Diamond platnumz usichoke, endelea kuwa shule kwa wasanii wetu

Diamond platnumz usichoke, endelea kuwa shule kwa wasanii wetu

Kidingi

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2012
Posts
1,872
Reaction score
1,832
Hakika Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla tunajisifu sana na uwepo wako hata wale wasiofuatilia muziki kwa juhudi, uthubutu, kujituma, na heshima yako inatoa fundisho kubwa sana.

Huyu mtu hakika ni chuo cha Bongo flavour, na haikukosewa kabisa kumuita Nembo ya Taifa la Tanzania, bado tu kutengeneza sanamu yake na kuipa barabara/shule/hospitali jina lake kumuenzi, kwani amekuwa chachu ya maendeleo ya vijana wengi hususani wanamuziki, na wengi wamekiri hili wakiwemo Joh makini, alikiba, Sauti sol, Vanessa mdee, Belle 9, Nicki wa pili, n.k.

Huwezi ukaandika mazuri ya huyu mtu afu ukamaliza kwani ni mengi mno.

Huyu jamaa ukianzia kwenye label yake tu ameonyesha heshima ya muziki wake, kwani unaendesha familia nyingi mno. Wakati wasanii wengine wakifanya mambo kienyeji, kufanya muziki ili kupata pesa kula bata mjini huku wakisahau kuwekeza zaidi kwenye kazi zao, diamond amewapa mwangaza kwenye hili.

Kuanzia kwenye management, kwa Tanzania anao mameneja si chini ya wa4 salam, babu tale, fela na ricardo momo, bado Nigeria ana manager mmoja Paulo. Ana mpiga picha wake(kifesi), ana mchukua video wake(akili), anao madancers wa kudumu zaidi ya 6, ana mlinzi wake. Bado kwenye ofisi za WCB kuna waajiliwa, akiwemo producer, msimazi wa ofisi, n.k

Kama haitoshi akatuletea Harmonize ambae kwa video yake ya kwanza tu kafanikiwa kuonekana hadi mtv base kitu ambacho wasanii kama alikiba, richi mavoko, ben pol, barnaba, hawajawahi kufanikisha,,, ila diamond kwa moyo mkunjufu kamtoa harmo mtaani alikokuwa muuza chai kariakoo, na muda mwingine kuuza mitumba karume akamuhudumia kisanaa mpaka kufikia alipo, na wiki iliyopita alikuwa anashoot video yake ya pili na God father hapa nchini pamoja na RAYMOND msanii mpya anayesimamiwa na diamond.

Diamond hakuwa wa kwanza kuanza kuwekeza kimataifa, kulikuwa na AY hapo kabla.. Ila ukijiuliza kwanini kumekuwa na kasi kubwa ya wasanii wetu kukazana kutoka kimataifa kuanzia 2015? Hii imetokana na mafanikio ya Diamond, ambaye ameifanya Tanzania itambulike kimuziki pia.. Mafanikio yake yamewafanya wasanii waone kunauwezekano wa kufanya haya na ukafanikiwa, hamasa ambayo haikuwepo hapo mwanzoni.

Ikumbukwe mengi sana amefanya huyu mtu, kipindi wasanii wanalipwa pesa ndogo sana kwenye show Diamond alianza kuwaonyesha thamani yao, ambapo 2013 mwanzoni akasema bila milioni kumi siwezi kutumbuiza kwenye show, na jinsi alivyokuwa anafanya vizuri gharama ikazidi kupanda mpaka 2014 baada ya kutoa my number one remix ikawa milioni 25, mpaka mwaka huu kuja kulipwa milioni 100 kwenye tigo kiboko yao concert pesa ambayo wasanii wengine zaidi ya kumi gharama ndio inafikia hiyo..

VIVA DIAMOND PLATNUMZ, KING OF AFROPOP
 
DIAMOND PLATINUMZ ndiyo msanii pekee ambaye kama wewe unataka utoke kimziki basi jifanye unabifu naye hakika utatoka kwasababu utapata sapoti kutoka kwa alimwagana nao kimapenzi na wasanii wenzake aliowapita kimuziki na kimafanikio na utajihisi wewe unajua sana muziki kumbe watu wamepata pa kupunguzia hasira zao. Lakini si wanunuzi wa kazi zako wala mambo yako kukuingizia pesa hawakupi sapoti ukitaka kudhibitisha hilo waangalie wanaojifanya wanabifu nae aina ya mashabiki walionao ( mfano halisi ni mlinzi wa tembo ) asante Kidingi kwa uzi mzuri sana kwa ajili ya Icon wetu.
 
Last edited by a moderator:
Apo umesema ukweli na chnginee jaman ukogwe kazini sio ufanisi ilaa niaa ndio ufanisi mzuri mfano DIAMOND ni msanii mwenye nia kubwa na mziki wa TANZANIA na AFRIKA kwa ujumla
 
DIAMOND PLATINUMZ ndiyo msanii pekee ambaye kama wewe unataka utoke kimziki basi jifanye unabifu naye hakika utatoka kwasababu utapata sapoti kutoka kwa alimwagana nao kimapenzi na wasanii wenzake aliowapita kimuziki na kimafanikio na utajihisi wewe unajua sana muziki kumbe watu wamepata pa kupunguzia hasira zao. Lakini si wanunuzi wa kazi zako wala mambo yako kukuingizia pesa hawakupi sapoti ukitaka kudhibitisha hilo waangalie wanaojifanya wanabifu nae aina ya mashabiki walionao ( mfano halisi ni mlinzi wa tembo ) asante Kidingi kwa uzi mzuri sana kwa ajili ya Icon wetu.
ukweli kabisa mkuu...
 
Last edited by a moderator:
Ila binafsi nimefurahi jamaa ametoa audio na video zote muda huo huo,,,ebana nimeshazidownload zote tayari..naona kuna tangazo la Dr.Mwaka kama umecheki video kwa youtube naamini ni ule uvumi wa milioni 50 alizopewa ila bongo kuna watu wanaweza kutumia fursa vizuri aiseee...daahh
 
Huyu jamaa inatakiwa awe anatoa wimbo muda tofauti kidogo na wenzake maana anafanya watu wawazie Utanipenda tu na kusahau nyingine ndio maana dimpoz na FA walisogeza mbele siku za kutoa nyimbo zao
 
Hakika amna msanii bongo hii kama platinum nathubutu kusema utimu utimu mala utimu kiba sio mzur must tumsaoti ili mziki wetu uendelee kukua si wenyewe tunajionea mambo anayo fanya
 
Mambo anayo fanya platinum there is no any musician in bongo do something like these and big up broo
 
Huyu mwenye huu mjengo kapiga pesa. Wizkid Baba Nla & Diamond Utanipenda.. naona location south africa zinazidi kuisha
 

Attachments

  • 1450007894588.jpg
    1450007894588.jpg
    106.4 KB · Views: 120
Huyu mwenye huu mjengo kapiga pesa. Wizkid Baba Nla & Diamond Utanipenda.. naona location south africa zinazidi kuisha

Duuuuh noma sana... sema itakuwa walipaelewa sana hapo, ila nyumba kali zipo nyingi tu haziwezi kuisha..!!
 
Duuuuh noma sana... sema itakuwa walipaelewa sana hapo, ila nyumba kali zipo nyingi tu haziwezi kuisha..!!

Madirector kazi wanayo. Unajua niwasanii weng sana wa Nigeria na Tz wanafanya videos kule + wasouth wenyewe na directors wazur wako kule kwaio ni challenge sna inapokuja swala la locations
 
Back
Top Bottom