Diamond: Niliwahi kupendwa na Msichana baada ya kujifanya mimi ni Z-Anto

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
1,016
Reaction score
2,195



Diamond Platnumz na meneja wake, Babu Tale jana walikuwa wakihojiwa kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM na kupitia Heka Heka alishare mambo mengi ambayo watu hawayafamu

Muimbaji huyo alidai kuwa kabla hajatoka kwenye muziki, alikuwa anapenda sana kuimba wimbo wa Z-Anto, ‘Binti Kiziwi' kiasi cha watu wengine kuamini yeye ndio Z- Anto.

Alisema ikatokea msichana mmoja akampenda akijua anayempenda ni Z-Anto lakini baada ya video ya wimbo huo kutoka, watu wakamjua kwamba sio yeye.

Anadai kuwa baada ya kujulikana ukweli huo, ilibidi asiendelee kukatiza maeneo ya Kariakoo aliyokuwa akiyatumia kukaa mara nyingi na kumchukua wiki tatu bila kwenda huko.

Alisema siku alipokutana na binti huyo aliyempenda kwa kudhania ni Z-Anto, alibadilisha njia fasta kwa kuhofia kuumbuka!

Chanzo: Bongo5
 
Imebaki historia sasa wanajileta wenyewe kwa raha zako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…