Diamond Platinumz Fans' Special Thread: Njooni tukutane hapa

Me nadhani hiii ishu ni mtego tu....hio barua naweza sema sio official koz haina stamp na pia imefichwa kwa iendako.....maana mkataba unaombwa kati ya kampuni na diamond platnumz.....je diamond na wcb for example ni separate entity????




My conclusion hiii ni Kik ya kijinga from haters kama ile barua ya kuomba msamaha jwtz....na very soon watakanusha tra...sidhani tra ni wajinga to the extent ya kuandika utumbo huo.
 
Oh vipi Maneke atanliliaa,

Je wasanii wenzangu wataniimbia,

au litafutika jina laangu,

na nyimbo hamtozisikia,

Ouh vip wasafi watanliliia,

je ndugu rafiki watahudhuriaa,

au ntakapokufa sina changuu,

na hata mama angu mtamkimbia
 
Hii barua kwa kweli nilipoiona kule kwenye jukwaa la siasa... ilinitatiza kidogo kwahiyo nikaamua kutoijadili na sana sana nikawa nahoji kauli za wadau! Tena nakumbuka nilita kuuliza ikiwa kizungu kimenipiga chenga au ni nini hasa coz' ukiangalia content na kinachojadiliwa ni tofauti! Tena ukiisoma vizuri wala sio issue ya WCB bali ni as if kuna kampuni X ambayo inafanya kazi na Diamond! Assume hiyo kampuni ni Coca Cola ambayo bidhaa zake zinatangazwa au kuwa promoted na Diamond!

Sasa basi, ikiwa Diamond ana-promote biadhaa za hiyo kampuni manake kampuni husika inamlipa Diamond! Hivyo basi, hata kama barua ni genuine bado issue yenyewe itakuwa haihusiki na muziki moja kwa moja bali nafasi yake kama ambassador wa kampuni hii ama ile! Na kama barua ni genuine, ina maana TRA wanafahamu au wanahisi kwamba kwa mtu kama Diamond na management yake hawawezi kuwa na proper accounting na hivyo kuamua kurudi kwa kampuni ambayo wana uhakika wa 100% kwamba lazima watakuwa wanatunza mahesabu na hivyo TRA watafahamu Diamond amelipwa shilingi ngapi na kampuni husika!

Sasa tuki-assume barua yenyewe ni ya kweli, kwanza kama nilivyosema haitakuwa inahusiana na show za muziki! Lakini hata hivyo, cjui nchi hii kuna celebrities wangapi wanao-deal na matangazo hadi iwe kwa Diamond peke yake! Aidha, tuki-assume kwamba ni ya kweli halafu ukafanya kwa celebrities wengine wote, basi hao wengine ndio watakaoumia zaidi kuliko Diamond! WHY?

Hizi kampuni zinapotoa michongo ya matangazo, wabongo wezetu walio kwenye hizo ofisi wanaojifanya kukufanikishia mchongo huwa wanapiga panga la kufa mtu! I mean, unaweza kuta Mkataba ni sh. 100 millioni... jamaa wanakuambia hadi mchongo ufanikiwe, kuna watu kibao inabidi tuwakatie ili wa-aprove! Kwahiyo unaweza kukuta mkataba wa 100 million unazoingiza mfukoni mwako ni 50 million pekee na zingine umeziacha huko huko!!!!! Sasa kwa msanii ambae hajawahi kupata michongo, kwake ataona poa tu lakini TRA wakitumia staili hiyo watakachojua wao sio kwamba uliondoka na 50 million bali uliondoka na 100 million!!!!

Kwa upande mwingine, hata kama itakuwa kweli, mtu kama Diamond haiwezi kumwathiri sana kama wengine simply because Diamond ameanza kuzidengulia deal za matangazo muda mrefu hivi sasa! Kutokana na hili, kama unamletea mkataba wa sh. 100 million halafu unamtaka 50 million aziache hapo hapo, hesabu biashara yenyewe ndo inaishia hapo hapo... labda yeye ndo aamue awapoze ngapi kwa kufanikisha! Kwa level ya Diamond, Lazima mchongo wa matangazo utakuwa unatokea juu kabisa... labda kwa Makerting Director.... "I want Mr. Diamond to be in this campaign...!" Hapo hakuna wa kupinga wakati kwa wengine, atakachofanya bosi wao ni kutoa kauli "I want a suitable candidate for this campaign...!" Hapo wabongo ndo wanaanza kutafuta nani aliye rahisi kumpiga panga!!!!

Hivyo basi, issue inabidi tuichukulie kwa sura mbili... mosi, ni UZUSHI na pili, ni kweli lakini kama ni kweli haihusiani na show za muziki bali TRA wanaweza kutumia kama njia sahihi ya kukisia nani alilipwa nini kupitia matangazo! Kwavile wanafahamu ni vigumu kupata taarifa husika kwa wasanii wenyewe kv hawatunzi mahesabu, taarifa hizo zinaweza kuwepo kwenye kampuni zinazotoa michongo hiyo! Na kama ni kweli, there's no way unaweza kumuhusisha Diamond peke yake bali kwa wote na ikiwa hivyo msiba utakuwa sana kuliko inavyofikiriwa kutokana na sababu zile zile.. kwamba TRA itamuona msanii X alilipwa 100 million kumbe maskini ya Mungu alitoka na 60 million!!!!

Itoshe tu kusema kwamba, kwa TRA hii iliyoshindwa kukusanya kodi kwa wenye misuli wala haiwezi kushindwa kuwafiafia watu kama akina Diamond!
 

Kuna madoshibegi wengi waliamini hiii habari ktk ile hali ya kwamba "diamond anafilisiwa"
 
Wadau,hii ngoma diamond aloshirikishwa na linex,hakika ndo vitu hasa mimi kama mpenzi wa mziki nnavovitaka kutoka kwa wasanii wetu.Mziki mzuri ni ule ambao ukiusikia kwa mara ya kwanza tu....unajua hapa....kazi ipo. Yan hii ngoma imenikumbusha enzi zileee za kina P funk palikuwa panaletwa vitu unavipenda from the first day.Hongera linex kwa kuchagua chagua sahihi katika ngoma hii.Na wewe kama kawa hujakosea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…