Diamond Platnumz; Mafanikio ya Kimataifa, Tabia za 'Kiloko'

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
1,016
Reaction score
2,195
Tukubaliane kwa pamoja sasa kwamba Nasibu Abdul ‘Diamond' ni habari nyingine. Weka pembeni habari ya nyota, juhudi zake binafsi zimekuwa chachu ya kumfikisha alipo sasa. Inahitaji akili kuwa mbunifu na juhudi isiyosinzia kuchanja mbuga iliyowashinda wengine.

Hakuna wa kubisha kuwa Diamond Platnumz ndiye wa kwanza katika historia ya muziki Tanzania kufanikiwa kutengeneza mzani sawa kwa mambo makubwa matatu, moja ni sanaa yake, pili ni biashara, tatu ni kujiuza kimataifa. Hakika, kwa sasa Diamond ‘Mwanatandale' ni msanii mkubwa Afrika. Ukibisha kichaa!

Kwa muda mrefu, taifa lilikuwa likifeli kwenye medani ya sanaa. Wamepita wasanii wengi wazuri. Kazi zao zilisikika na kuteka jamii ya Kitanzania kwa upana wake. Walichoshindwa ni kutengeneza mzani sawa japo kwa mambo mawili tu, sanaa na biashara.

Diamond ameweza matatu! Amebakiza moja, kuliteka soko la kimataifa kwa upana wake, yaani duniani kote kazi zake zifike, asikike na kutumbuiza. Siyo hizo ‘shoo' za kualikwa Ulaya na Marekani kwenda kuwatumbuiza Watanzania na Waafrika wachache wanaoishi huko, anahitaji kukonga nyoyo za jumla. Akialikwa Uingereza, raia wenyewe wa nchi hiyo wapate mshawasha wa kumuona.

Sina shaka na jitihada alizonazo Diamond pamoja na timu yake katika kuhakikisha kazi zake zinafika mbali zaidi. Ni suala la muda tu na kumuombea Mungu, atafanikiwa. Hakuna wa kuzuia, mbingu pekee ndiyo kikomo (sky is the limit).

KWANZA HEKO YA MTV
Usiku wa Julai 18, mwaka huu (Jumamosi), Diamond aliendeleza kile ambacho alikuwa ameshakianza katika Tuzo za MTV Africa Music (MAMA) ambazo huratibiwa na kituo cha kimataifa cha televisheni cha MTV Base.

Kwa tuzo za mwaka huu, Diamond aliteuliwa kuwania tuzo katika vipengele vitatu, Msanii Bora wa Kiume Afrika, Mtumbuizaji Bora Afrika na Wimbo Bora wa Kushirikiana, Bumbum alioimba na Mnigeria Iyanya Onoyom Mbuk.

Mwaka huu, ilikuwa ni mara ya nne, Diamond kushiriki Tuzo za MTV Africa Music, na bila utani, katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Durban International Convention Center, jijini Durban, Jimbo la KwaZulu-Natal, Afrika Kusini, alithibitisha ‘msuli' alionao hivi sasa.

Diamond alinyakua Tuzo ya Mtumbuizaji Bora Afrika, akawaachia hizo nyingine. Bila shaka atazichukua kipindi kingine kijacho. Tuzo hiyo ya mtumbuizaji bora haina ubishi kwa sababu uwezo wa Diamond na timu yake jukwaani unajulikana. Wanamuziki wengi wanaheshimu shughuli yake anapokabidhiwa jukwaa.

Hayo ni mafanikio makubwa zaidi kwa muziki wa Diamond na sanaa ya Tanzania kwa jumla. Amefika kule ambako watangulizi wake walishindwa. Na amefika akiwa na umri mdogo, hivyo ni wazi anaweza kufika mbali zaidi kama ataendeleza nidhamu ya kazi aliyonayo kwa sasa.

KUNA KAMA DIAMOND?
Tunakubaliana pia hakuna! Zingatia kuwa hakijapita kitambo kirefu tangu alipotoka kutungua tuzo tatu za Channel O Music Video na kuandika historia mpya. Alishinda Tuzo ya Msanii Bora Chipukizi, Msanii Bora Afrika Mashariki na Msanii Bora wa Afro Pop.

Kwa kifupi usiongelee utitiri wa tuzo ambazo ameshazikamata. Ni nyingi na kwa asilimia kubwa hata Diamond mwenyewe ukimsimamisha barabarani akutajie idadi kwa haraka unaweza ukakutana na moja kati ya majibu matatu. Anaweza kukwambia hakumbuki, au akakutajia idadi batili, na si ajabu akababaika bila kutoa jawabu.

Ndiye msanii namba moja Tanzania kwenye maeneo mengi. Kwa kujaza watu katika maonesho yake ndani na nje ya nchi, kuuza kazi zake hususan nyimbo kwenye miito ya simu (ringtones), kupata mialiko yenye malipo makubwa kwenye kampeni za kisiasa na zile za kibiashara, vilevile kwa kusaini mikataba ghali zaidi ya kibiashara (endorsements).

ANA KAWAIDA YA KUJISAHAU
Ni ukweli hapaswi kuwa na dharau kwa sababu ya mafanikio yake lakini lazima akumbuke yeye ni nani. Inawezekana vipi pale alipo ambapo anaangaliwa na kila mfuatiliaji wa muziki na sanaa kwa jumla, asisemwe kwa mabaya na mazuri? Yeye Diamond ni nani hasa asisemwe?

Je, hajiangalii alipotoka? Na hajioni mahali alipo leo? Kama ndivyo, anataka kutegemea watu wakae kimya na wasimseme? Vema akubali kuwa gumzo katika kada mbalimbali. Lazima asemwe vizuri na wale wanaompenda na wasiompenda hawawezi kukosekana, watamshambulia tu!

Yesu (Nabii Isa) na utakatifu wake wote lakini alisemwa maneno ya kila aina na alidhalilishwa. Mtume Muhammad (SAW), alishambuliwa, alipigwa na kutupiwa kejeli za kila aina. Ni kwa nini walipata madhila wakati nao walikuwa wanafanya kazi ya Mwenyezi Mungu?

Ni kwamba ileile kazi yao ya kulitangaza neno la Mungu (SW), ilikuwa kero kwa wengine. Diamond hapa angejiuliza, kama kazi ya Mungu manabii na utakatifu wao walipingwa na kushambuliwa, itakuwa yeye na muziki wake ambao ukiachana na ushabiki pamoja na hoja za kuitangaza nchi, mafanikio ya jumla ni yake binafsi.

Diamond anataka asisemwe! Mbona anajisahau? Anasahau ni yeye, dada na mama yake walichangia chumba cha kulala wakati umri ukiwa umeshasogea na kila mmoja alihitaji faragha yake. Yalikuwa maisha ya dhiki Tandale, akiwa hana chochote cha kumiliki. Leo hii ni supastaa mkubwa Tanzania na Afrika. Kweli asisemwe?

Anamiliki majumba, magari, amebadilisha maisha ya mama yake na familia yake yote. Anamiliki kampuni yenye timu kubwa ya watu na kila mmoja anamtegemea yeye na inaonekana kabisa kwamba maisha hayagombi kwa kila mfanyakazi wake. Kila kitu upande wake kinasomeka juu ya mstari!

Mafanikio yake hajui kama kuna wengine yanawachoma? Ina maana hilo halijui? Anataka asifiwe tu! Wangapi amewakuta na kuwapita, anadhani wanafurahia matokeo? Mbona ni wengi wanapambana kufikia alipo na wanafeli, hao nao wamchekee tu!

Diamond aache kujisahau, atambue kuwa yeye ni kioo. Na kwa mafanikio yake anahitaji kujua yeye ni jalala la Mzungu, visafi na vichafu vitatupwa kwake. Anachopaswa kufanya ni kuongeza juhudi ya kazi. Vilevile akitambua kuwa kadiri anavyofanya kazi nzuri na kufanikiwa zaidi ndivyo atakavyoendelea kuongeza idadi ya marafiki, mashabiki, wanafiki na maadui kwa wakati mmoja.

AMEKUWA WA KIMATAIFA, AACHE ‘ULOKO'
Diamond ni wa kimataifa, anapaswa kuacha Uswahili, yaani tabia za ‘kiloko'. Julai 19, mwaka huu, baada ya kunyakua Tuzo ya MTV Africa Music, Mtumbuizaji Bora, ‘aliposti' kwenye akaunti zake za Instagram na Facebook, video ya modo, Jokate Mwegelo, akicheza wimbo Mdogomdogo, ulioimbwa na yeye mwenyewe Diamond.

Jokate, mbali na mitindo, ni mjasiriamali katika eneo la ubunifu wa mavazi, vilevile ni mrembo aliyeshika nafasi ya pili kwenye fainali za Miss Tanzania 2006, akitokea kuwa malkia wa Temeke. Huku nyuma ilishathibitika Diamond kuwa na uhusiano na Jokate kisha wakaachana.

Upepo ulipita katikati, ikadaiwa kuwa Jokate yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki hasimu wa Diamond, Ali Kiba. Hata hivyo, wote wawili wamekuwa wakikanusha, wakieleza kuwa urafiki wao ni wa kikazi, hakuna mapenzi katikati. Ya ngoswe mwachie ngoswe, watajijua wenyewe na mapenzi yao, ama ni kweli au uongo!

Uloko wa Diamond unaonekana katika maneno aliyoyaandika akisindikiza video hiyo ya Jokate, alisema: "Mbona bado, mtanyooka tu." Swali, je, Diamond alitaka kufikisha nini kwenye maneno hayo? Anataka kuwanyoosha akina nani? Jokate na Ali Kiba wake au nani mwingine?

Ni kweli kwamba Jokate alimfanyia kampeni kubwa Ali Kiba mpaka akatwaa tuzo sita za Kilimanjaro Tanzania Music (KTMA) 2014-2015, wakati yeye Diamond aliambulia mbili tu. Je, baada ya hapo Diamond aliandika uadui kiasi kwamba hataki kuona Jokate anacheza wimbo wake popote?

Jokate mwenyewe anasema video hiyo ni ya zamani na si kweli kuwa alirekodiwa akishangilia ushindi wa Diamond. Mimi nasema hata kama ni kweli alishangilia ushindi wa Diamond MTV Afrika, kulikuwa na ubaya gani?

Tunaweza kupingana nyumbani lakini tukakubaliana ugenini. Kwamba KTMA Diamond alikuwa anashindana na Watanzania wenzake lakini MAMA, alishindana na wanamuziki wa mataifa mengine. Kuna ubaya gani wote bila kuangalia tofauti za nyuma, kuungana kumsapoti ashinde kimataifa? Na baada ya ushindi kushangilia?

Kimsingi Diamond ameonesha Uswahili wa kiwango cha juu. Sisi sote ni Waswahili lakini Uswahili ninaoumaanisha ni zile tabia za fifi, inda, kinyongo na kadhalika. Ni tabia za kiloko ambazo Diamond anatakiwa kuachana nazo, hazitamsaidia, hazitaongeza chochote katika safari yake.

Muhimu ni kufahamu kuwa mpaka jua literemke haitatokea apendwe na watu wote. Anapopendwa na kuchukiwa, hana budi kuheshimu na kutambua kwamba hayo ni matunda ya kazi yake. Hey dogo, jitambue sasa, weka uloko wako pembeni, fanya kazi zaidi na uzidi kutisha zaidi!

By Luqman Maloto
 
Big up kwa aliyeandika hii, nacomment hapa kistaarabu kwakuwa hajaandika kishabiki, kabalance story na kuandika ukweli. Mimi ni shabiki wa Diamond na nakiri hapo alikosea, hapaswi kuwajibu haters, inatakiwa aendelee kufocus kwenye kazi zake kufanya vitu vizuri zaidi ili kuwaprove wrong haters, na namsifu maranyingi huwa hawajibu haters, ni marachache kumuona amefanya hivyo na akifanya hivyo jua 'limemfika hapaa' (in gossipcobb voice).

Siwezi kumlaumu sana yeye ni binadam kama binadam wengine, anamoyo, vitu vingine vinauzi ujue, unapoanza kumpigia kampeni Davido kwa lengo la kumshusha mtanzania mwenzako atoke kapa inakera kwa kweli, kama unampigia kura Davido piga kimyakimya, hawa wadada wawili Wema na Jokate timu zao ndio zilifanya huo upuuzi, hata ningekuwa Mimi 'kibinadam' ningefanya kama alivyofanya Diamond, inakera sio kidogo. Watu wamefanya kampeni za kumshusha nyumbani wakaona haitoshi wakahamia na ugenini hii INAKERA kwakweli.

Halafu nikurekebishe kidogo, hiyo haimaanishi kwamba wasanii inteneshno ndo hawana tabia za ajabu ajabu, marangapi tunasikia hawa inteneshno wanagombana tena kwenye social network kwa mambo ya kipuuz eg kugombea mademu?

Chris Brown deile anagombana kwa mambo ya madem huko twitter, Meek Mill sahivi anaandika ujingaujinga huko insta kumuhusu Drake kisa kagongewa demu wake Nicki Minaj, 50 Cent hapa majuzi kapandishwa kizimbani kwa kosa la kuupload sex tape ya ex girlfriend wa hasimu wake rickross matandaoni, kumbe hata hawa inteneshno tunaowaamini nao wana tabia za kiloko teh teh....!!!!
 
Ndugu yangu MR. CONFIDENT

Tasnia ya burudani ni tasnia ya ajabu kidogo na inawezekana uajabu huu unatokana sana na asili wadau wake na wale wanaowazunguka!!! Nakumbuka mwaka jana ilipotokea misunderstanding kati ya Diamond na Davido, binafsi niliweka ushabiki pembeni na nikalaani sana alichofanya Diamond! I was too emotion kiasi kwamba nikamtumia message mmoja wa watu wake! Hata hivyo, baada ya kutulia na akili kunirejea, kwanza nikajilaumu nikajiona boya kishenzi kwa nguvu niliyotumia kulaani hadi kufikia kumwandikia huyo jamaa ambae alijibu kwa kifupi sana baadae "chige bhana....!" hapo kwenye chige palikuwa na jina langu!!!

Ninachotaka kusema ni nini? Hawa watu wanaishi dunia tofauti sana na hii tunayoitaka sisi and trust me, ukitaka kupasuka kichwa, basi jaribu kufuatilia maisha ya wasanii... na hii si kwa Diamond tu bali na kwa wengine pia, including hao waliopo huko huko wanakojiona wamestaarabika! Zipo few exceptions... VERY FEW ambazo kimsingi zinatokana sana na vile mtu alivyoumbwa... kuna wengine wanaumbwa na pengine kukulia mazingira ya ukimya; si watu wa maneno maneno... hizo few exceptions ni za watu kama akina Ali Kiba hivi, Mwana-FA na wachache wengin ambao wanaweza kuwa wamefikia mafanikio lakini bado wakawa vile vile! Kwa bahati mbaya, hata kwenye maisha ya kawaida hao wati waliozaliwa na karama za upole na pengine unyenyekevu si wengi!!!

Tukija kwenye tasnia ya burudani sasa... majority wanaingia wakiwa na umri mdogo na baada ya hapo inakuwa wanatumia muda mdogo sana na akina mjomba, shangazi, mama n.k na badala yake huwa wanazungukwa na watu ambao hawana time ya kukuambia this's not good at all!

Mchukulie Davido kwa mfano! Yule jamaa ni mtoto wa kishua; amekulia Marekani, home pesa zipo lakini kimsingi kimatendo wala hana tofauti na mtu kama Diamond!! Rudi Marekani kwenyewe, angalia wasanii waliopo, wengi wanakuja kuacha mambo ya hovyo hovyo baadae sana! Mwangalie Chris Brown; mwangalie Justin Beiber... wote ni watu wa hovyo hovyo! It's very unfortunately kwa kuwa wewe ni Mtanzania unaweza usifahamu tabia za kiloko za Wamarekani... Nenda kwa Waingereza kwa mfano; kama huna uzoefu nao unaweza kuamini kwamba Kiingereza chao sawa lakini waliozoweana, ni kama sisi hapa mtu hata akiongea Kiswahili, unaweza kufahamu kwamba huyu ni Mchaga, Msukuma, Mmakonde n.k!!!

Hivyo basi, hakuna kundi pasua kichwa duniani kama kundi la wasanii na kama hutaki kuumiza kichwa, penda kazi zao mengine achana nayo... mwachie mwenyewe na ndugu zake!!! Lakini kama una mpango wa kususia burudani, basi jaribu kuyafanya maisha ya hawa jamaa kuwa ni sehemu ya mahaba yako kwao!!! Yaani wala usitarajie eti mtu kama Diamond anaweza kuja kubadilika... huenda akabadilika with age!
 
Last edited by a moderator:
luqman maloto! Umechambua vizuri sana, akitaka kuelewa atakuelewa na atabadilika (kama akiridhika kuwa uswahili ni tabia mbaya) asipotaka hataelewa na ni lazima tuheshimu alivyoamua kuishi.

Sio lazima unavyoishi wewe na mwenzio aishi hivyo hivyo. Life is too short to be normal, if you think he is mswahili then it's okay!
Mtu kuwa kioo cha jamii haimaanishi kila siku tumpangie namna ya kuishi. Haimaanishi kila siku aishi kwa kuiridhisha jamii.
Kizuri nilichogundua kwenye uchambuzi wako ni kwamba People will always have something to criticise when they see progress, and that's a sign that your far better than them and it hurts them. Pointing out someone's wrong doings is very easy task, But at least Luqman maloto appreciates.
 
Sometimes heshima kitu cha bure,niliona aibu alipopewa tuzo kaanza kuongea vizuri kwa english,alipoongea kwa kiswahili akapiga kelele ""papapapapaaah paaah '',kama anauza mitumba tandale.
 
Sometimes heshima kitu cha bure,niliona aibu alipopewa tuzo kaanza kuongea vizuri kwa english,alipoongea kwa kiswahili akapiga kelele ""papapapapaaah paaah '',kama anauza mitumba tandale.

hahahaha embu acha hizoo, sema hajui maswaga flani amazing ya kikatoliki..

huonagi ongea ya yemi alade??
 
Mtoa mada umenena, lakini ukae ukijuwa hivyo ni vitu vya kawaida tu...

Wizkid alikuwa anatupiana maneno na skales juzi kati hapa, vipi ingekuwa kwa diamond nadhani ungefungulia threds kumi... Uswahili upo tu!!

Kwa meekmill kinachoendelea sasahivi na drake ni uswahili???

Alichopost rihanna jana twitter kwamba anatembea na Jay z tena na kumtag beyonce kwenye hiyo tweet ni utandale???

KILA MTU ANA MAISHA YAKE KUNA VITU VIDOGO SANA KALE KALIKUWA KAKIJEMBE FLANI AMAZING TU!!!!
 
Mmh hongera una muda kweli wa kuandika kuhusu maisha ya watu!. Mi kusoma tu nimeshindwa.
Wacha nimalizie kitabu changu cha 'The Magic of Thinking Big' naona kinanisaidia.

Mkuu iko kitabu nakitaka sana sana
 
Aisee inauma sana kuona watz wenzako wanaongoza kampeni kupigia kura wanaijeria ili akose

Kwa mtoto wa kiswazi kama Chibu ilikua ni ngumu sana kukaa bila kuwajibu kiswahi swahili
Msamehe bure
 
MeekMill anamdiss Drake, sasa hivi kuna misunderstanding lakini watu wanaona ni internet beefing. Tumewahi kuona diss kutoka kwa mahardcore kabisa kama Eminem au Snoop Doggy tena wakieleza kwa madem. Chriss Brown alisharusha maneno kwa X wake. Tumeshaona beef za kwenye internet kama Iggy Azalea vs Snoop Doggy, Iggy Azalea vs Eminem, Iggy vs Britney Spears, Taylor Swift vs Katy Perry......Yaani orodha ni ndefu. Na hawa ni wamarekani wala sio waswahili.
 
mwenyewe alishaga sema yeye ni mswahili wa tandale hakuna haja ya kuumia kichwa pigeni kazi mukomboe familia zenu!
 
Halafu tasnia ya burudani bhana, sijui ipo vipi!!! Kwanza ukijifanya wewe ni mtoto mzuri sana, una nidhamu, mtiifu, mtoto wa mzee wa kanisa, mtoto mwenye heshima, na mambo mengine kama hayo, trust me, unakuwa unaboa ile mbaya!! Kama we ni wa hivyo, kiroho safi tu, rudi kanisani kafanye collabo na akina Christina Shusho au kama vipi jichanganye na kaswida na huku waachie waliolanduka... ukizingua watu wanakuzingua vile vile na wakikuzingua; hakuna mambo ya "mi namwachia Mungu, atanilipa" huku... kwanza mambo yenyewe washatuambia haramu, halafu unatarajia nini!!!
 

Well said ,na nahis ndo maana mtu kama beni pal ,rich mavoko kuimba wapo vizuri sana ila hawana mambwembwe mengi hawafanyi mtu uwe curious
 
Well said ,na nahis ndo maana mtu kama beni pal ,rich mavoko kuimba wapo vizuri sana ila hawana mambwembwe mengi hawafanyi mtu uwe curious
Umeona enh?! Kwa mtazamo wangu umemwacha na Bell Center Forward... halafu huwa namkubali sana Amin... lakini wapi!! Muziki ni fani ya machizi na hata huko kwenye Injili wanaofahamika ni wale wale machizi machiz wale!!! Huyo Michael Jackson mwenyewe pamoja na maisha yake yote ya kujificha ficha kama digidigi lakini alikuwa full of drama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…