Diamond: Nililipwa 100mil kutumbuiza jukwaa moja na Ali Kiba

bizzle11

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2015
Posts
246
Reaction score
198
Diamond asema alilipwa shilingi milioni 100 ili kutumbuiza jukwaa moja na Alikiba katika show ya ‘Kiboko Yao'.

Mashabiki wengi wa muziki wa Bongo wanatamani siku moja kuwaona Diamond na Alikiba wanafanya kazi pamoja, kama ambavyo Wizkid na Davido ambao wameahidi kuachia joint yao siku si nyingi baada ya kuthibitisha kuwa hakuna beef kati yao.

Upande wa Diamond amesema kuwa yupo tayari kufanya chochote katika muziki endapo kina maslahi kwake. Kuthibitisha hilo ametoa mfano kuwa alikubali kushiriki tamasha la ‘Kiboko Yao' lililofanyika Leaders Club mapema mwaka huu ambalo na Alikiba pia alitumbuiza, kwa sababu lilikuwa na maslahi mazuri kwake.

"Unajua mi nafanya biashara, na kitu chochote ambacho kwangu mi kinakuwa kina maslahi mi siwezi kukataa kukifanya." Diamond ameaimbia 255 ya XXL ya Clouds Fm.

Baba Tiffah ameongeza kuwa alilipwa shilingi milioni 100 ili kutumbuiza kwenye tamasha hilo.

"Nakupa mfano hapa katikati kulikuwa na show ilivyokuja mi nikawaambia hii show ni biashara kwangu mi sikatai lakini you have to pay me, show mi nimelipwa milioni 100 ndo nimetumbuiza, siamini kama kuna msanii wa kiTanzania alishawahi kulipwa milioni 100, hili swala si umetengeneza kama beef, tuifanye kibiashara, nikalipwa milioni 100..

Nisiwe mnafiki milioni 100 sababu show hizo natozaga nikiwa na show nje labda Kenya , Rwanda naweza nikapiga show milioni 120, 130 lakini ilikuwa mara ya kwanza Tanzania milioni 100, lakini kwa sababu ilikuwa beef na sio kwamba show haikulipa, ililipa kwasababu ilikuwa imeshatengeneza tension yaani flani na flani kwahiyo tuzitumie hizi vitu kimaslahi zaidi."


Chanzo: Bongo5
 
ilikuwaje kuwaje mpaka akaongea hayo
 
Tigo wakanushe kumlipa hiko kiasi. Wasipokanusha mimi nitaamini hivyo.
 
Pia asisahau kuwa Alikiba alikula milion milion #120 na rich mavoko alikula milion #80 so hiyo ni kawaida jamaa aache ulimbukeni.
 
Tigo wakanushe kumlipa hiko kiasi. Wasipokanusha mimi nitaamini hivyo.

Tigo wanajishughulisha na mambo ya maana zaidi, mambo ya kuwaongezea maslahi.
Sasa porojo za baba tiffah na zenyewe wazitolee ufafanuzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…