanya ziada gani? Ni kweli inauma ila inabid amsamehe tu baba yake! .
 
Diamond aliwahi kuimba hivi kwenye wimbo wake "Binadmu"

"Kidogo nakula na Mama yangu, siwezi kuwasahu na ndugu zangu, salaam zifike kwa baba yangu, japo ALINIKATAA"

sasa shida iko wapi..kama alikataliwa hakuna tabu aendelee na life lake.....amtunze mama ake..alaah!
 
Wa kulalamikiwa hapa ni serikali ya CCM kwa kutoboresha huduma za afya. Lakini kulalamikia watu eti wanakunywa bia huku wengine wakiugua hilo linakuwa zengwe.
Anyway, ukiona hivyo huyo sio baba yeke.

CCM inakujaje hapo mkuu?
 
Diamond aliwahi kuimba hivi kwenye wimbo wake "Binadmu"

"Kidogo nakula na Mama yangu, siwezi kuwasahu na ndugu zangu, salaam zifike kwa baba yangu, japo ALINIKATAA"

Aisee! Kumbe Baba alimkataa???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…