Kwa kipindi kirefu kumekua na tuhuma mbali mbali zikimhusu nguli wa bongofleva Nasib Abdul aka Daimondo aka Ndomo. Kutokana na hali hii niliamua kufanya utafiti wangu wa kina ili kujua ukweli wa suali mtambuka. 1.MAZINGAOMBWE.....Kwa mara ya kwanza baada ya kuwika na kutwaa zawadi tatu za Kili music awards miaka michache iliyopita tuhuma ya kwanza ikaanza dhidi ya ndomo kwamba haiwezekani kupata zawadi zote kwa mpigo lazma atakua anatumia mazingaombwe aka abracadabra! 2.FREEMASON....Baada ya tuhuma ya Mazingaombwe kuonekana haina mashiko ikaundwa tuhuma nyingine kuwa Daimondo ni Freemason!! Tuhuma hii ililazimishwa kwa kupitia magazeti ya udaku kuiandika mara kwa mara ili iaminike. Lakini kwakua Watanzania ni werevu haikupita muda hata tuhuma hii ikaonekana ni ushuzi mtupu kwahiyo nayo ikapotezewa. Hata hivyo, wazee wa fitina hawakulaza danu wakaingia mafichoni na baada ya miezi kadhaa wakaibua tuhuma nyingine 3. MGANGA WA KIENYEJI..... Magazeti ya udaku yakaanza kuandika kuwa Mwana Mbagala anashinda kwa Kigagula na ndo maana nyimbo zake zinapendwa sana na watu! Ikadaiwa kwamba nyimbo zake si nzuri kiivyo ila basi tu ni kutokana na kigagula tu. Ili kujenga hoja wakamleta mganga feki ili kuthibitisha. Maskini ya Mungu mganga mwenyewe alipoletwa mbele ya radio flani na kuhojiwa na kupigigwa maswali akawaanajichanganya tu. Akaishia kudai kua "kama hamniamini, mwaka huu kwenye kili awards Diamond hatapata hata zawadi moja na nyota yake naififisha kabisa"..the rest is history. Wazee wa fitna kama kawa baada ya kuona Mzee wa Tandale amepangua hata hii tuhuma feki wakaingia mzigoni na kuingia chimboni na kuibuka na tuhuma nyingine. 4. MADAWA YA KULEVYA. Wanadai eti Mzee wa Totoz kali ana pesa ndefu ambazo hazitokani na muziki bali ni madawa eti kwanini anafanya ziara nyingi nchi mbalimbali!! Katika tuhuma hizi zote kuna mambo yanafanana fanana 1. Tuhuma zote zinahusisha mambo ambayo mtu hawezi kuyathibitisha 2. Tuhuma zote huanzishwa na magazeti ya udaku. Mimi niliwasiliana na rafiki zangu wawili walioko kwenye gazeti la udaku na mwingine gazeti la serikali. Wao , bila hiana wakatiririka kwamba "Diamond wataendelea kumpakazia hadi akome. Kisa ni kwamba magazeti ya udaku ndo yaliyomtoa na zamani alikua anawatoa kwa kitu kidogo lakini siku hizi amekua na mkono wa birika. kila wakimwendea anadai eti ye hashiki hela, hela zote ziko chini ya management, eti ratiba zake, nguo zake na hela hapangi yeye bali management yake". Walidai eti simu zake 6 zimenyanganywa na pia passport yake imechukuliwa kwakua ye ni mtu wa madawa. Hizi zote ni fiksi tu. Daimond jumapili anaenda Kenya kwaajili ya mambo ya cocacola na cm zake zote anazo. Hawa jamaa sasa watatunga tuhuma nyingine na msishangae wakadai DAIMOND NDIE ANAYETENGENEZA TINDIKALI YA KUMWAGIA WATU!. Watanzania achene hizo, msapotini kijana wenu, daimondo anafanya mazoezi masaa 7 kila siku ndo maana mwili wake uko kimazoezi zaid, anakula vizuri ndo maana tungo zake zimeenda shule. Analipwa TZS 10,000,000 kwa shoo moja bongo na nje ya nchi US $ 15,000. Na mara nyingine kwa wiki anakua na shoo 3. Je ataacha kua na hela nyie kenge???? ACHENI FIGISUFIGISU BANA. KULA TANO DAIMONDO AKA NDOMO!!