Diamond Platinamuz show tatu za nguvu kwa miezi mitatu

eddy

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2007
Posts
16,054
Reaction score
11,568
Diamond alifanya show ya mwaka mpya katika uwanja wa amahoro Kigali, ni kweli hii show ilikuwa kali na ilimlipa vizuri. Kafanya show ya Tigo pale leaders club Dar hii ni sponsored show hivyo ilimlipa si haba hadi akarushia washabiki burungutu la mihela. Badae akalamba sponsored show ya CCM kule songea nayo nasikia kapiga hela nzuri na sasa atapiga sponsored show kwa madiba ya Africa Magic Award.

Ukweli hizi show kazipatia na zinamlipa, ile tabia ya kujichoresha kwenye magazeti ya shigongo imepungua kama sio kuisha, muda mwingi anaonekana kwenye faragha za fukwe naona kapata mshauri mwema, hata ule msururu wa wapambe nao naona umepungua.
 
Niliwahi kusema ule msafara wake unamgharimu sana akipiga mil 10 anabak na 5
 
Niliwahi kusema ule msafara wake unamgharimu sana akipiga mil 10 anabak na 5
Mkuu, ule msafara unalipa kibiashara... kila aliye kwenye industry anafahamu kwamba Diamond anasafairi na msafara kwahiyo hata anavyojiiingiza kutaka kufanya kazi nae, anafanya hivyo huku akijua kwamba jamaa anasafiri na msafara... hata ukimwambia ana ngapi, amatakae Diamond atajipiga pini mwenye huku kv anafahamu kwamba anasafairi na msafara... hata kama wote wale wanalazwa kwenye chumba kimoja... na usishangae ukakuta wote wale wanalala kwenye chumba kimoja double lakini amtakae Diamond hawezi kuyajua hayo... moja kwa moja atauchukulia huo msafara ni moja ya gharama zinazotakiwa kuwa compensated! Usishangae ukaona wengi wao hakuna wanachoambua zaidi ya kupanda ndege na kusafiri lakini bado wanaingizwa kwenye gharama WHY? Diamond lazima ajumlishe gharama za bodyguard wake... huwezi kusema usije na bodyguard.... atakujumlishia na gharama za DJ wake (Rommmy) huwezi kusema huyo hapana wakati yeye ndie anaijua taste ya mwanamziki umtakae, atakuambia anakuja na meneja wake.... huwezi kusema hapana... mifano ipo mingi lakini kwa ujumla wake inaongexa thamani ya Diamond kuliko unavyodhani!
 
DIAMOND 4 rever... wengi wanaxubili ashuke...lkn jamaa anazd kushika chat tu.....

Diamond kashashuka kimuziki na yeye kashalitambua ndio maana alienda naijeria kuongea na p-square ili wampe siri ya mchezo! Vp Jini alilotupiwa mama yake lishatoka?
 
Niliwahi kusema ule msafara wake unamgharimu sana akipiga mil 10 anabak na 5

huo msafara ndio unaongeza thamani na unapandisha thamani yake..msome chige kaeleza kila kitu!
 
Last edited by a moderator:
Diamond kashashuka kimuziki na yeye kashalitambua ndio maana alienda naijeria kuongea na p-square ili wampe siri ya mchezo! Vp Jini alilotupiwa mama yake lishatoka?
Sasa kushuka kimuziki, kuongea na p-square kunahusiana vp na huko kutupiwa jini unakosema? By the way, hivi tangu uanze kumuombea mabaya umeshawahi kufanya tathimini na kuona umefanikiwa kwa kiasi gani?? In addition, hivi unaamini ilikuwa ni lazima hayo maoni yako kwenye huu uzi ambao haujadili kupanda au kushuka kwake zaidi ya mleta mada kuzungumzia mkusanyo wa mkwanja??! Hebu anzia hapo kwanza... hivi sasa amefirisika/choka mbaya, au?
 
Diamond kashashuka kimuziki na yeye kashalitambua ndio maana alienda naijeria kuongea na p-square ili wampe siri ya mchezo! Vp Jini alilotupiwa mama yake lishatoka?

Umemuombea kila baya toka 2010 mpaka sasa 20!5 haujachoka tu? Kubali matokeo, kisha tafuta kazi kwa bidii kuna siku Mungu atakubariki utapata tu ajira ila ukiacha hii roho ya choyo.
 
Daimond anatutambulisha jamani tuache masihala, hii nyimbo ntampata wapi nilikuwa naizarau sana mwanzo sasa naiona inazidi kupaa tv za nje zinacheza sana kwamba imekubalika,Daimond anajua hii biashara yaa muziki wa bongo anachakalika sana
 
Diamond kashashuka kimuziki na yeye kashalitambua ndio maana alienda naijeria kuongea na p-square ili wampe siri ya mchezo! Vp Jini alilotupiwa mama yake lishatoka?

Uliliona acha kupiga lamri na kutaka kutuaminisha ujing* kwani wewe ni mganga wa kienyej hata ukaagua hayooo??!?ebooo!!
 
Diamond kashashuka kimuziki na yeye kashalitambua ndio maana alienda naijeria kuongea na p-square ili wampe siri ya mchezo! Vp Jini alilotupiwa mama yake lishatoka?

Hahahaaa, ukweli unaochoma!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…