Diamond Platnumz badili mwenendo before it’s too late!

Tukubaliane kuwa yule mama yake naye ni tatizo kubwa, hivi halioni hilo kwa mwanae? Ameweza kucontrol mangapi ya Diamond hilo limshinde? Diamond ana access na wataalamu wa kila aina angetaka wamsaidie kuishinda addiction asingeshindwa.

Diamond wa kipindi cha wema alikuwa amekonda bado kapauka pauka kiasi, Diamond wa kipindi cha Zari alikuwa ana ka mwili, anavaa smart anapendeza, akivaa suti inakaa, huyu Diamondi wa Tanasha na wa Zuchu aisee pamoja na hela zote hatazamiki, kakondeana, ngozi imevutika, ana mirasta yaani haeleweki.

Anyways: It is never too late, kama ni addict kweli bado ana nafasi ya kupona, watu wake hawawezi kumwambia ukweli yamkini wanafaidia na yeye kuwa alivyo. Na pakisambaratika kila mtu atabeba mbao zake atasambaa!

Binafsi ntasikitika sana tukimpoteza huyu kijana wa Tandale aliyefanikiwa kufika mahali ambapo wasanii wetu hawakuweza kufika, “Super star”.
 
Inahusiana Vipi Na mada
 
Hilo mimi nilipoanza kulisikia nikaanza kumtazama sana kwenye youtube, kuna ukweli kwenye hilo, Diamond hata kuongea kwake kumebadilika, anaongea kama teja kabisa.

Chanzo kikuu kinachowasibu hawa vijana ni kutaka kuonesha udume kwa njia yoyote ile kwenye ufuska.

Tumuombee abadilike, hakuna ataeweza kumbadili isipokuwa yeye mwenyewe. Lakini hali ni mbaya kweli, mpaka kubadilika namna ya kuongea, ni pakubwa si padogo.

Inatisha.
 
Mtu anapata wapi ujasiri wa kumfuatilia na kumpangia mtu maisha ya kuishi ?
Ikizingatiwa wewe sio Baba ake wala sio mama ake.?

Jiulize swali mmoja tu Kutumia kwake madawa kunaathir nin ktk maisha yako?

Ama akiwa sio mtumiaji wa madawa kunakunufaisha nin ktk maisha yako.?

Yaani mtu unaamka asubuh asubuh na kushusha kitabu kizima cha maneno kwa kumpangia mtu maisha ya kuishi.

Itoshe kusema kama hakuna lolote unalofaidika nalo ungeacha kufatilia maisha ya watu.
 
Nilikweli ulipoteza muda wako kumfuatilia mbona hukuhitaji hayo yote. Mabadiliko tayari yameanza kuonekana, hata kwa macho tu, sema yeye ni teja mwenye pesa ndio maana ilikufanya ushindwe kuamini.
 
Ukienda google ukaandika Diamond Platinumz utaletewa wasifu huu kwa hisani ya wikipedia.
Ni wasifu ulioletwa na jitihada za kweli za kijana huyo.
Kesho wasifu huo utasomekaje ikiwa ataangamia na upande huo aliopo sasa(hatuombi ifike huko)
Anhaaa Hapo sawa
 
Huo ni ukweli mchungu, mwamba alianza kwenye upunda na sasa kaamua alambe kabisa, wanavyoanza wanasema wanapandisha energy wakishakua addicted ndio vile tena....
Wasi wasi wangu asije akamuharibu na kale kabinti
Mbona kabinti kenyewe nacho tayari kameshaanza kulamba sema ndio kapo ktk early stage.

Ndio maana hakichagui cha kuimba, mara mibuno, mala sokomeza kavukavu, mara nailamba yote.

Ni athali za madawa hizo.
 
 
Acheni ulozi, madawa hata trump anatumia. Kuna madawa classic hayana madhara sio hayo wanaotumia watoto wenu huko kinondoni
 
Kwani akifanya vizuri sisi huwa inatuhusu nini? It is not about that “Kufuatilia maisha yake” tunatoa maoni yetu kwa jinsi tunavyoona inafaa na si lazima ayafanyie kazi. Halafu hajashauriwa kitu kibaya brother, tatizo ninini?

Sisi wengine ni mashabiki zake humu, unless wewe ni mgeni JF, Nifah ni mtani wa Jadi wa timu yetu, maoni yake ya leo ni constructive sioni ubaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…