Diamond platnumz, baba ni baba tu, rudi kwa baba yako

hana mapenz mzee anataka kutumia fursa apige hela tu
 
Waacheni wenyewe. Baba amesema hawajaonana muda mrefu ila akiwa na tatizo anamtumia fedha. Hiyo ni hatua nzuri maana kama kuonana hata sisi wengine tunaonana kwenye matukio makubwa tu na tuko mjini.
 
Naheshimu muda uliotumia kuandika haya maandiko, hilo tu! Nadhani ungerudi ukasoma comment ya niliyemqoute & mimi nilivyomjibu tena! Kama ni mtihani napitisha mstari tu, kwa sababu umejibu off point! Kifupi umekurupuka.
 
Mbona mara kadhaa wa kadha aliweza msamehe Wema anashindwaaje msamehe baba yake mzazi,if he real believe in God forgiveness is a blessing.
Kweli kabisa..kwanza ugomvi wa mama na baba yeye haumhusu..anaamini vp kama mama yake hakuwa na makosa??labda huyo mama yake ndo alikuwa chanzo..hata maandiko yanasema tusameheane.
 
Diamond, rudisha moyo wako nyuma. Samehe sabini mara sabini. Katika imani ya dini yako kuna hadithi ya Mtume Muhammad inayosema kuwa pepo ipo chini ya miguu ya wazazi wawili.

Kama kweli unamwamini Mungu na Mtume ni kiigizo chako chema, basi wewe unakosea sana. Msamehe mzazi wako, kutokana na maandiko huwezi kuwa na hiari katika hilo.

Mimi ni shabiki wako mkubwa, lakini kwa hili tutatofautiana milele.
 
Mbona mara kadhaa wa kadha aliweza msamehe Wema anashindwaaje msamehe baba yake mzazi,if he real believe in God forgiveness is a blessing.
Wema si kilikua kikojoleo,rahisi kusamehewa
 
sijaelewa amsamehe apate baraka za mungu au ampe hela maana naona uzi wakumtaka dai atoe hela. huyo mzee aendelee na maisha yake hivi kutelekezwa na mzazi mjue ule upendo kwake unakufa hata ujilazimishe haujiii, amkaushie hivyohivyo awe fundisho kwa wengine
 
Inawezekana mama yako alikua na maneno machafu kwa baba yako fanya uchunguzi kabla hujahukumu

maneno machafu ya mama ndo umtelekeze mtoto? mfano anasoma hata ukipeleka ada huko shuleni waalimu nao watakutukana amkaushie tu daimond fanya yako akitaka aje na DNA kudhibitisha wewe nibaba yake na maelezo kuwa ugomvi na mama yako.ilikuwaje akaacha kutumza mtoto
 
Kama ni yule ndio baba wa Diamond,Diamond ni sawa tu anavyochuna.
Yule jamaa ujanani alikua anaitwa Abdu kuku,kazi yake kubwa ilikua kushughulika na kuku,alikua golikipa mzuri sana wa timu pale pemba street.
hela ya mitumba na kodi ya nyumba zilimfanya apotee kwa sandra,na kumfanya sandra auze vitumbua huku yeye anatumbua na mizigo mibovu.
Hiyo nyumba ya urithi hela zake ndio zimemfikisha pale,jamaa sio teja wala nini.
mwacheni Diamond aishi na mama yake jamaa hakuwahi kutoa hata senti tano kumtunza Diamond
 
Lakini kisaidiwa anasaidiwa hela anatumiwa kama anahitaji kuwa karibu na mwanae angeanza yeye kumpigia kumtembelea madale sababu yeye ndo aliwatupa sasa yeye pia angejirudi kwa mawasiliano ya karibu nao mpaka dukuduku zao ziwaishe na kugeuka upendo asisubiri ubwete wa kufatwa kisa yeye baba
 
Haya ndio matatizo ya Haya maradhi ya 'single parent' ..Hata wakati huu ndio imekua fasheni sana...Mtu anazaa na jamaa linakimbia hataki hata kujua kama alizaa. na mama nae analea pekee yake watoto hawamjui baba.
baba ni baba na wazee ni muhimu lakini baba anapokua kawakimbia watoto hawauliza kheri wa shari anakuja kujitokeza alipoona mafanikio ..huyo baba hakufata watoto amefata mafanikio ya mtoto-pesa.
na ni vigumu kwa Diamond kurejesha moyo kirahisi. alichofanya huyu baba ni sawa na kumwambia mama diamond hao sio watoto wangu koma !!!

inachotakiwa clouds wampe ukweli kuwa ni mzee mwenye tabia mbaya anaekimbia majukumu hafai kuwa baba na atumie muda huo kuwaomba radhi watoto wake ..na sio kulalamika
 
Naona wewe utoto bado unakusumbua ungekua umeolewa au umeoa haya mambo ungeyajua lakini kwa sasa huwezi jua lolote kuhusu ndoa
 

MAMBO HAYA NI AMAIZING. NINA MTU WANGU WA KARIBU AMBAYE MZEE WAKE ALIPOTEA TOKA MIAKA YA MWANZONI MWA TISINI, ANAMTAFUTA SANA NA KILA SIKU ANAHUZUNIKA. SASA HUYU MZEE WAKE YUPO HAI ANASHINDWA KUJISHUSHA TU, KAWAIDA MKUBWA HUWA HAKOSEI, NA VILE VILE HATUWEZI JUA BEEF LILIANZAJE ILA KWAKUWA AMEJITAHIDI NA KUWA NYOTA WA TANZANIA BASI AMSAMEHE MZEE DUNIA IENDELEE.

MAMBO HAYA HUWA HAYAISHI VIZURI COZ BIBLE INASEMA " waheshimu baba na mama upate miaka mingi na heri duniani" not viceversa. Mungu hakosei na hiyo ilikuwa one way COMMAND. Hakuna palipoandikwa mzazi akikosea basi hataishi miaka mingi.

Ila anyway, hiyo ndo faida ya kumsikiliza sana mama.
 
Guys, issue ya baba kutelekeza familia au kumtenga mtoto akiwa mdogo au kukataa mimba yako vyote kwa pamoja visikieni tu kwa watu. vinaumiza sana.
 
Hawa wazee wana matatizo nyie acheni tu. But diamond usiache kumpa matumizi.
 
Kweli kabisa..kwanza ugomvi wa mama na baba yeye haumhusu..anaamini vp kama mama yake hakuwa na makosa??labda huyo mama yake ndo alikuwa chanzo..hata maandiko yanasema tusameheane.

Hata huyo baba alitakiwa ajue ugomvi wake na mama yake haumuhusu mtoto. Angemtunza tu kwa njia yoyote ile. Kuna watu kibao wa karibu ambao angeweza kuwasiliana nao hadi mtoto akapata huduma kama alikuwa hataki kuonana au kuongea na mama diamond. Nyie mnao mtetea huyu baba hamjui uchungu wa kutelekezwa.
 
Kwa watu makini kabla ya kuvuka barabara wanaangalia kushoto na kulia na ndivyo inavyotakiwa hata wakati wa kutoka Maoni yako ni vyema ungesikiliza pande zote,naamin jf kuna magreat thinker ila kunawakati nakwama.
 
Uuuwiii jamani waacheni angekuwa ni mama kawaomba msamaha ningesema angalau alibeba mimba na kumzaa kwa uchungu wkt angewe kuitoa hiyo mimba. Jamani wanaume wanaumaaa maumivu makali zaidi ya n'ge kwa familia. Baba ulikosana na mke ila watoto hujui wako wapi na wanaishije hata ile salamu ya Mungu ya bure huwapii na wakikupa au kukutafuta kwa jeuri ya afya na uzima unawajibu kashfa na matusi juu na wengine wanasemaga nani kakwambia mimi baba yako? kama huyo malaya kakuambia kakudanganya! just imagne mzazi yanakutoka hayo? hivi unadhani Mungu ni mdhalimu asimpe yule mwanamke uliyemkataa na wanae maisha bora zaidi ya yale yaliyokuwaga yanakupa kiburi na jeuri? Nawaunga mkono sana watoto hao... imeandikwa samehe 7x70 sikatai na kusamehe kasemehewa ila anachotaka si msamaha mzee yuleee anataka kula matunda yaliyoiva sasa ambayo hakuwahi kujaribu kuyamwagia maji hata robo kikombe zaidi ya kumwagia asidi yafe katita uso wa dunia na Mungu aliijua haki akageuza asidi ile kuwa mbolea na maji ya baraka ktk kufanya mti ule na matawi yake kuzid kuchanua na kulipendezesha jangwa. Wito kwa wazazi wote haswa wanaumee hii afya na uzima mlionao leo inayowapa jeuri mnawatenda mpk watoto wa damu zenu/mke wa ujana wako kama aishivyo Mungu siku na saa yaja mtalia kilio cha kusaga meno na hakuna atayeona kilio chenu ktk watu hao.
 
Yeye hakuwa na huruma kipindi alipowatelekeza,diamond huruma aitoe wapi kipindi cha mafanikio!!!!
 
Kweli kabisa unakuta alikukimbia toka mimba halafu eti ukubwani ndiyo anatafuta mtoto.Ngoja na mimi nijielezee kidogo background nilizaliwa na kulelewa na babu na bibi wakati huo mama yeye alikuwa na mji wake.Lakini huyo baba nasikia alimwambia babu eti ilitokea hivyo mimi niwe zawadi kwa babu kwa kuwa yeye ana mke wake.Nimekuwa kwa babu mzaa mama mpaka shuleni na majina natumia ya babu huyu.Kioja niko Advance level wiki moja kabla ya NECTA natembelewa shuleni eti na baba.Toka mdogo sijawahi kumwona ila nikasikia ana cheo kikubwa jeshini.Japokuwa ninazo namba zake na amewapa namba baadhi ya ndugu kuwa wanitafute mimi kaka yao.Na hii nilianza kutafutwa wakati nipo Chuo sasa hapa Baba anakuwa na msaada gani.Nitamwangalia kama mtu baki anayehitaji msaada ni hiari kumsikiliza au kumpiga chini.Hivyo kwa kesi hiyo hata kama ni wewe huwezi kuwa na upendo wa baba,mimi nilishafutaga kichwani suala la baba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…