figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Baada ya kuwa katika upinzani wa muda mrefu, hatimaye wasanii nyota nchini Tanzania, Diamond Platinum na ALIKIBA wamekutana na kumaliza tofauti zao za muda mrefu.
Hatua hiyo imepokelewa kwa furaha na mashabiki wa pande zote mbili ambao wengi katika mitandao ya kijamii wamepongeza hatua hiyo.
Hivi karibuni, msanii Abdul Nasib maarufu kama Diamond akizungumza na waandishi wa habari, alimkaribisha mwenzake Alikiba kujumuika naye katika Tamasha La Wasafi 2018 linalotarajiwa kuanza Novemba 24.
Lakini katika kuonesha wawili hao wako tayari kufanya kazi kwa pamoja, Alikiba alijibu kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa amepokea mwaliko huo lakini kutokana na muingiliano wa ratiba yake ya kuzindua bidhaa yao ya Mofaya hataweza kushiriki na badala yake ametangaza kudhamini tamasha hilo kupitia bidhaa hiyo.