Diamond mdogo wangu, naomba nikushauri kidogo

Zero Hours

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2011
Posts
12,942
Reaction score
18,669
Naomba Nikushauri kwa kutumia mfano wa wasanii Wakubwa maana ndyo Role model wako.

Mwaka 2008 had 2012, Lil Wayne alikuwa miongini mwa wasanii wanaotamba katika mziki wa dunia. Mwaka 2008 alipata Grammy, mtv , BET za kutosha kutokana na albam yake the carter 3 ambayo iliuza zaidi ya kopi milliin ndani ya wiki ya kwanza.

Baada ya apo aliendelea kutoa hit songs ambazo zilitamba billboards, Had 2012.

Lil Wayne aliendelea kutoa albums na mixtapes ambazo zilipata negative responses kutoka kwa mashabiki wake. Hii ni kwa sababu ya Explicit contents zilizokuwa kwenye Audio na Video ya miziki yake. Tv na Radio mbali mbali zilishindwa kucheza miziki yake sababu ya izo Explicit contents.

Amekuwa akitoa album na miziki mingi lakini imekuwa taged under explicit contents.
Explicty contents sio images tu za matus. Hata maneno pia.


Drake naye ni msanii aliyeanza kuhit kuanzia miaka ya 2012. Mwanzoni sikuvutiwa na style ya drake ya kurap sababu ilikuwa amecopy ya Lil wayne. Mpaka hivi leo ukimsikiliza Drake akiimba unaweza sema ni Lil Wayne. Ila cha kushangaza huyu drake leo anahit kumzidi Lil wayne alyemkocopy style ya kuimba.
Hii ni kwa sababu nyimbo na video za drake haziwi taged under PAL ( Parental Advisory Label) sababu hakuna explicit contents kwahyo nyimbo na album za drake huweza pigwa katika radio na television zote duniani kuliko za lil wayne.

Sasa narudi kwa diamond mdogo wangu.
Kwa haka katabia unakotaka kuanzisha. Katakutoa kwenye game vibya sanaa. Utakuwa unatoa hit songs kila siku lakini Anashangaa awards wanapewa wengine.

Angalia usijekuwa kama Lil Wayne. 2012 anatoa nyimbo na album nyingi lakini azihit ingawa ni hit songs.
 
diamond nazani ataka kumpoteza shabiki yake nambari moja tz,ndugu Jakaya Mrisho Kikwete...sidhani km mstaafu atafurahishwa na hii video,naomba Kikwete amuite na amuonye kwa wema.

btw,ngoma ni fire,replay since released offiacially!
 
mashabiki maandazi wataponda,wanapenda hadi wanakuwa vipofu na viziwi
 
Achen wivu iyo ngoma sija ona tatzo lolote tatzo mlivyo na chuki una kuna mtanzania mwenyewe ndo yuko bussy kui report ngoma ifungiwe nd ujue wa bongo mlivyo ma boyaaa.......nyimbo ngapi za nje zina pigwa Tz na video ni vile vile kama amtaki kuangalia fumbeni machoooo [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] POVU LANGU LA LEO
 
Kama Kuandika kiswahili kunakushinda, "Hamtaki" unaandika "amtaki" utaweza kweli kudadavua mambo makubwa na athari zake katika nchi.



Rudi shule ndio uje kuongelea mambo makubwa zaidi ya uwezo wako wa akili yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…