Diamond Platnumz bado ni mshamba sana

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Jamaa kwanza kwenye uvaaji tu bado sana. Na tena afadhali ameacha kuvaa kofia za baridi wakati yuko Madale anatandikwa na jua kali, ilikuwa ni aibu.

Tuje kwenye uimbaji. Kila siku habari za mapenzi tena matusi. Hata kina Michael Jackson wameimba nyimbo za maisha kiujumla, yeye anataka kukaa kimya.

Tuje kwenye uchezaji. Diamond hajaweza kuwa na dance style yoyote iliyotrend Afrika. Kila siku anacopy style tena ambazo zimeshachoka.

Beyonce hakukosea. Bila nguvu za Makonda na CCM, Diamond ni kama Jux tu.

Inashangaza eti kuna mtu anamuweka level moja na Davido!!

Ningetoa ushauri ila sidhani kama utapokelewa kwa mikono miwili.

NYONGEZA: Sina chuki binafsi na Naseeb ila naona kipaji chake hajakitumia kikamilifu. Hana washauri wazuri. Washauri wenyewe nao sasa hivi wako busy wanagombania umaarufu huo huo.
 
Hayo mawazo yako na chuki zako binafsi.Kwani wasanii wote waliotamba wana dance zao binafsi?

Hebu nitajie dance binafsi ya Burnaboy,Patoranking,2 face Idibia?

Eti,msanii hana jipya,hana jipya kwako,msanii na show zaidi ya 90 karibia kila mwaka,hebu nitajie wasanii watano tu Africa wenye utitiri wa show kama Diamond.

Makonda ana mchango gani katika kupeleka mziki wa Diamond mbele?

Mbona Steve Nyerere na Bongo movie kila siku wapo na Makonda lkn hamna hata mmoja aliyefikia level za Kanumba.
 
Hata Makonda Mkolomije akipiga pamba hazimpendezi kawaida sana cha muhimu account iwe imenona na pupuchi unazila unavyotaka.
 
Ushamba ni nini? Je, ina-define-wa kidunia au ni mtazamo wa mtu mmoja mmoja?
 
Wewe mjanja uko nyuma ya keyboard hata nyuma ya nyumba yenu hawakujui..

Kudhihirisha ushamba wako Diamond ameanza kuwika 2009 mwaka ambao Makonda wa ccm hajatoka koromije..
Sasa huyo makonda unayemuongelea ni nani??
 
Roho ya korosho ukisikia kifo cha taratibu ndiyo wewe utakufa kwa wivu, fanya kazi upate pesa
 

Mada yangu ukiirukia kwa haraka unaweza ukadhani nina chuki binafsi. Ila ukweli ni kuwa kipaji cha Diamond kimetumika vibaya labda kutokana na ushauri anaopewa na watu wa karibu. Siyo watu wenye maono ya mbali.
 

Show 90 kwa mwaka ni dhahiri halipwi vizuri bali anadunduliza.
 
Mada yangu ukiirukia kwa haraka unaweza ukadhani nina chuki binafsi. Ila ukweli ni kuwa kipaji cha Diamond kimetumika vibaya labda kutokana na ushauri anaopewa na watu wa karibu. Siyo watu wenye maono ya mbali.
Kutumika vibaya kivipi ?
Kwani anaiba au anakula kwenu?
We mwenye maono alimsaidia msanii gani kufikia level ya Diamond?

Manake unaweza unapiga kelele humu kumbe unakaa kwa shemeji,bando la shemu na unalala kwenye chuma kirefu.

Kijana hii inchi kila mtu ana uhuru wa kufanya atakacho ili mradi usivunje sheria za nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…