Diamond na Alikiba wachanga Milioni 40 kusaidia watoto walemavu

Diamond na Alikiba wachanga Milioni 40 kusaidia watoto walemavu

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,072
Hili ni la kupongeza!

Wasanii 'A-List' wa muziki wa kizazi kipya nchini, Diamond Platnumz na Alikiba wamejikuta wakichangia takribani shilingi milioni 41 katika Taasisi ya 'GSM' ili kusaidia jitihada za upasuaji kwa watoto wenye tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Awali, Diamond alitangulia kwenye taasisi hiyo na kukabidhi kiasi cha Milioni 20 kama mchango wake....
Diamond-na-Rais-wa-GSM.jpg


Na kisha baadae alifuatia Alikiba ambaye nae alitoa Milioni 21 hivyo kwa pamoja kutimiza kiwango cha milioni 41.

AliKiba-akiwa-na-bosi-wa-GSM.jpg


Hongereni sana Diamond & Alikiba..
 
Bravooooo....
Ila swalo oft -Mond n wakaa wa io nembo
 
Hawa GSM si ndio wazee wa Quality Center..
Mmmh Machale kundesa..
The Boss, kuna la kusema hapa? Mkuu Nguruvi3 give us an insight plz.. Huu sio udobi wa hela kweli huu?!
 
JazakaAllah kheri! Ila baba mzazi anakufa njaa
 
Wao ni Icon ya mziki wetu...inatia moyo wanapokuwa Icon ktk kutoa misaada km hyo....wanastahili pongezi
 
Hongera zao ila hizi hela kweli zinatoka mifukoni mwao? Au kuna ujanja fulani? Maana hali ilivyo ngumu kutoa hela yote hiyo just like that.kama kweli zimetoka mifukoni mwao hongera zao
 
Mkuu acha kukurupuka, nazungumzia baba ake mzazi mtoa mchango
Kwani huyo baba ake unaishi nae unajua kila kitu iyo kufa na njaa si tungeshamzika toka siku nyingi kabla ata mwanae kuna star
 
Back
Top Bottom