Diamond: Ningekuwa na sauti kama ya Ally Kiba, ningefanya makubwa zaidi

ruanganyi

Senior Member
Joined
Aug 19, 2014
Posts
115
Reaction score
34


Diamond Vs Ali Kiba ni ushindani usio rasmi unaochochewa zaidi na mashabiki wa muziki Tanzania kwa kuwa wawili hao licha ya kuwa wote ni wasanii wenye uwezo mkubwa sana kwenye uimbaji wanatajwa kuwa na tofauti au vita baridi.

Wapo wengi ambao wanauzungumzia hata kama sio kwenye vyombo vya habari na kuna wachache ambao maoni yao yamefika kwenye vyombo vya habari.

Vijimambo imezungumza na mmiliki wa G Records, Guru Ramadhani aka DJ G-Lover ambaye studio yake ndiyo ilimtoa Ally Kiba na kumfikisha kwenye mkondo mkubwa wa muziki ametoa maoni yake kuhusu utofauti anaouona kati ya wasanii hao.

Guru anaamini kuwa Ali Kiba ana hazina kubwa ya sauti na anakumbuka kuwa Diamond aliwahi kuisifia.

"Kwa kweli tofauti ukija kwenye masuala uimbaji, wengi wanaongelea hata katika mitandao tofauti tofauti kwamba Ali ana sauti nzuri na anaimba vizuri. Hata Diamond kuna wakati alikuwa anakiri kwamba angekuwa ana sauti kama ya Alikiba basi angefanya mambo makubwa zaidi." Amesema G-Lover.

Kwa mujibu wa G-Lover, wakati Ally Kiba yuko juu kupitia studio yake alikuwa na team ya watu wasiopungua thelathini, kitu ambacho Diamond anakifanya sasa hivi.


Chanzo: Vijimambo
 
toa utumbo wako hapa...yaani diamond sijui kawafanya nini watz?
 
"MEDIA WANAPROMOTE BEEF ETI WANADAI ZINAKUZA MUZIKI"-Propaganda
 

utoto.
 
Sio mpenzi sana wa Bongo Fleva, lakini huwa nashikwa na bumbuwazi watu wanaomsifia Ally Kiba kuwa anajua kuimba.

Binafsi sijaona ukali wake, anaimba neno moja anarudia mara 20 halafu mnasema huyo ni msanii mkubwa???

Kidogo Diamond anajitahidi kufurukuta
 

Huyo glover ndio adui no moja wa kiba, mr blue hata dully na yule sharobaro walikua nao wapotezwe tu na huyo glover. Yeye huwa anaona sifa kuwa na kundi kubwa la wasanii lkn hana dira na hajui awafanyie nini hao wasanii. Kwa wasiofaham glover alikua anamiliki kundi kubwa la new jack family lililokua na kina solo zaharani duly queen dahleen blue taqwa etc. Lkn alikua hajui hata anaweza kuwasaidiaje zaidi ya kukaa nao kijiweni tu pale kkoo. Mzushi sana huyo mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…