Diamond Platnumz ashinda tuzo kubwa ya BOA

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
15,351
Reaction score
21,362
Msanii mkubwa wa kimataifa kutoka Tanzania Diamond Platnumz usiku wa Jana alifanikiwa kuchukua tuzo ya Philanthropic Endeavour community action kutokana na mchango mkubwa anatoa kwa jamii.Tuzo hizo zinahusisha wachezaji maarufu pamoja na watu mashuuri wanaofanya vizuri.

Tuzo hizo ziliudhuriwa pia na mchezaji wa zamani wa man United Rio Ferdinand ukiachana na Diamond lakini pia mchezaji maarufu wa Chelsea na team ya ufaransa N'golo Kante pamoja na Wilfred Zaha walipata pia tuzo na wengine baadhi.

Lakini pia msanii wetu Diamond alipata fursa pia ya kuhojiwa na kituo kikubwa Cha uingereza sky sport.

NB: naona kijana azidi kututoa kimasomaso.

-----
Wengine walioshinda kwenye Tuzo hizo zilizotolewa Jijini London, Uingereza. Ni Fuse ODG, Wilfried Zaha, Mosamba, N’golo Kanté, Stormyz, Pia tuzo hizo zilihudhuriwa na watu mbalimbali maarufu akiwemo mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand.

Tuzo za BOA zinafanyika mwaka huu kwa mwaka wa 8 mfululizo, Na huwa zinawaleta pamoja watu mbalimbali ambao wanaunga mkono na kushiriki kwenye maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika bara la Afrika, pamoja na kuwapa Tuzo washindi wa vipengele mbalimbali.

Tuzo za Best of Africa huwa zinawahusisha zaidi wanasoka pamoja na watu mashuhuri ambao wanafanya vizuri kutoka Afrika.
 
Naomba mwenye kujua kuweka picha atuwekee picha la hili tukio me nimeshindwa kuweka picha please kwa wale ambao hawajui tuwajulishe
 
Tanzania Mtu Akishakuwa Na Mamlaka Kidogo Na Vipesa, Anaabudiwa Kinyama
 
Nampongeza sana Diamond. Ila wabongo wafupi sana jamani. Tunakwama wapi? Maana hapo Diamond ndiyo anduje...au mambo ya chips mayai?
 
arafu utasikia kuna mjinga mmoja anasema chibu wa sasa sio kama wa 2017, kwa hiyo anashuka kimziki.[emoji57][emoji57][emoji57]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…