Diamond platinumz ndio nani????

eastmea

Senior Member
Joined
Jul 28, 2018
Posts
159
Reaction score
133
Diamond ndio
1. Msanii pekee ambaye nyimbo zake hazipigwi kwenye media na bado anakimbiza tofauti na ilivyokuwa kwa Sugu, Dudu baya pamoja na Z anto.

2. Ni msanii mwenye mashabiki wengi Afrika Mashariki pia ni moja ya wasanii wenye mashabiki wengi Afrika kwa ujumla . Ana followers million 5 kwenye mtandao wa Instagram ambapo hakuna msanii ambaye ameikia idadi hiyo. Pia yupo kwenye listi ya wasanii watano ambao wanafollowers wengi Afrika tofauti na wale ambao wanafanyia shughuli zao nje ya Africa.

3. Ni msanii mwenye manager wengi afrika, ana mameneja watatu ambapo hakuna msanii Afrika ambaye amefanya hivyo.

4. Ndio msanii mwenye nyota inayong'aa zaidi Afrika Mashariki ambapo ukiwa karibu naye itapelekea kung'aa zaidi. Kwa mfano miaka ya nyuma wasanii ambao walibahatika kuwa karibu yake waling'aa zaidi tofauti na sasa ambapo wanang'aa ila sio kama walivyokuwa na Diamond Platinumz. Wasanii ni pamoja na Ney wa Mitego,Shetta, Ommy Dimpoz n.k

5. Ndio msanii ambaye amefanikiwa kuwainuwa vijana kutoka mtaa na kuwa wasanii wakubwa ndani ya Tanzania na wengine nje ya Tanzania ambao ni Harmonize, Rayvanny, Mbosso, Lavalava. Pia amejiri vijana wengine kutoka mtaani kama vile photographer wake anayejulikana kwa jina la Lukambao pia ndo msanii aliyeajiri vijana wengi Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla kupitia vitega uchumi vyake ambavyo ni Diamond Karanga, wasafi TV, Chibu perfume. Pia ameajili vijana wengi kwenye label yake ambayo ni moja kati ya label kubwa Afrika.

Lakini Diamond ndiye msanii anayepigwa vita sana pamoja na kufanyiwa fitina za chinichini na wadau mbalimbali wa mziki ili asifanikishe malengo yake lakini pamoja na fitina hizo lakini hajawahi kukata tamaa na kila siku anazidi kufanya maajabu katika game hii ya bongo fleva yenye fitina nyingi na kuwa inspiration kwa vijana wengine.

Tafadhali ongezea vitu ambavyo vinamuweka juu huyu msanii wetu
 
Inawezekana umeandika mambo mazuri, lakini mpangilio wa habari yako upo hovyo.
 
Kachukuwe hela yako ya kula sasa pale madale,kwani kazi umeifanya vizuri
 
Kaka sawa wewe ni mdananda mzuri unajua kusifia ila jifunze kuandika...
 
nampenda sana diamond plutnumz kikazi.. nilipata bahati ya kuongea nae anajua anachofanya.. hajaenda shule sana ila anajua mambo mengi sana
 
Hawezi kumshinda mwandishi wa vitabu mashuhuri, Le Mutuz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…