Diamond Platnumz Kufikishwa Mahakamani

MstahikiMeya

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2014
Posts
1,633
Reaction score
560


MSANII nyota wa muziki wa Bongo Flava nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz' huenda akaingia matatani baada ya juzi kupanda jukwaani kutumbuiza katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 akiwa amevaa sare ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kinyume cha sheria.

Tangu msanii huyo afanye hivyo, mjadala umeibuka kwa wengi wao kujiuliza nini maana yake na kama alifanya hivyo kwa kibali maalumu au la, hasa ikizingatiwa ni hivi karibuni Jeshi hilo lilitoa onyo kwa wasanii na wengineo kutotumia mavazi hayo.

Mbali ya Diamond, hata vijana wake nao walishambulia jukwaa wakiwa katika mavazi hayo, akiwemo msanii aliyemshirikisha katika moja ya nyimbo zake, Ney wa Mitego.

Wakati shoo hiyo ikiendelea, baadhi ya mashabiki walianza kumzomea kila alipoimba kabla ya video kubwa ambazo zilikuwa mbele ya jukwaa hilo kuanza kuonyesha picha za mnato na video za mwanamuziki huyo akiwa amevaa mavazi hayo huku akiwa kama askari ‘anayekoki' risasi katika katika bastora na baadaye katika bunduki ya kivita.

Kitendo hicho, kilionekama kuwakera zaidi maelfu ya wapenzi na mashabiki wa muziki waliokuwa wamejazana katika viwanja vya Leaders Club, huku kila mmoja akiwa na tafsiri yake.

Baada ya tukio hilo la juzi usiku, kitendo cha nyota huyo kuvalia mavazi hayo ya JWTZ, kimeibua mjadala hadi katika mitandao ya kijamii kuanzia jana asubuhi, ambapo picha za msanii huyo zikitumika kujenga hoja ya uhalali wa kufanya hivyo, huku vijana kadhaa wanaokutwa nazo mitaani wakiteswa vibaya na jeshi hilo.

Kwa upande wake Diamond, alitoa taarifa ndefu katika ukurasa wake wa Facebook na Instagram, akiishia kuelezea ni kwa nini alizomewa katika shoo hiyo.

Tanzania Daima ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura juu ya kitendo cha msanii huyo, alisema alikuwa hajui chochote na kuahidi kulifanyia kazi kama atapelekewa taarifa na wasaidizi wake.

Alipotafutwa Kaimu Msemaji wa JWTZ, Meja Joseph Msanja, simu yake iliita bila kupokelewa na alipotafutwa msaidizi wake, alikiri kupata taarifa na kujionea kupitia shoo hiyo, huku akisisitiza bosi wake anaweza kulizungumzia hilo.

Tukio hilo limefanyika ikiwa ni siku chache tu tangu kijana mmoja aliyekuwa amevalia mavazi ya kijeshi maeneo ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam, kuvuliwa na kupewa adhabu ya kuogelea katika dimbwi la maji machafu yaliyotuama.

Aidha, msanii Gwamaka Kaihula ‘Crazy GK' aliwahi kuhojiwa na Jeshi hilo kwa kutumia mavazi ya kijeshi katika kibao chake cha Simba wa Afrika, ambapo alijitetea pamoja na kuomba msamaha kwa kilichofanyika.

Kutokana na wimbi la watu mbalimbali hasa wasanii kuvalia mavazi yanayofanana na sare za jeshi hilo, hivi karibuni Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya JWTZ, ilionya kama ifuatavyo:

"Kumejitokeza kama fasheni kwa baadhi ya wasanii, hasa wanamuziki wa Bongo fleva, kurekodi video zao wakiwa wamevaa sare za jeshi kama vile suruali, viatu, fulana, kaptula, mabegi au kofia.

"Inawezekana kwa namna moja ama nyingine, baadhi ya watumiaji wa sare hizo hawafahamu ni kinyume cha sheria ya nchi kukutwa nazo, ingawa kutokujua sheria bado sio utetezi mbele ya mahakama.

"Mtu yeyote yule asiye na ruhusa ya kushona, kuuza au kuingiza nchini sare za jeshi, atakuwa ametenda kosa, kwa hiyo atafikishwa mahakamani na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.

"Katika uvaaji au uingizaji nguo, kama itatokea kwamba nguo hizo zinafanana kwa aina yoyote ile na zile za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, ikadhaniwa kuwa ni hizo, mtu huyo ana hatia na anastahili kufikishwa mahakamani na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria zinazohusu sare za majeshi zilizopo," ilifafanua taarifa hiyo.

Chanzo:Tanzania Daima

 
nchiii inawatu wapambavu sana yaani msanii kuvaanguo zinazofanana na jeshi basi ishakuwa story ya mjini
kila siku wanawaza ujinga tu
 
Habari ambazo zinaenea kwa kasi hapa mjini kwa sasa ni kuwa Dimond ameambiwa ndani ya saa 48 awe amereport makao makuu ya JWTZ akiwa na sare za jeshi hilo alizovaa siku ya Fiesta,
Kama hiki kitu ni kweli,basi washauri wa Ndomo wafanye mpango mapema kumpeleka kuliko hawa watu wamtafute wenyewe,
Kila la kheri bwana DANGOTE
 
Habari ambazo zinaenea kwa kasi hapa mjini kwa sasa ni kuwa Dimond ameambiwa ndani ya saa 48 awe amereport makao makuu ya JWTZ akiwa na sare za jeshi hilo alizovaa siku ya Fiesta,
Kama hiki kitu ni kweli,basi washauri wa Ndomo wafanye mpango mapema kumpeleka kuliko hawa watu wamtafute wenyewe,
Kila la kheri bwana DANGOTE
 
Aende tu apigwe intro ya masaa 8.Watu wengine wanadhani kuvaa sare za makamanda ni kitu rahisi tu.Makamanda lile kazi ilo.
Hapana kuchezea makamanda wa JWTZ.Lazma afanye kazi za watu..... Mpeni lonja jamaa
 
Aende na nguo za kubadilisha wasije wakamwambia apige mbizi kama yule jamaa wa kkoo aliyepigishwa mbizi kweye maji machafu.
 
Official report ingetolewa toka jana na Jeshi au tusubiri leo official toka jeshini
 
nawaza tu kwani huyu jamaa hana washauri?na kama anao ina maana wote hawajui sheria inasemaje kuhusu raia wa kawaida kuvaa sare za jeshi? au wanajiona masuperstar kila kona ya nchi? haya acha tusubirie
 
Wa kumkamata yuko wapi akat hao maaskar walikuwepo siku ya show
 
Aende tu apigwe intro ya masaa 8.Watu wengine wanadhani kuvaa sare za makamanda ni kitu rahisi tu.Makamanda lile kazi ilo.
Hapana kuchezea makamanda wa JWTZ.Lazma afanye kazi za watu..... Mpeni lonja jamaa

Ni kweli aende tu mtu ana zivaa wakati.hajafanya hata zoezi moja la jeshi tena anajipaka na wanja na lipstick anaimba nalo mwanaume hapo si kulozalilisha jeshi kwa mambo muhimu wanayo tenda tena jeshi letu lina heshimika kote sub saharan mana kuvaa hivo na wengine wataiga wataona kawaida kwa vile daimond alivaa na hakuchukuliwa hatua
 
Wewe si ulikua unamtetea yule mwingine aliyeoga pale k/koo?
 
Hiyo kesi natamani niwe wakili wake swali moja tu la msingi je amevaa nguo za JWTZ au zinazofanana na za JWTZ ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…