Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Tukubaliane kwa pamoja sasa kwamba Nasibu Abdul ‘Diamond' ni habari nyingine. Weka pembeni habari ya nyota, juhudi zake binafsi zimekuwa chachu ya kumfikisha alipo sasa. Inahitaji akili kuwa mbunifu na juhudi isiyosinzia kuchanja mbuga iliyowashinda wengine.
Hakuna wa kubisha kuwa Diamond Platnumz ndiye wa kwanza katika historia ya muziki Tanzania kufanikiwa kutengeneza mzani sawa kwa mambo makubwa matatu, moja ni sanaa yake, pili ni biashara, tatu ni kujiuza kimataifa. Hakika, kwa sasa Diamond ‘Mwanatandale' ni msanii mkubwa Afrika. Ukibisha kichaa!
Kwa muda mrefu, taifa lilikuwa likifeli kwenye medani ya sanaa. Wamepita wasanii wengi wazuri. Kazi zao zilisikika na kuteka jamii ya Kitanzania kwa upana wake. Walichoshindwa ni kutengeneza mzani sawa japo kwa mambo mawili tu, sanaa na biashara.
Diamond ameweza matatu! Amebakiza moja, kuliteka soko la kimataifa kwa upana wake, yaani duniani kote kazi zake zifike, asikike na kutumbuiza. Siyo hizo ‘shoo' za kualikwa Ulaya na Marekani kwenda kuwatumbuiza Watanzania na Waafrika wachache wanaoishi huko, anahitaji kukonga nyoyo za jumla. Akialikwa Uingereza, raia wenyewe wa nchi hiyo wapate mshawasha wa kumuona.
Sina shaka na jitihada alizonazo Diamond pamoja na timu yake katika kuhakikisha kazi zake zinafika mbali zaidi. Ni suala la muda tu na kumuombea Mungu, atafanikiwa. Hakuna wa kuzuia, mbingu pekee ndiyo kikomo (sky is the limit).
KWANZA HEKO YA MTV
Usiku wa Julai 18, mwaka huu (Jumamosi), Diamond aliendeleza kile ambacho alikuwa ameshakianza katika Tuzo za MTV Africa Music (MAMA) ambazo huratibiwa na kituo cha kimataifa cha televisheni cha MTV Base.
Kwa tuzo za mwaka huu, Diamond aliteuliwa kuwania tuzo katika vipengele vitatu, Msanii Bora wa Kiume Afrika, Mtumbuizaji Bora Afrika na Wimbo Bora wa Kushirikiana, Bumbum alioimba na Mnigeria Iyanya Onoyom Mbuk.
Mwaka huu, ilikuwa ni mara ya nne, Diamond kushiriki Tuzo za MTV Africa Music, na bila utani, katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Durban International Convention Center, jijini Durban, Jimbo la KwaZulu-Natal, Afrika Kusini, alithibitisha ‘msuli' alionao hivi sasa.
Diamond alinyakua Tuzo ya Mtumbuizaji Bora Afrika, akawaachia hizo nyingine. Bila shaka atazichukua kipindi kingine kijacho. Tuzo hiyo ya mtumbuizaji bora haina ubishi kwa sababu uwezo wa Diamond na timu yake jukwaani unajulikana. Wanamuziki wengi wanaheshimu shughuli yake anapokabidhiwa jukwaa.
Hayo ni mafanikio makubwa zaidi kwa muziki wa Diamond na sanaa ya Tanzania kwa jumla. Amefika kule ambako watangulizi wake walishindwa. Na amefika akiwa na umri mdogo, hivyo ni wazi anaweza kufika mbali zaidi kama ataendeleza nidhamu ya kazi aliyonayo kwa sasa.
KUNA KAMA DIAMOND?
Tunakubaliana pia hakuna! Zingatia kuwa hakijapita kitambo kirefu tangu alipotoka kutungua tuzo tatu za Channel O Music Video na kuandika historia mpya. Alishinda Tuzo ya Msanii Bora Chipukizi, Msanii Bora Afrika Mashariki na Msanii Bora wa Afro Pop.
Kwa kifupi usiongelee utitiri wa tuzo ambazo ameshazikamata. Ni nyingi na kwa asilimia kubwa hata Diamond mwenyewe ukimsimamisha barabarani akutajie idadi kwa haraka unaweza ukakutana na moja kati ya majibu matatu. Anaweza kukwambia hakumbuki, au akakutajia idadi batili, na si ajabu akababaika bila kutoa jawabu.
Ndiye msanii namba moja Tanzania kwenye maeneo mengi. Kwa kujaza watu katika maonesho yake ndani na nje ya nchi, kuuza kazi zake hususan nyimbo kwenye miito ya simu (ringtones), kupata mialiko yenye malipo makubwa kwenye kampeni za kisiasa na zile za kibiashara, vilevile kwa kusaini mikataba ghali zaidi ya kibiashara (endorsements).
ANA KAWAIDA YA KUJISAHAU
Ni ukweli hapaswi kuwa na dharau kwa sababu ya mafanikio yake lakini lazima akumbuke yeye ni nani. Inawezekana vipi pale alipo ambapo anaangaliwa na kila mfuatiliaji wa muziki na sanaa kwa jumla, asisemwe kwa mabaya na mazuri? Yeye Diamond ni nani hasa asisemwe?
Je, hajiangalii alipotoka? Na hajioni mahali alipo leo? Kama ndivyo, anataka kutegemea watu wakae kimya na wasimseme? Vema akubali kuwa gumzo katika kada mbalimbali. Lazima asemwe vizuri na wale wanaompenda na wasiompenda hawawezi kukosekana, watamshambulia tu!
Yesu (Nabii Isa) na utakatifu wake wote lakini alisemwa maneno ya kila aina na alidhalilishwa. Mtume Muhammad (SAW), alishambuliwa, alipigwa na kutupiwa kejeli za kila aina. Ni kwa nini walipata madhila wakati nao walikuwa wanafanya kazi ya Mwenyezi Mungu?
Ni kwamba ileile kazi yao ya kulitangaza neno la Mungu (SW), ilikuwa kero kwa wengine. Diamond hapa angejiuliza, kama kazi ya Mungu manabii na utakatifu wao walipingwa na kushambuliwa, itakuwa yeye na muziki wake ambao ukiachana na ushabiki pamoja na hoja za kuitangaza nchi, mafanikio ya jumla ni yake binafsi.
Diamond anataka asisemwe! Mbona anajisahau? Anasahau ni yeye, dada na mama yake walichangia chumba cha kulala wakati umri ukiwa umeshasogea na kila mmoja alihitaji faragha yake. Yalikuwa maisha ya dhiki Tandale, akiwa hana chochote cha kumiliki. Leo hii ni supastaa mkubwa Tanzania na Afrika. Kweli asisemwe?
Anamiliki majumba, magari, amebadilisha maisha ya mama yake na familia yake yote. Anamiliki kampuni yenye timu kubwa ya watu na kila mmoja anamtegemea yeye na inaonekana kabisa kwamba maisha hayagombi kwa kila mfanyakazi wake. Kila kitu upande wake kinasomeka juu ya mstari!
Mafanikio yake hajui kama kuna wengine yanawachoma? Ina maana hilo halijui? Anataka asifiwe tu! Wangapi amewakuta na kuwapita, anadhani wanafurahia matokeo? Mbona ni wengi wanapambana kufikia alipo na wanafeli, hao nao wamchekee tu!
Diamond aache kujisahau, atambue kuwa yeye ni kioo. Na kwa mafanikio yake anahitaji kujua yeye ni jalala la Mzungu, visafi na vichafu vitatupwa kwake. Anachopaswa kufanya ni kuongeza juhudi ya kazi. Vilevile akitambua kuwa kadiri anavyofanya kazi nzuri na kufanikiwa zaidi ndivyo atakavyoendelea kuongeza idadi ya marafiki, mashabiki, wanafiki na maadui kwa wakati mmoja.
AMEKUWA WA KIMATAIFA, AACHE ‘ULOKO'
Diamond ni wa kimataifa, anapaswa kuacha Uswahili, yaani tabia za ‘kiloko'. Julai 19, mwaka huu, baada ya kunyakua Tuzo ya MTV Africa Music, Mtumbuizaji Bora, ‘aliposti' kwenye akaunti zake za Instagram na Facebook, video ya modo, Jokate Mwegelo, akicheza wimbo Mdogomdogo, ulioimbwa na yeye mwenyewe Diamond.
Jokate, mbali na mitindo, ni mjasiriamali katika eneo la ubunifu wa mavazi, vilevile ni mrembo aliyeshika nafasi ya pili kwenye fainali za Miss Tanzania 2006, akitokea kuwa malkia wa Temeke. Huku nyuma ilishathibitika Diamond kuwa na uhusiano na Jokate kisha wakaachana.
Upepo ulipita katikati, ikadaiwa kuwa Jokate yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki hasimu wa Diamond, Ali Kiba. Hata hivyo, wote wawili wamekuwa wakikanusha, wakieleza kuwa urafiki wao ni wa kikazi, hakuna mapenzi katikati. Ya ngoswe mwachie ngoswe, watajijua wenyewe na mapenzi yao, ama ni kweli au uongo!
Uloko wa Diamond unaonekana katika maneno aliyoyaandika akisindikiza video hiyo ya Jokate, alisema: "Mbona bado, mtanyooka tu." Swali, je, Diamond alitaka kufikisha nini kwenye maneno hayo? Anataka kuwanyoosha akina nani? Jokate na Ali Kiba wake au nani mwingine?
Ni kweli kwamba Jokate alimfanyia kampeni kubwa Ali Kiba mpaka akatwaa tuzo sita za Kilimanjaro Tanzania Music (KTMA) 2014-2015, wakati yeye Diamond aliambulia mbili tu. Je, baada ya hapo Diamond aliandika uadui kiasi kwamba hataki kuona Jokate anacheza wimbo wake popote?
Jokate mwenyewe anasema video hiyo ni ya zamani na si kweli kuwa alirekodiwa akishangilia ushindi wa Diamond. Mimi nasema hata kama ni kweli alishangilia ushindi wa Diamond MTV Afrika, kulikuwa na ubaya gani?
Tunaweza kupingana nyumbani lakini tukakubaliana ugenini. Kwamba KTMA Diamond alikuwa anashindana na Watanzania wenzake lakini MAMA, alishindana na wanamuziki wa mataifa mengine. Kuna ubaya gani wote bila kuangalia tofauti za nyuma, kuungana kumsapoti ashinde kimataifa? Na baada ya ushindi kushangilia?
Kimsingi Diamond ameonesha Uswahili wa kiwango cha juu. Sisi sote ni Waswahili lakini Uswahili ninaoumaanisha ni zile tabia za fifi, inda, kinyongo na kadhalika. Ni tabia za kiloko ambazo Diamond anatakiwa kuachana nazo, hazitamsaidia, hazitaongeza chochote katika safari yake.
Muhimu ni kufahamu kuwa mpaka jua literemke haitatokea apendwe na watu wote. Anapopendwa na kuchukiwa, hana budi kuheshimu na kutambua kwamba hayo ni matunda ya kazi yake. Hey dogo, jitambue sasa, weka uloko wako pembeni, fanya kazi zaidi na uzidi kutisha zaidi!
By Luqman Maloto