Diamond Platnumz hili la kumfananisha demu (msichana) wako na Yesu (Mungu) utuombe radhi wakristo na utubu au wimbo wake ufungiwe na BASATA

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2015
Posts
1,393
Reaction score
3,237
Nimeusikiliza wimbo mpya wa Diamond Platnumz uitwao ongeza kiukweli anatakiwa atafute mhariri wa mashairi na mistari yake. Kwenye ngoma ya ongeza anasema "we ndo wangu yesu mkombozi sa mbona unaniacha mwenyewe" anamuongelea mwanamke/ msichana/demu wake.

Kwa hili Diamond hapana umeenda mbali mno na umetukosea Wakristo. Hivi mkristo aimbe wimbo amljnganishe demu wake na Mtume Mohammad au Allah atakuwa sawa?

Kwetu Wakristo Yesu ni Mungu kweli, mtu kweli Yohana Mtakatifu 1:1-10. Yesu ni Mungu mwana katika nafsi tatu za Mungu zinazofanya Utatu Mtakatifu.

Yesu aliacha kiti chake cha enzi kule mbinguni akauvaa mwili akashuka duniani ili atufie na kutukomboa sisi na dhambi zetu. Alisulubiwa akafa, akazikwa siku ya tatu akafufuka na sasa ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba na hapa tulipo tunasubiri arudi aje awahukumu walio hai na wafu. Maana ameahidi anakwenda kwa Baba kutuandalia makao na atakuja kutuchukua ili alipo nasi tuwepo. Je ni Yesu huyu wa kumlinganisha na demu wake kweli Diamond Platnumz?

Yesu huyu ambaye alikuwepo kabla ya ulimwengu kuumbwa ambaye maandiko yanasema vitu vyote viliumbwa kwa jina lake na pasipo yeye hakuna kilichoumbwa? Huyu ndiyo wa kumlinganisha na demu.


Ni kweli sanaa inahitaji ubunifu lakini siyo kwa kiwango hiki Diamond aombe radhi kwa kweli au wimbo wake ufungiwe na BASATA.
 
Ni makufuru kumlinganisha Yesu na girl friend wake, lakini pia ni makufuru kumwita Yesu Mungu Muumba wa mbingu na dunia.

Soma Mathayo 16:16,17 Simoni Petro akajibu: “Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”17 Yesu akamwambia: “Mwenye furaha ni wewe, Simoni mwana wa Yona, kwa sababu mwili na damu havikukufunulia hilo, bali Baba yangu aliye mbinguni ndiye aliyekufunulia.

Yohana 14; 28 Mlisikia nikiwaambia, ‘Ninaenda, nami nitakuja tena kwenu.’ Kama mngenipenda, mngeshangilia kwamba ninaenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.
 
Yohana 8:58
Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye IBRAHIMU ASIJAKUWAKO, MIMI NIKO.

NIKO ni jina la Mungu peke yake. Tunakutana na jina hilo pale Musa alipoongea na Mungu na kutumwa kuwakomboa wana wa Israeli kutoka Misri. Imeandikwa:

Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake n'nani? Niwaambie nini? Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO (Kutoka 3:13-14).

 
Isaya 9:6
Maana kwa ajili yetu MTOTO amezaliwa, Tumepewa MTOTO MWANAMUME; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, MUNGU MWENYE NGUVU, BABA WA MILELE, Mfalme wa amani.

Aya hii iko wazi kabisa. anayetajwa ni Yesu kwamba Yeye ni Mungu mwenye nguvu.

 
YESU NI NENO
Yohana 1:1
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye NENO ALIKUWA MUNGU.
 
Yohana 8:58

NWT: Jesus said to them: “Most truly I say to you, before Abraham came into existence, I have been.

TLB: Jesus: “The absolute truth is that I was in existence before Abraham was ever born!”

WE: Jesus answered, `I tell you the truth. I already was before Abraham was born.'

Hapa Yesu anaeleza kwamba alikuwepo kabla hata ya Ibrahimu kuzaliwa.
 
Nimekupa vifungu kibao huko juu, hata hivyo lengo langu si kubadili msimamo wako, unaweza endelea kuamini unavyoamini. Lakini lengo la huu uzi ni kuonesha ni jinsi gani sisi tunaomwamini Yesu kama Mungu Diamond Platnumz ametukosea ama lah!

Lengo la huu uzi siyo kujadili kwamba tunachoamini ni sahihi ama lah bali imani yetu inastahili heshima bila kujali Diamond Platnumz au wewe unakubaliana nayo ama lah.

Mimi kwa upande wako na wengine wenye hoja kama zako nimemaliza.
 
YESU NI NENO
Yohana 1:1
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye NENO ALIKUWA MUNGU.
Yohana 1:1

“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.”

Yohana 17:3

Uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na yule uliyemtuma, Yesu Kristo.

Yohana 20:17

Yesu akamwambia: “Acha kuning’ang’ania, kwa maana bado sijapanda kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu, nawe uwaambie, ‘Ninapanda kwenda kwa Baba yangu na Baba yenu na kwa Mungu wangu na Mungu wenu.

Bottomline: Kuna Mungu na mungu.

Ikiwa Yesu anamwabudu Mungu Yehova kwanini wewe umwabudu mungu Yesu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…