kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,875
Ndg zangu amani iwe kwenu!
Kwanza sipendi sana kuzungumzia mambo ya wasanii sana maana kwangu mimi mziki ninaoufagilia ni miziki ya zamani. Na wimbo wangu bora kabisa ni wa mzee marehemu Moses fan fan unaoitwa Papa lolo. Lakini kama mtanzania naomba niwape vijana wenzangu hawa tahadhari kwa mienendo hii niliyoona kwao.
Ndg zangu Diamond na Harmonize si mara moja nimewaona mkiwa mnawasogeza mashabiki wenu kuwasogelea ili kuwa karibu na jukwaa au stage. Lakini mnafanya hayo wakati waandaaji wa tamasha wakiwa wameweka barrier au wall kutenga stage na mashabiki . Lengo la waandaji ni kuzuia mashabiki kuwasogelea sana hali inayoweza kusababisha madhara kwenu lakini pia wanafanya hivyo ili kuweza kuwathibi mashabiki kirahisi (kuimarisha ulizni).
Cha kushangaza nyie mnapopandwa na mzuka mnawaita mashabiki karibu nanyi yaani ili wawasogelee, adhari yake ni kwamba wenyewe mnajiweka kwenye risk maana wale mashabiki wote si watu wazuri wengine wanaingia pale kwa malengo tofauti mnaweza kuudhurika. Lakini pili mnapoita watu mnafanya wale walinzi washindwe kuthibiti watu na kuzuia athari inayoweza kutokea lakini cha mwisho na cha muhimu mnaweza kuleta maafa kwa watu kukanyagana maana ikitokea wakati mnasogeza watu mtu/ watu akaanguka /wakaanguka hakika kifo au vifo lazima vitokee. Sasa chukueni tahadhari mapema na muache mara moja kusogeza mashabiki karibu na ninyi maana maafa yakitokea kwenye nchi za watu nyie wasanii na waandaaji hamtaachwa salama.
Jambo lingine ni tabia ya kugawa hela kwa njia ya kurusha hewani ili watu wagombanie, hivi ndugu zangu unaporusha hela hewani kwenye kundi la watu mnadhani hiyo hela inaweza kufika mkononi mwa mtu ikiwa bado ni hela inyofaa kwa matumizi? Mimi naamini hizo hela zinachanwa kwenye harakati za watu kuzigombania, acheni hizo tabia ni bora mkatafuta njia nzuri kugawa hizo hela bila kuzirusha hewani. Halafu kama watu walikupenda wakati huna hela kwanini leo utafute kupendwa zaidi kwa kurusha hela hewani. Ndg zangu hela haina rafiki wa kudumu hasa kwa mtu asiye na heshima kwakwe.
Mwisho nimshauri kijana mwenzangu Harmonize, najua hatujuani na najua sijakusaidia kufika hapo ulipo ila natamani uendelee kufika mbali, naushauri wewe na wengine wanaoweza kukuiga acha kabisa tabia ya kugomea show wakati ushafika kwenye nchi za watu. Yaani unatoka DSM unaenda hadi Nairobi au Mombasa unazungushwa mtaani kwamba utafnya show halafu muda unafika hutokei eti kwasababu hela unayolipwa ni ndogo au kwasababu yoyote ila. Hivi wale shabiki zako waliotaka wakuone watakuelewa kweli? je siku nyingine ukiwa na show huko watarudi tena? je kwa tabia hii watakusapoti tena? Sijasema ufanye show hata kama hela ni ndogo lakini iweje utoke dsm hadi kenya kama hujui kiasi utakacholipwa? Kijana mwenzangu utajiharibia kumbuka ni watu ndiyo walikupandisha na watu hao hao watakushusha kumbuka kenya umegomea show mara 2 baada ya kufika na watu kujaza ukumbi.
Nikiwa namalizia naombeni sana wasanii wetu msijifanye majeuri sana , mfano wewe harmonize umefika mombasa ukaingizwa kwenye prado kali ili uzungushwe kama kawaida, wenye prado yao wanakuonya kugawa pesa karibu na hiyo gari maana inaweza kuharibiwa kwa ujeuri unawajibu ikiharibika utalipa. Haya ukagawa hela watu wakavunja kioo cha gari unaletewa invoice unaona garama ni kubwa unakataa kufanya show, kwanini ulikataa kuwasikiliza waandaji wako? Kijana ukiendelea hivi utajiharibia sanaa yako.
NB; Mimi nimetoa tu tahadhari maana natamani mfike level za wasanii wakubwa huko duniani, nafurahia mafanikio yenu japo si shabiki sana wa mziki wenu